Msaada: Mafundi wazuri wa Nissan X-Trail

kinondoniilala

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
988
762
Wanabodi,

Leo asubuhi wakati nawasha gari yangu ya Nissan X Trail ikatoa muungurumo usio wa kawaida yake. Muungurmo wa gari uliotoa ni kama ule wa magari ya mashindano au kama ule unaofanana na Subaru Forester.

Nimeshindwa kuondoka nalo kwenda nalo ofisini imenibidi nilipaki nyumbani. Naomba kwa mtu anayejua mafundi wazuri wa Nissan X Trail QR 20 Model ya mwaka 2005 hususani upande wa Exhaust wanipe direction nikawaone.

Mimi nipo jijini Dar es Salaam, naishi Mbezi ya Kimara.

Nawasilisha.
 
Dahhh....
Kwanza naomba nikupe pole kwa adha ulio ipata leo kwa kutembea kwa miguu, pole sana kwa uchovu.
Pili naomba nikupongeze kwa kumikili gari huku unaishi Daslam.
Lakini nisikitike tu kwakusema kwamba sijui lolote kuhusu mafundi wala magari, hapa nilikuja kukupa pole na kukupongeza tu.
 
Issue ya exhaust pipe ni ndogo sana,tafuta garage yoyote hapo Mbezi watakurekebishia,ni kazi isiozidi nusu saa,labda tu iwe ni Muffler imepasuka hapo kidogo itakuchukua muda ila inarekebishika...
 
Nimejaribu kuliendesha jioni hii, naona bado muungurumo wa SUBARU FORESTER bado upo...hadi majirani wananiuliza nimebadilisha Exhaust

Umeshindwa kuondoka na gari kwa sababu ya mlio tu?? ilibidi uondoke nalo uwe unalisikilizia ili kujua ugonjwa. Wakati mwingine ni mvumo tu umetokea na ungeisha wenyewe... unalea gari kama yai... Kuna faida gani sasa kuwa gari!
 
Nimejaribu kuliendesha jioni hii, naona bado muungurumo wa SUBARU FORESTER bado upo...hadi majirani wananiuliza nimebadilisha Exhaust
Hiyo ni exhaust imetoboka au kuchanika au kufunguka ulipogonga mahali
peleka garage yoyote wakachomelee lkn chunga sana ukae karibu kwenye muffler kuna vitu wanachomoa au watakwambia wavitoe havifai kataa kabisa
Basi na mrejesho tuletee sio uwe mbali ili tujifunze NISSAN X
 
NITAREJESHA MKUU
 
twapeja nsaji twingija ng'wehu!

ule mkebe wenye kengele?
Dahhh....
Kwanza naomba nikupe pole kwa adha ulio ipata leo kwa kutembea kwa miguu, pole sana kwa uchovu.
Pili naomba nikupongeze kwa kumikili gari huku unaishi Daslam.
Lakini nisikitike tu kwakusema kwamba sijui lolote kuhusu mafundi wala magari, hapa nilikuja kukupa pole na kukupongeza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom