Msaada: Maana ya ndoto hii

Msaada: Maana ya ndoto hii

Mama kama ni mama mzazi ni kama kumwona Mungu, maana ukiacha Mungu kuumba mama ndio anaewakilisha uumbaji wa Mungu duniani.Amekwambia kwenye maisha matatizo ni kawaida.
Kuna misukosuko ya kiasili au ya kiungu ilipata kutokea au itatokea.Kuna jambo linamhusu mkeo lakini hamlijui ndo maana baadae humwoni anakupotea.Mji mwingine ni ishara ya dhoruba inayosababishwa na watu ambao si jamaa zako yaani ndugu.
Mvua ni dhoruba ila nguvu kuu za kikarama zimekuepusha kama zilivyokuepusha kwenye dhoruba ya kwanza.Mti mkubwa kukudondokea ni Mtu mkuu aliyetaka kukudhuru au kukuponza, umemzidi lakini jiwe ni jaribio jingine la mtu mbishi na mkatili Mungu akakukwepesha tena.
Mwisho mama akadhihirisha tena ndie alikuzaa na ndie mwenye haki na yanayokuhusu, na si vinginevyo.Mwanamke anawakilisha jambo jema lakini lenye vikwazo vya kiuadui na chuki.
OgaBoy
 
Ndoto hazinaga maana yeyote ok labda kwa wachache humaanisha

Ndoto yeyote ukihadithiwa utaona ina tafsiri tu hata mtu akitunga "nimeota nimeona mawe makubwa kuna maji yanamwagika" ukiwaeleza watu watasema sijui hayo maji yanaamisha kushuka kwa maisha yako sijui bla bla kibao
 
Shida ni kwamba watu wanafuata kanuni ukishasema ni ndoto, watu watachambua ulivyovitaja kwa kutumia kanuni za kiroho na kimaono.Kama unadanganya ni wewe na udezi wako.Kama ilivyo hesabu na ndoto zina hesabu zake.
 
Bila Shaka mu wazima wa Afya. Mungu mkubwa.

Mpaka wakati huu naandika 'Post' hii, nimekuwa natafakari nilichoota usiku wa kuamkia leo. Si ndoto ya kutisha, La hasha, lakini imefanya nitafakari sana, nadhani yeyote angetafakari kama angelitilia maanani.

Ni hivi; Mazingira niliyootea yana mandhari ya Shule, naam, shule, na ni katika ngazi ya Elimu ya Upili ya Sekondari, yaani 'Advanced', katika eneo ambalo, linaakisi Mazingira yasiyo ya mjini, Pasi na shaka ni kijijini, au mji unaokuwa hivi sasa. Kwa kuweka sawa, elimu hii nilisoma mkoani Ruvuma, hivyo najaribu kupafananisha na mazingira niliyootea.

Basi bwana, katika eneo moja, la ninchodhani ni shule, tulikuwa kwenye foleni ndefu, inafanana na foleni ya chakula, sina hakika mbeleni kilikuwa kinatolewa kitu gani, sikumbuki, ila nahisi kwa 80% ni chakula.

Nafasi yangu haikuwa nyuma sana, wala mbele sana na zoezi lilipokuwa likiendendelea, lakini kwenye mstari huo hapakukosa stori za hapa na pale na wale waliosimama mbele na nyuma yangu, nikiangalia mstari, Alhmadullilah, ulionyesha nakaribia kufika, nikigeuza kichwa niendelee na soga na wale mabwana, ambao kwa maumbile na namna walivyo ukilinganisha na tulichokuwa tukizungumza iliashiria kwamba ni Wanafunzi, kisha niangalie tena mbele nilikuta foleni inazidi kuwa ndefu, na pale zoezi lilipokuwa likiendendelea pako mbali na macho yangu.

Nilisimama kwenye foleni tu, sina kumbukumbu vizuri, kama wale niliokuwa napiga nao soga awali, ndio hawa hawa niliowakuwa nao wakati yote yakiendelea, lakini hali hii ya kukaribia kwenye 'Lile zoezi' na kukuta mbele watu wamejaa zaidi.

Basi katika tukio moja nalokumbuka ni kwamba, kuna bwana alijaribu kujipenyesha kwenye mstari, nadhani ni kama mtu wa pili kutoka nyuma yangu hivi, alisemwa yule bwana, alisakamwa, ikambidi aepuke lile nongwa, akakaa pembeni akingoja. Hiki ni kati ya kisa nakikumbuka kwenye ile ndoto.

Karibuni kwa Msaada wa Ufasiri.

Ndoto yako inashiria upo gerezani ukisubiri chakula, jihadhari usifanye makosa utaenda gerezani
 
Kuna ndoto nimeota usiku wa kuamkia leo, kwakweli najiuliza maswali mengi na sipati majibu. Na haijawahi kutokea before.

Nimeota natembea (Sio porini) lakini cha kushangaza njiani nikawa nakutana na nyoka waliokwisha uliwa, yaani napiga hatua moja ya pili nyoka hawa, yaani ni kama njia nzima wamezagaa nyoka waliouawa.
Hivyo ikanilazimu niwe natembea kwa tahadhari ili nisikanyage nyasi ama vishimo (kulikuwa na vishimo vidogo vidogo) kwa kuhofia kunaweza kukawa na nyoka walio hai wasije nidhuru.

Naombeni msaada wa ndoto hii.
Yeee!! Niliwahi ota napaa, na halafu chini kuna watu wakawa wananikimbiza, ni kundi la watu, nikaja kupaa nikaenda mpaka juu ya mti mrefu, kule pia nikakutana na Nyoka walikuwa wamekufa wote, yaani ukitikisa tawi, yanaanguka. Ni noma
 
Japokuwa hujasema hali yako ya maisha kwa sasa ikoje...I mean unasoma, unafanya kazi, biashara na kipato chako kipoje, kuota upo shule wakati ulishamaliza shule siku nyingi maana yake ni "kurudishwa nyuma" kuwa kwenye foleni ambayo haufiki maana yake ni "kucheleweshwa" ukichukua maana ya kwanza (kurudishwa nyuma + Kucheleweshwa) utagundua kuwa kuna nguvu zinapambana na wewe ktk kile unachokifanya sasa, chukua taadhari na mwombe sana Mungu akuvushe!! kitu chochote kinachotokea kwa mtu huanza ktk ulimwengu wa "roho" then matokeo yake huonekana ktk ulimwengu wa mwili
Na hii ndio maana halisi ya ndoto hiyo.
 
Ahsante sana kwa ufafanuzi.

Niliwahi kuota ndoto kama hii, tulikuwa tupo kwenye foleni ya msosi ikulu, nilikuwa kama mtu wa 3 hivi, ilipofika zamu yangu, Rais wa nchi wa wakati huo alikuwa amekaa table yenye msosi akanizuia kupakua msosi huo (ilikuwa nyama) akaniambia kwa ishara nikae pembeni ya foleni, waliofuata nyuma yangu walipakua msosi. Nilibaki mnyonge sana. Ndoto hii asubuhi nilipoamka niliikumbuka vyema kabisa. Sikuipata maana yake.
 
Daaaah!! Ikuluu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom