Wewe nakuona kama nabii kwani unayoyasema yako hivyohivyo.Hao sio mabint ni madume, hutumia majina mazuri ya kike ili wawaibie wanaume wazembe.
Ukiangalia wote hutaka uwape email yako wakijifanya hawana muda wa kuwa fb. Mi nishawazoea ukifungua profile zao utakuta kapicha kamoja au tuwili pia utakuta ana friends wasozidi 5.
Ukiwa makini utagundua hii account magumashi tupu. Majina yao wengi from West Africa.
Awake my fellow members!
Mkuu hata mimi leo imenitokea hiyo binti anatoka senegal anaitwa Jennth Jobe, nimegundua ni wezi mkuu, hapa najipanga nimtukane!
Habari zenu wakuu.Mimi ni mtumiaji pia wa facebook.Kuna mabinti sasa wanafikia watatu ambao waliniomba niwe mshirika wao wa biashara kuwekeza nchini kwetu TZ.Kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiomba ushirikiano wa kibiashara.Lakini hadi hapa nimegundua yafuatayo:
1.Maelezo yao kwenye email yanafanana
2.Maeneo wanayojieleza kutokea yanafanana(Senegal,Siera Leon)
3.Sababu ya kuwa kambi za wakimbizi zinafanana(Baba zao walifariki na walikuwa viongozi wa serikali au wafanya biashara.)
4.Hawataki tuwasiliane kwa facebook ila kwa email tu.
Hao wote wametaka maelezo yangu binafsi,maisha na akaunti za benki ila sijawapa.Haya ni majina yao;Tina Thiara,Queen Thiara na Minnie Bagbo Sankawulo.
Ndugu zangu,huu mchezo unaitwaje na je niko salama?Kuna yeyote amewahi kukutana na majina hayo?Nahitaji msaada wenu zaidi hapo.
Aende nao mwishoni starling awe yeye
utapigwa hela bure kaka hao ni wasanii tu.
Nalog off