Mkuu hilo suala limekaa kisaikolojia zaidi, binafsi nakushauri kama utapata muda wa ziada mpeleke kwa wataalamu wa saikolojia watakupa ufumbuzi wa maana.
Mpeni vitu anavyovihitaji kwa wakati.....hata mimi huwa nauzika nikiwa nataka kitu lakini sikipati kwa wakati......hasa hasa nikiwa na njaa....na ndio ulikuwa ugomvi mkubwa kati yangu mimi na mama.....
Dah, mimi nina dume langu lina miaka 2 linasumbua kweli mpaka wakati mwingine inabidi nilichape! Lina dada yake ana miaka 4 huwa linamfanyia fujo hadi anabaki analia tu mda wote yaani tabu tupu! Ngoja tuone I hope kadri linavyokua litatulia!
Ana mapepo.
Ndugu wana-Jamvi,
Mwanangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi nane lakini anakabiliwa na tatizo la kuwa na hasira hasa pale anapoona amecheleweshewa kupewa kitu mfano kama uji au juice.
Unaweza kumpa juice ikiisha anakitupa kikombe au chupa au anaenda kwenye kabati anatoa kikombe anakipasua basi roho yake inakuwa imetulia. Sasa jambo hili linanipa wasiwasi endapo ataendelea kuwa na hasira za namna hii.
Kama kuna tiba yoyote naombeni msaada.
Ndugu wana-Jamvi,
Mwanangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi nane lakini anakabiliwa na tatizo la kuwa na hasira hasa pale anapoona amecheleweshewa kupewa kitu mfano kama uji au juice.
Unaweza kumpa juice ikiisha anakitupa kikombe au chupa au anaenda kwenye kabati anatoa kikombe anakipasua basi roho yake inakuwa imetulia. Sasa jambo hili linanipa wasiwasi endapo ataendelea kuwa na hasira za namna hii.
Kama kuna tiba yoyote naombeni msaada.
Chapaaa_
Mimi nilikuwaga na hasira za namna hiyo, sitashangaa mwanangu wa kiume akiwa nazo. Ila nilitandikwaga aisee...hasira zenyeweee.
Fimbo na Maonyo hutia hekima, Bali mwana "alieachiliwa" (sasa hapo Neno linamaana kubwa) ni mzigo wa mamaye,
Quoted from Mithali (sikumbuki ngapi)
Tafuta kisu au kiwembe, akivunja kikombe au gilasi mweke chanjo/chale usoni kama ya wamakonde halafu msogezee kioo ajione. Kama atapenda kuona chanjo/chale hizo zinavyoengezeka na zinavyopamba uso wake ataendelea kuvunja, vyenginevyo ataacha kihererehere,kisirani kitayeyuka na hasira zake zitaisha..Ninajaribu kufanya hivyo ila anabaki na kisirani
nenda kaonane na daktari wa magonjwa ya akili kwa watoto, mwanao inaelekea ana tatizo. serious mkuu maana kwa hasira hizi ukipata mtoto mwingine si utakuta keshamchoma kisu cha tumboni? achana na ushauri wa kienyeji mara mapepo mara nini. sisi waafrika tuliweka mbele sana imani za kishirikina ndio maana hatukundelea. pia achana na habari ya kumpiga mwanao, inampa unyonge na matatizo ya kisaikolojia ambayo yatamsumbua maisha yake yote zaidi sana ukubwani, atakua ni mtu asiyejiamini na mnyonge. jiulize kwanini wazungu hawawapigi watoto wao lakini bado wanakua na kua watu wazuri wenye akili? as a young generation we are supposed to leave the old school of thoughts "corporal punishment" also we are required to think critically and not to be judgemental
Tafuta kisu au kiwembe, akivunja kikombe au gilasi mweke chanjo/chale usoni kama ya wamakonde halafu msogezee kioo ajione. Kama atapenda kuona chanjo/chale hizo zinavyoengezeka na zinavyopamba uso wake ataendelea kuvunja, vyenginevyo ataacha kihererehere,kisirani kitayeyuka na hasira zake zitaisha..
Unataka kusema wamakonde na wanaojitia tatoo wanafanya abuse?......sasa huku ni kumuabuse mtoto, seriously! Umkwaruze mtoto na viwembe? Huu ni uonevu.