Msaada: Laptop yangu inagoma kuwaka

Msaada: Laptop yangu inagoma kuwaka

Joined
Oct 13, 2016
Posts
94
Reaction score
21
Ndugu wana Jf laptop yangu haifunguki kila nikijaribu kuwasha ikifikia kipengere cha WELCOME inaniandikia maneno yafuatatayo.

The application or DLL C/WINDOWS/system32/LSASRV,dll is not applications valud Windows image, please check this against your installation diskette
Msaada tafadhali
 
Jaribu ku boot tena alafu press F8 kabla haija load Windows OS - itajitokeza Windows Advanced Option Menu kuna option karibu kumi na moja wewe chagua inayo sema: Last Know Good Configuration - yaani settin7gs za mwisho zilizo fanya kazi kabla ya tatizo kujitokeza. Ukisha i select press enter uangalie kinacho endelea ukifanikiwa mpaka mwisho utakuwa umesolve problem - lakini ikikwama tena usikimbilie ku install OS upya, we toa harddrive ifunge kama external drive kwenye housing yenye USB, sasa tafuta komputa yenye latest Anti virus ifunge hiyo drive kwenye one of the usb ports, system ikisha detect external HD yako basi fanya complete scan ya harddrive for virus, ukisha maliza ifunge tena kwenye laptop yako - kama tatizo litaendela hapo ndipo itakubidi ku reinstall OS ya Windows upya.

Hapa nimesema kuhusu virus kutokana na mara nyingi ku corrupt some data link libraries - utakuta watu wanakimbilia kuweka upya systems software kabla hawaja scan virus kwanza na kujiridhisha kwamba virus aihusiki, ndiyo wakimbilea ku re install.Huo ndiyo mchango wangu.
 
Back
Top Bottom