Msaada: Mtoto akijisaidia utumbo unatoka nje

Msaada: Mtoto akijisaidia utumbo unatoka nje

makenze

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
356
Reaction score
217
Mtoto wa jirani yangu anaugua ugonjwa akijisaidia utumbo unatoka nje.
Ana miaka mitatu.

Ila kikubwa jirani hana uwezo wa matibabu sababu hata kujua mtoto tatizo lake linahitaj upasuaji mimi ndo nimemwambia baada ya kuuliza huku na huku.

Ameshaenda hospitali lakini anadai bado dogo anatoa utumbo nje.

So kama.kuna daktari humu wa kutoa msaada huo namuomba hata kumfata inbox au hapa kwa msaada zaidi.

Kiukweli uwezo kifedha hana kabisa.
Ukijiona una matatizo subiri wenzio wakuhadithie yao.
 
nadhani itakuwa ni Bawasili na siyo utumbo unatoka nje.
kama ni bawasili huo ugonjwa unatibika kwa njia ya vidonge na tatizo likiwa kubwa sana basi anafanyiwa upasuaji mdogo tu.
 
Hiyo ni Rectal Prolapse (sehemu ya utumbo mpana kutoka nje).
Mara nyingi huwapata watoto wadogo kuanzia mwaka 1 - miaka 6.

Sababu zipo nyingi, huwenda ikawa Parasitic au bacterial infection.

Cha kufanya ili kupata majibu sahihi na mtoto aweze kupona, ni kwa kufika kwenye kituo cha afya. Wao ndio watachukua vipimo na kujua tatizo linasababishwa na nini.

Kwahiyo msipoteze muda, fanyeni mumpeleke hospitali.
 
Nilisumbuka na mwanangu Kwa Zaid ya mwaka na usheee. Nilifika mpaka muhimbili kitengo cha magonjwa ya watoto sikupata majibu. Mpaka mama mkwe alipotoa ushaur wa kumtahiri mtoto. Toka ametahiriwa hajawahi pata tena hiyo kitu huu mwaka na nusu sasa
 
MalcolM XII, Naungana na wewe

Ni kweli kabisa kwa utafiti uliofanywa na chuo Cha afya cha South Korea nchini Korea watoto kuanzia umri mwaka 1 mpaka 7 wapo katika hatari ya kupata rectal prolapse.

Afike kituo Cha afya kwa uchunguzi zaidi maana akiendelea kukaa inaweza kumletea madhara makubwa zaidi.

Sometimes tunatoaga dawa ANUSOL SUPPOSITORY kutibu ugonjwa Kama huo lakini kitaalamu haturuhusu kutumia dawa pasipo kuambiwa na mtaalam wa afya ili kuepuka usugu wa dawa.


By: NGAYONGA DANIEL
 
Nilisumbuka na mwanangu Kwa Zaid ya mwaka na usheee. Nilifika mpaka muhimbili kitengo cha magonjwa ya watoto sikupata majibu. Mpaka mama mkwe alipotoa ushaur wa kumtahiri mtoto. Toka ametahiriwa hajawahi pata tena hiyo kitu huu mwaka na nusu sasa
wa wa kike ingekuwaje sasa
 
Back
Top Bottom