Kwa uelewa wangu mtoto anaweza kuwa na hasira sababu kuu zikiwa mbili.
1-wakati mama akiwa mjamzito hamkua na mawasiliano mazuri hiyo ikamfanya mwanamke kuwa na hasira muda mwingi na stress zisizoisha,hii humuathiri mtoto moja kwa moja,tiba hapa ni kuwa karibu na mtoto na kumwonyesha upendo ili kupunguza msongo aliozaliwa nao.
2-Malezi limekua tatizo kubwa,unamlea mtoto kama yai,lazima ujue mtoto anaanza kuwa na utambuzi akiwa na miezi 4 mpaka 5 pale anapoanza hata kuchagua watu wa kumbeba,ukichunguza kipindi hicho akifanya kitu kibaya ukimfoka atalia au ataogopa na hapo ndo tunapofanya makosa,mtoto anakosea kitu hata kumwonyesha kwamba hakufanya vizuri unamwacha ukijidai bado mdogo,tabia hukuzwa,nimekuwa na jirani yangu ana kitoto kina mwaka na nusu kina tabia mbaya sana,kinampiga makofi mama yake,kina kiburi yani tabu tupu,ukimwambia mbona mwanao hivyo anasema bado mdogo ataacha,mpaka majirani hawataki acheze na watoto wenzake,akikosea ukamfoka au kumfinya umenunua kesi kwa mama yake,mnakosana kabisaa,me binafsi nina kijana ana mwaka na nusu ila anajua kwamba hiki baba hataki na hiki nitafinywa na mama yuko well kabisa,ila kwa kosa ambalo najua umri wake bado huwa natafuta namna ya kumsaidia,sio unaona kitoto kinavuruga nyumba kinagombana na wenzake na matusi juu bado unasema akikua ataacha pole.