Msaada: Mabinti hawa email zao zinafanana

Msaada: Mabinti hawa email zao zinafanana

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,317
Habari zenu wakuu.Mimi ni mtumiaji pia wa facebook.Kuna mabinti sasa wanafikia watatu ambao waliniomba niwe mshirika wao wa biashara kuwekeza nchini kwetu TZ.Kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiomba ushirikiano wa kibiashara.Lakini hadi hapa nimegundua yafuatayo:
1.Maelezo yao kwenye email yanafanana
2.Maeneo wanayojieleza kutokea yanafanana(Senegal,Siera Leon)
3.Sababu ya kuwa kambi za wakimbizi zinafanana(Baba zao walifariki na walikuwa viongozi wa serikali au wafanya biashara.)
4.Hawataki tuwasiliane kwa facebook ila kwa email tu.
Hao wote wametaka maelezo yangu binafsi,maisha na akaunti za benki ila sijawapa.Haya ni majina yao;Tina Thiara,Queen Thiara na Minnie Bagbo Sankawulo.
Ndugu zangu,huu mchezo unaitwaje na je niko salama?Kuna yeyote amewahi kukutana na majina hayo?Nahitaji msaada wenu zaidi hapo.
 
Mkuu hao ni wezi sana usiwape taarifa yako yoyote.
 
Matapeli hao ndg yng... Kuna mtu anajiita peace pia nae anataka detailz km hz.. Waongo haooo
 
Mbona hao wako wengi mkuu wala usije uka respond ni matapeli wakubwa. Tena wala sio mabinti ni madume ila yanatumia majina ya kike ili wakunase wakuibie vizuri. Mimi nimeshatumiwa nyingi sana hizo.
 
Mkuu hata mimi leo imenitokea hiyo binti anatoka senegal anaitwa Jennth Jobe, nimegundua ni wezi mkuu, hapa najipanga nimtukane!
 
Alafu eti anasema baba yao alipofariki alimwambia ana dolla mil.6 ziko kwenye benk ya Standard Chartd ya Uingereza kwa hiyo wamemwambia atafute mtu mwaminifu wa ili azichukue hela zake mimi atanipa 20% alafu zilizo baki tunawekeza huku kwetu au kwao pia kuanzia sasa ananichukulia kama baba huku akiniita my love, huku akinibembeleza nimsaidie!
 
mwambie kauli mbiu yetu ni"piga tu" asije akapotezwa,,,,,mwosha huoshwa na wewe waoshe sio lazima uibiwe ww ven ya unaweza
 
umewahi kusikia utapeli wa mtandaoni wewe?

kimbia na usigeuke nyuma.
 
Back
Top Bottom