Kwanza afanye kazi moja tu ya malezi kwa Sasa, akubali mengine yampite tu
Anaweza kuendelea kumnyonyesha vizuri tu, hadi pale mimba ikifikia miezi 7 ndipo amuachishe, muhimu ahakikishe anajali ulaji wake na huyo mtoto maana mwaka anakuwa anakula vyakula laini,(chakula Bora)
Iliwahi kunitokea hiyo Tena mtoto akiwa na miezi 5 nikanasa, niliendelea kunyonyesha mpaka ujauzito ulipofikia miezi 8 na wiki 1 nikamuachisha hakuwa tahira wala chochote, na bado wote watatu tulikuwa wenye afya safi tu na nilizaa mtoto mwenye kg 4.4 sikutumia dawa yoyote ya mitishamba,
Zingatia haya;
βUsafi Ni muhimu sana
βLishe Bora kwa mama na mtoto
βKwa vile mtoto ni mkubwa anaweza kumlisha zaidi mchana halafu usiku ndipo anyonye
βUkaribu wako kwa mkeo unahitajika zaidi wakati huu
βAkiugua amuwahishe kupata matibabu
βKauvivu kamimba ajitahidi kukapuuzia maana hako ndiko huleta uchafu, mtoto kutokula kwa wakati hivyo kupelekea mtoto kuugua mara kwa mara na mwishowe ni kifo
Kila la heri baba kijacho, msalimie mama kijacho