Msaada: Matibabu ya Ulcerative Colitis

OTIS

JF-Expert Member
Sep 7, 2011
2,251
827
Habari wananzengo,

Mdogo wangu amekuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ulcerative Colitis tangu 2016 hadi leo. Ugonjwa huu unahusisha kujisaidia damu pale uendapo chooni. Tulimpeleka Aga Khan Hospital na baada ya kufanyiwa Colonoscopy, madaktari walijiridhisha kuwa anaumwa Ulcerative Colitis na sio Hemorrhoids.

Tangu 2017 hadi leo amekuwa anatumia dawa za hospitali ila bahati mbaya ugonjwa huu hauponi ila unatulizwa tu kama matumizi ya ARV kwa mwenye VVU.

Kupitia jukwaa hili nina amini kunaweza kuwa na watu walipitia changamoto kama hii au wanaojua matibabu mbadala ya ugonjwa huu.

Natanguliza shukrani.
 
Anaweza kufanyiwa surgery ya kukata utumbo mkubwa sehemu iliyoathirika na kuwekewa kipochi cha kujisaidia (colostomy).

Inategemea na ukubwa wa athari, wengine utumbo unaungwa tena na maisha yanaendelea na wengine hujisaidia kwenye kipochi maisha yao yote.
 
Anaweza kufanyiwa surgery ya kukata utumbo mkubwa sehemu iliyoathirika na kuwekewa kipochi cha kujisaidia (colostomy).

Inategemea na ukubwa wa athari, wengine utumbo unaungwa tena na maisha yanaendelea na wengine hujisaidia kwenye kipochi maisha yao yote.


Asante kwa ushauri ila hali haijawa mbaya kufikia kukatwa utumbo. Tatizo ni kutumia dawa za hospitali na anatafuta tiba mbadala kama zipo.

Akitumia dawa za hospitali anakuwa mzima kabisa na vipimo vinaonesha utumbo upo sawa kabisa.

asante
 
Ushauri mwingine ni chakula cha kuimarisha immune system, protein, broccoli na matunda.

Ushauri wako umepokelewa vyema.

Nina imani kuwa wadau wengine wanaweza changia pia hasa kwenye tiba mbadala.

asante
 
Pole Sana mie mwenyewe ni mhanga wa ulcerative colitis, nimeamua nifanye Mambo mawili tu
1 kula mboga za majani na matunda
2 mazoezi nipunguze weight kidogo

Pole kwa mdogo wetu
 
Pole Sana mie mwenyewe ni mhanga wa ulcerative colitis, nimeamua nifanye Mambo mawili tu
1 kula mboga za majani na matunda
2 mazoezi nipunguze weight kidogo

Pole kwa mdogo wetu

Pole pia na Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi.

Ushauri wako umepokelewa.

Asante sana
 
Kuna mbadala wake?
Hatuwezi kusema kuna mbadala..maana kuna dawa utapewa kutegemea na aina ya U.C uliyo nayo yaani Mild,Moderate au Severe..sasa unaweza kupewa dawa mfano aminosalicylates kama sulfazalazine au mesalamine na kukutokea remision unaandikiwa Prednisolone..

Matibabu ya hii kitu yapo complex kidogo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom