Thanks mkuu ubarikiweUdongo uwahi ungali maji/mbichi. Huyu mtoto unatakiwa umdhibiti kabla hivyo anavyovifanya havijawa tabia, mazoea au kawaida.
Siku akifanya huo ujinga hebu chukua kafimbo mtandike na umwambie hiyo tabia ni mbaya na asirudie tena. Pia mwambie madhara ya kuharibu vitu nini ili aelewe ni kwa nini umemwadhibu. Pia siku kakikililia uji mweleze avumilie wanamwandalia atulie. Baadae katakuja kuwa kasumbufu kwani hakana subira, inaweza kupelekea kwenye udokozi kwani hawezi kusubiri maana anataka muda huo huo apate anachotaka. Hili nalo si dalili njema kwa mwanao idhibiti mapema.
Huyu mtoto dhibiti mapema hizo tabia zote mbili anazoonyesha sio njema kabisa.
Ninajaribu kufanya hivyo ila anabaki na kisirani
Kama baba yake mtoto ni mkurya kazi ipo.Ni kopi ya mura hiyo.
Hasira ni kitu cha kawaida.Ila kama anaanza kuvunja vitu (destructive anger) hapo inabidi uanze kumdhibiti mapema kwa kumwonyesha umechukia na kumvuta aisifanye kile atakach😵f course atalia sana ukimvuta na kumzuia anachotaka kufanya lakini baadaye akivutwa vutwa mara nyingi ataacha.usimpe nafasi ya kutekeleza azima yake akiendelea hivyo atakuja haribika mno mbeleni.
Ila akikua kidogo ni vizuri kuanza kumchapa kidogo kidogo anapokosea ili ajue kila kosa lina adhabu.Ataacha hivyo vi hasira koko vyake na akikua ataogopa kulipuka hasira mno akijua kuwa atashughulikiwa kama mzazi ulivyokuwa ukimshughulia.Usipomshughulikia atakua akijiona yeye mfalme anayeweza fanya chochote na asifanywe chochote.Ndio maana adhabu muhimu hasa kwa mtoto anapokuwa mdogo anapokosea.
Tabia ni moja kati ya traits ambazo mtoto hurithishwa kutoka kwa wazazi, hivyo hasira kama tabia nayo mtoto hurithi...
Pia inaaminika kuwa watoto wa kiume huwa na tabia ya kufanya vurugu za hapa na pale wanapokuwa wakikua, kuvunjavunja vitu ni moja ya vurugu hizo...
Je mwanao ni jinsia gani?
Kama ni wa kiume basi kwa sasa ni ngumu kujua kuwa hicho alichonacho ni tabia ya hasira auni sehemu tu ya ukuaji?
Ndugu wana-Jamvi,
Mwanangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi nane lakini anakabiliwa na tatizo la kuwa na hasira hasa pale anapoona amecheleweshewa kupewa kitu mfano kama uji au juice.
Unaweza kumpa juice ikiisha anakitupa kikombe au chupa au anaenda kwenye kabati anatoa kikombe anakipasua basi roho yake inakuwa imetulia. Sasa jambo hili linanipa wasiwasi endapo ataendelea kuwa na hasira za namna hii.
Kama kuna tiba yoyote naombeni msaada.
Ana mapepo.