Wataalamu wa computer naomba msaada

Afisa Muuguzi

JF-Expert Member
Sep 28, 2018
215
173
Habari wanajukwaa wa technology. Kama kichwa kinavyoelekeza, kuna laptop hapa 32 bit os,2.3Ghz processor, RAM 4GB HD graphics 3000. Hii laptop ilikuwa na window 7 sasa ikawa imeisha muda wake nikawa nataka ku-update basi nikaanza zoezi la ku-update.

Ikawa kila nikifanya activation ikifikia hatua ya pili kama 56% inagoma alafu inazima haiendelei tena. Nikajaribu mara kadhaa bila mafanikio nikaamua kuiacha. Sasa akaja jamaa yangu na flash akapiga ikakubali nikasema fine lakini baada ya hapo ndio tatizo likaanza sasa.

Kwanza mouse ikawa haifanyi kazi kwa hiyo nikawa natumia keyboard ila baadae nikafanikiwa kutatua tatizo. Sasa tatizo lililobaki ni upande wa Network kwa sasa haikubari kuunga mtandao kwa njia yeyote ile iwe Wi-Fi, USB hata modem na pia nimegundua pale kwenye network icon hakuna zile bars |||| kama mwanzoni ila sasa hivi kuna kama kibox halafu kimepigwa X sasa sielewi.

Pia upande wa video inaonyesha chenga chenga na picha zisizoeleweka nimejaribu kufanya setting zote lakini hamna kitu. Pia wakati wa kuwasha pale baada ya brand name zinatokea windows 7 mbili moja chini moja juu sasa nataka kuitoa moja nifanyeje.

Jana nimejaribu kupiga window upya nikihisi labda nitatatua tatizo lakini katika option ya kuboot from USB pale nikichagua tayari ila kila nikibonyeza ENTER haikubali haiendi popote sasa nashindwa kuelewa shida ipo wapi.

Tafadhali kama kuna namna yeyote ya kufanya naombeni msaada wataalamu katika hili. Ahsante

Chief-Mkwawa Mwl.RCT Mtwara Smart
 
mQutubi,

Hapo naona jamaa yako alifanya ku install windows mpya bila ya kufuta mafaili ya OS ya zamani. Na hiyo unayoiona chenga chenga kwenye video ni unatakiwa ku update Graphics Drivers baada ya kufanya installation ya windows mpya.

Touchpard ni same story drivers pia or kama haujawahi kuifungua au imejizima kwenye BIOS. Hiyo network nina uhakika ni drivers.

Naomba unijibu maswali haya tumalize hili tatizo:

1. Wakati jamaa alivyokuwa anafanya installation pale kwenye kufanya setup ya language na Etc touchpard ilikuwa Inafanya kazi?
2. Mshawahi kufungua hiyo PC na kutoa CMOS battery?
3. Naomba system model ya hiyo PC (Sio specification).

Asante
 
Mtwara Smart,

Ndio mwanzoni ilikuwa inafanya kazi baada ya zoezi kuisha ndio ikagoma haikufanya kazi tena hadi nilipoiset kwa fn na f12 ndo ikaja kukubali. Cmos battery hatujawahi kuitoa mkuu.

System model siijui ndo unamaanisha nini ila hii inaitwa Packard bell easynote ts 11HR
 
Ndio mwanzoni ilikua inafanya kazi baada ya zoezi kuisha ndo ikagoma haikufanya kazi tena hadi nilipoiset kwa fn na f12 ndo ikaja kukubari.

Cmos battery hatujawahi kuitoa mkuu.

System model siijui ndo unamaanisha nini ila hii inaitwa Packard bell easynote ts 11HR
Sawa Sasa Usifanye Installation Na Upya Wa Hiyo Windows

Tumalize tatizo la DRIVERS

Then Nitakufundisha Jinsi Ya Kufuta Mafile Ya Hiyo Windows Nyingine Inayoonekana Wakati Wa Ku Boot
 
Sawa Sasa Usifanye Installation Na Upya Wa Hiyo Windows

Tumalize tatizo la DRIVERS

Then Nitakufundisha Jinsi Ya Kufuta Mafile Ya Hiyo Windows Nyingine Inayoonekana Wakati Wa Ku Boot

Hakikisha una MB Za Kutosha Na Internet Ina Speed

Ingia Hapa
1572422595967.png



Nisha Select Tayari Model Ya Laptop yako kwenye link hapo Juu

Nenda Humo Download Drivers Hizi Hapa

1. GRAPHIC 1

1572422744381.png


2. GRAPHIC 2

1572422797377.png


3. WIRELESS

1572422875627.png


UKIMALIZA KU DOWNLOAD RUDI HAPA JUKWAANI TUKUELEKEZE JINSI YA KUFANYA MANUAL INSTALLATION


Kama Unaona Hiyo Ngumu Jaribu Hii

1. Ingia Hapa


1572423016374.png


2. Bonyeza Hapo Install All Required Drivers

3. Ukimaliza Run Hiyo .exe File Ulilodownload linatwa Driverpack-17-Online Utakutana Na Kitu Kama Hiki

1572423213002.png


4. Select Kule Juu Kushoto Pameandikwa "Start In Expert Mode"
Itakuja Hivi Chini

1572423334785.png


5. Kuepuka Kupoteza Muda Select Drivers Unazohitaji Tu Za Muhimu
Ambayo Ni Graphic, Wireless Na Touchpard.

Then Isubiri Imalize, Hakikisha Una MB Za Kutosha.
Ikimaliza Restart PC Then Angalia Umefanikisha???

Kama Kuna Tatizo Rudi Jukwaan Tukusaidie.

Wasalaam

Mtwara Smart
 
Hapo ni ku update drivers tu, ingia official website ya manufacture wako ama tumia windows update, njia rahisi ni kuwa na modem hii huwa na drivers zake utapata network hata kama huna drivers za wifi.
 
Back
Top Bottom