Msaada Madaktari!!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,691
2,000
Habari Jf Doctors,.


Nimekuwa na maumivu ya muda mrefu licha ya kufanya vipimo na tatizo kutoonekana,.


Upande wa kulia mwa mbavu ninahisi maumivu sana hasa pale ninapovuta hewa ndani, pia chini kabisa ya ubavu huu wa kulia nikibonyeza mbavu inauma sana mithili kama imevunjika,.

Nimeshafanya vipimo mbalimbali lakini bado tatizo halijaonekana badala yake daktari aliyenihudumia alinishauri nitumie dawa ya kukomaza mifupa iitwayo KoAct ambayo naona bado haijanisaidia kabisa,.

Pia nimeshafanya vipimo vya damu (Full Blood Picture ) na tatizo halijaonekana,.

Mimi ni mfanyaji mzuri wa mazoezi ingawa kuna muda nilisitisha kufanya mazoezi ila kwa sasa nimerejea katika mazoezi,.


Ninafanya mazoezi hali hii hutoweka kwa muda na kurejea baade,.


Tafadhali nahitaji ushauri wenu juu ya hili tatizo langu madaktari,.

Cc: MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom