Msaada: Mchepuko umenipa gono, zinaa sasa basi

Msaada: Mchepuko umenipa gono, zinaa sasa basi

DOGofGOD

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
1,341
Reaction score
480
Amani kwenu wadau wa MMU

Nilikua nimejipumzisha zangu gheto leo jioni mida kama ya saa12 hivi mara nasikia grrrrrrrrrrrrrr!..simu inaita.Kuichungulia kumbe ni demu wangu mmoja nilimgegedua jumapili iliyopita.Demu mwenyewe ni kama mchepuko flani hivi na sio yule shemeji yenu wa ukwe..e mnaemfahamu.Maongezi yetu yalikua kama ifuatavyo

"Baby mimi mwenzio naumwa" ~ "unaumwa nini baby wangu?""kuna vitu naviona uku chini vinantoka lakini sivielewielewi.mwanzoni nilidhani labda niko kwenye red.lakini naona vitu vyeupe vyeupe ambavyo sijawai kuviona" ~ "mmmmmh!..ndo vitu gani tena hivo baby mbona sikuelewi?"

"Hata mimi sielewi baby na hata nikikojoa mkojo unauma sana" ~ "mmmmmh!.pole baby sasa kwanini hujaenda hospitali?""hospitali nimeenda ila wamenambia ni ugonjwa ila hawajanambia ni ugonjwa gani na wamesema hawawezi kunipa matibabu mpaka twende wote mimi na wewe" ~ "mmmmmh!..baby matibabu mpaka twende wote?"

"Ndio baby wamenambia nije na mpenzi wangu ili tutibiwe wote kwasababu kama nikitibiwa peke yangu nikapona badae nikija kukutana na mpenzi wangu ugonjwa utarudi tena kwahiyo itakua kazi bure" ~ "mmmmmh! baby mimi sitaweza kwenda ila we nenda ukatibiwe na wakikuuliza mpenzi wako yuko wapi waambie amesafiri kikazi"

Maongezi yetu yalikua marefu kidogo ila nimejaribu kuelezea tu kwa kifupi.Kwasababu najua wengi wetu humu ni magreat thinkers kwahiyo akili zetu uwa zinajiongeza zenyewe.Na kwa jinsi ya maelezo ya huyu demu inaonekana ana gono na nahisi tayari ameshaniambukiza.Hivi jamani haya magonjwa bado yapo tu.

Manake nna mda mrefu sana sijayasikia.Istoshe magonjwa ya zinaa mimi binafsi nayaogopa sana.Lakini akili yangu kichwani inawaza zaidi isije ikawa huyu demu kashaniungia kitu cha mtera.Kwasababu inaonekana huyu demu ana mambo mengi sana.Kalitoa wapi ili gonjwa?Nimeamua kutupia uzi huu kwasababu najua wadau wengi watajifunza kitu apa unless uwe na kichwa kigumu kama cha Shy Land au Lala1

Kwa leo sitaki kuwachosha sana ila ningependa kushare na nyie mambo muhimu yafuatayo:
Kwanza kabisa nahitaji sana maombi yenu.Kama huyu demu ni wakala wa Tanesco basi maombi yenu yatasaidia ili hii gridi ya taifa iruke iki kijiji changu.Manake apa nilipo wadau sio siri sielewi.Presha inapanda presha inashuka.Kwasababu mimi binafsi inshu yeyote inayohusu magonjwa ya ngono uwa inantisha sana.

Pili ni ushauri wangu kwenu wadau.Jamani haya mambo ya kujifanya vidume vya mbegu na hivi vitabia vyetu vya kugegedagegeda tu ovyoovyo tena bila ya kutumia kinga vitatumaliza.Magonjwa ya zinaa yapo na mbaya zaidi gridi ya taifa ipo live mtaani inatafuta kuunganisha wateja wapya.Mpaka sasa bado sijaenda kupima lakini kwa maombi yenu nikilipata hilo gono ntashukuru sana na ntarudi humu kuwashukuru kwasababu ni bora kuliko hilo gonjwa jingine.Zidisheni tu maombi.

Kwa hili tukio la leo nahisi kama islaeli ananibeep kwa mbaaaali.Kwahiyo kwasababu bado najipenda.Kuanzia leo natangaza rasmi mimi na uzinzi basi,michepuko sio dili na Tanzania bila ukimwi inawezekana!!Mwisho nawaombeni wadau wa MMU kwa yeyote anaejua dalili za awali za hili gonjwa anijuze kwasababu mpaka sasa bado sijaanza kusikia dalili zozote.

Nataka nikiona dalili yeyote niwai haraka kwenda kupata matibabu.Please guys kwa wale vichwa ngumu ambao swala la kubadili tabia ni halamu kwao.Basi wajitahidi kuishi kwa kuzingatia ABC za afya ya uzazi.Abstaining, Be faithful, Condomising.

Miss chagga,
madame B,madame S,madammeX, heaven on Earth,shy land,lala1,kikulachochako,apologise lady,honey faith,watu8,ruttashobolwa,tee bag,evelyn salt,king'asti,TUPACified,M011,tamalisa,mshanar jr,warumi, na wadau wengine mmeipata hii,dawa ni kubadili tabia tu vinginevyo TB itatumaliza wengi.Anaekufa na TB sio fara ila ni kwasababu ya haya haya masihara yetu ya kila siku.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wadau.Naomba kuwasilisha!
 
Kwahiyo kwako matumizi ya Kondomu yamekupita kushoto mwenzetu?
 
That's great.

Great because that's the comeuppance you get for two-timing your significant other.

It doesn't get any better and fairer than that!
 
Hebu nisimulie.......eti kapata gono......?........gono bado ipo karne hii.........?

Hata Mimi Nashangaa Jamani.Mimi Nilidhani Haya Magonjwa Yalishafutikaga Kenye Ramani.Mara Ya Mwisho Kuyasikia Ilikua Mwanzoni Mwa Miaka Ya 90.Sasa Sijui Kalifukunyua Wapi
 
Na majuto ni mjukuu....

Mpigie simu umuulize hospital wamemwambiaje... maendeleo yakoje.. mdodose dosose tu

Amenambia Yeye Amewabembeleza Na Wamemruhusu Aanze Matibabu.Ila Bdo Anataka Na Mimi Niende.Lakini Mimi Bado Sijaamua Kwenda Kupima.Kwasababu Akili Yangu Bado Haifanyi Kazi Vizuri.Na Wasiwasi Pia Na Shemeji Yenu Kama Nimempa Sijui Ntamwambia Nini.Kusema Kweli Ntaumbuka.Na Sijui Atachukua Maamuzi Gani.
 
Kama ni mchepuko kwa nini hukuchukua tahadhari, au condom zinakupwaya?
Inawezekana wewe ndo umempelekea, kuna fangasi za candida unahamisha kutoka kwa mchepuko mmoja kwenda mwingine maana hawastawi vizuri katika maumbile ya mwanaume hivyo wewe unakuwa mbebaji.
 
Rx Azithromycin 500 mg orally twice for 7 days &Doxycycline 100 mg orally twice a day for 7 days -for acute gonorrhea
 
Back
Top Bottom