Msaada makadirio ya bei kwa kiwanja cha mita za mraba 210

RiOD

Member
Jul 10, 2020
20
2
Matumaini yangu mnaendelea vyema na maisha.

Mama yangu mpendwa aliyekuwa ananilipia ada chuo ameshindwa kufanya hivyo tena sababu ya uchumi kuwa mgumu kwake.

Alikuwa anajenga nyumba yake ambayo hajaimalizia. Kutokana na hali kuwa ngumu amenipatia nyumba hiyo rasmi na kuniambia niiuze Ili niweze kumalizia masomo yangu (bado miaka 4 nimalize chuo)

SWALI: Je wakuu kiwanja cha square meter 210 + nyumba iliyopauliwa tayari, haina madirisha wala milango (4 rooms, sebule + choo na bafu) naweza kuiuza kwa makadirio ya bei gani?

Location: MOSHI mjini.
 
Daaah!
Uuze nyumba kisa kwenda chuo?
Ambako huelewi mwisho wake ni upi?
Ukikosa mishe baada ya kumaliza chuo?

Tafakari upya mkuu. Hiyo nyumba inaweza ikawa ndo njia ya ww kutoboa endapo utatumia vizuri akili then inaweza ikawa ndio majuto yako milele
 
Matumaini yangu mnaendelea vyema na maisha.

Mama yangu mpendwa aliyekuwa ananilipia ada chuo ameshindwa kufanya hivyo tena sababu ya uchumi kuwa mgumu kwake.
Alikuwa anajenga nyumba yake ambayo hajaimalizia. Kutokana na hali kuwa ngumu amenipatia nyumba hiyo rasmi na kuniambia niiuze Ili niweze kumalizia masomo yangu (bado miaka 4 nimalize chuo)

SWALI: Je wakuu kiwanja cha square meter 210 + nyumba iliyopauliwa tayari, haina madirisha wala milango (4 rooms, sebule + choo na bafu) naweza kuiuza kwa makadirio ya bei gani?

Location: MOSHI mjini.
Huna wadogo zako? kama hauna ni sawa, ila kama wapo nao watapata share ipi, ?

Hauna wakubwa zako? kama hauna ni sawa ila kama wapo nao wana mchango gani kwako kukusomesha badala ya kumwachia mzazi jukumu hilo hadi afikirie kuuza nyumba?

Kwa nini unadhani ni sahihi kurisks mali ya familia nzima kwa ajili ya elimu yako peke yako? ikitokea elimu yako haikukupa matarajio unayotarajia ,huoni kuwa utakuwa umejiingiza kwenye lawama zisizokwisha na ndugu zako?.

Mama yako anakupenda sana kiasi.kwamba yupo tayari kupoteza nguvu zake zote kwa ajili ya maendeleo yako, ila elimu ya sasa sio Guarantee kuwa utapata returns za papo kwa hapo, Upendo huo unaweza kugeuka shubiri kadiri mtumbwi unavyozama , fuata ushauri wa mdau ambaye amesema unalizie nyumba mpangishe, then endelea na masomo kwa pesa za kodi , utachelewa kupata elimu lakini itakuwa far more safe kuliko route ya kuuza nyumba.
 
Mkuu moshi mjini Unaweza pata mteja na hela yakutosha kupata eneo Sehemu nyingine bado ukajenga na kulipa ada ya shule na chenchi ikabaki kubwa tuu, ni ushauri wangu binafsi
 
Angekuwepo mzee ungesikia maamuzi ya kiume .unataka uuze mpaka sasa hivi we unavingapi ?
 
Mkuu, achana na hesabu za kuuxa nyumba kwenda chuo. Utamaliza chuo kwa garama ya kuuza nyumva alaf huna mchongo utajilaum.

Kama upo tayari kuuza, bas mshuri mam hio nyumba mchukile mkopo benki ata M 10 za kulipa miaka ata mitano, then mfnye biashara ambayo mnawezakua mnarejesha kila mwezi roughly 300k.

Itawasaidia kujijenga kiuchumi zaid kuliko kuuza, & so long umefaulu, shule unaezaenda tu ata miaka mitano ijayo.
Hela ndo kila kitu mkuu.
 
Heeeh wa kwetu unataka uza nyumba, too bad
Anyway kwasababu Ni Moshi mjini, possibility ya kuuza kwa Bei kubwa ipo(hasa kiwanja Kama kipo sehemu nzuri) kanunueni nyumba or uwanja nje ya mji. Kasome kwa Budget ndogo,pesa ingine mama afanye Biashara kukpeleka 4years za masomo yako

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Acha chuo tafuta kazi au fanya biashara hata kama ni ndogo. malizia nyumba hiyo. Ikiisha weka wapangaji then tumia kodi kulipia ada. Shule sio sehemu nzuri kuweka kete zako zote. Angalia graduates walivyojaa mtaani.
Kazi/biashara sio rahisi kama unavyosema mkuu.
 
Back
Top Bottom