Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,672
- 2,697
Bila Shaka mu wazima wa Afya. Mungu mkubwa.
Mpaka wakati huu naandika 'Post' hii, nimekuwa natafakari nilichoota usiku wa kuamkia leo. Si ndoto ya kutisha, La hasha, lakini imefanya nitafakari sana, nadhani yeyote angetafakari kama angelitilia maanani.
Ni hivi; Mazingira niliyootea yana mandhari ya Shule, naam, shule, na ni katika ngazi ya Elimu ya Upili ya Sekondari, yaani 'Advanced', katika eneo ambalo, linaakisi Mazingira yasiyo ya mjini, Pasi na shaka ni kijijini, au mji unaokuwa hivi sasa. Kwa kuweka sawa, elimu hii nilisoma mkoani Ruvuma, hivyo najaribu kupafananisha na mazingira niliyootea.
Basi bwana, katika eneo moja, la ninchodhani ni shule, tulikuwa kwenye foleni ndefu, inafanana na foleni ya chakula, sina hakika mbeleni kilikuwa kinatolewa kitu gani, sikumbuki, ila nahisi kwa 80% ni chakula.
Nafasi yangu haikuwa nyuma sana, wala mbele sana na zoezi lilipokuwa likiendendelea, lakini kwenye mstari huo hapakukosa stori za hapa na pale na wale waliosimama mbele na nyuma yangu, nikiangalia mstari, Alhmadullilah, ulionyesha nakaribia kufika, nikigeuza kichwa niendelee na soga na wale mabwana, ambao kwa maumbile na namna walivyo ukilinganisha na tulichokuwa tukizungumza iliashiria kwamba ni Wanafunzi, kisha niangalie tena mbele nilikuta foleni inazidi kuwa ndefu, na pale zoezi lilipokuwa likiendendelea pako mbali na macho yangu.
Nilisimama kwenye foleni tu, sina kumbukumbu vizuri, kama wale niliokuwa napiga nao soga awali, ndio hawa hawa niliowakuwa nao wakati yote yakiendelea, lakini hali hii ya kukaribia kwenye 'Lile zoezi' na kukuta mbele watu wamejaa zaidi.
Basi katika tukio moja nalokumbuka ni kwamba, kuna bwana alijaribu kujipenyesha kwenye mstari, nadhani ni kama mtu wa pili kutoka nyuma yangu hivi, alisemwa yule bwana, alisakamwa, ikambidi aepuke lile nongwa, akakaa pembeni akingoja. Hiki ni kati ya kisa nakikumbuka kwenye ile ndoto.
Karibuni kwa Msaada wa Ufasiri.