Msaada mke wangu kabeba mimba akiwa bado ana mtoto anayenyonya je anaruhusiwa kumnyonyesha?

mimiks

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
1,374
2,000
Anaweza kunyonyesha mpaka mimba ikifika miezi sita. Ila pia mtoto wa mwaka mmoja anaruhusiwa kunywa maziwa ya ng'ombe anaweza akamuachisha kama ana hofu au mimba kama inamsumbua kwenye kula vizuri maana anatakiwa ale chakula vizuri kwa ajili ya mtoto wa tumboni na anaye mnyonyesha.
 
Sep 11, 2011
22
75
Mimi ilinitokea hivo lakini mtoto aliacha kunyonya mwenyewe(ladha ilibadilika), sidhani Kama ni sahihi kuendelea kumnyonyesha huku Ana mimba ingine, hapo box zinakuhusu, kuna umri akifika unampa ya ng'ombe tu
 

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,599
2,000
1. Haina shida yoyote kisayansi, mtoto anaweza kuendelea kunyonya tu, hata hadi mimba ikifika miezi 8 kulingana na nguvu zake.

2. Mkeo atahitaji virutubisho (nutrients) za kutosha ili aweze ku meet demand ya kinachokua kwenye kizazi chake na huyo anaenyonya;Ale vyakula vya protini kwa wingi sana pamoja na mboga za majani ma matunda.

3. Usisikilize uzushi wa mitaani ambao hauna ukweli wa kisayansi. Zingatia zaidi ushauri wa watoa huduma za afya mnapoenda kliniki, na msisite kuwauliza maswali pale mnapokua na utata au hamjaelewa kitu.
 

Noelia

JF-Expert Member
May 26, 2017
14,642
2,000
Kwanza afanye kazi moja tu ya malezi kwa Sasa, akubali mengine yampite tu

Anaweza kuendelea kumnyonyesha vizuri tu, hadi pale mimba ikifikia miezi 7 ndipo amuachishe, muhimu ahakikishe anajali ulaji wake na huyo mtoto maana mwaka anakuwa anakula vyakula laini,(chakula Bora)

Iliwahi kunitokea hiyo Tena mtoto akiwa na miezi 5 nikanasa, niliendelea kunyonyesha mpaka ujauzito ulipofikia miezi 8 na wiki 1 nikamuachisha hakuwa tahira wala chochote, na bado wote watatu tulikuwa wenye afya safi tu na nilizaa mtoto mwenye kg 4.4 sikutumia dawa yoyote ya mitishamba,

Zingatia haya;
✓Usafi Ni muhimu sana
✓Lishe Bora kwa mama na mtoto
✓Kwa vile mtoto ni mkubwa anaweza kumlisha zaidi mchana halafu usiku ndipo anyonye
✓Ukaribu wako kwa mkeo unahitajika zaidi wakati huu
✓Akiugua amuwahishe kupata matibabu
✓Kauvivu kamimba ajitahidi kukapuuzia maana hako ndiko huleta uchafu, mtoto kutokula kwa wakati hivyo kupelekea mtoto kuugua mara kwa mara na mwishowe ni kifo

Kila la heri baba kijacho, msalimie mama kijacho
 

Paroco

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,984
2,000
Ndoa za watoto hizo.
Kwaani hamkuseminishwa hata clinic tuu!!?😂😂😂😂

Mnyonyesheni afe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom