Msaada: Laptop yangu aina ya Toshiba Tecra ina tatizo la kuwaka (blinking) taa ya charge

tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
857
1,000
Habari ya majukumu wadau.

Kama ambavyo title inajieleza, Laptop yangu imegoma kuwaka na taa ya charge ina blink throughout.

Nimejaribu kutoa battery na kuunganisha charge moja kwa moja lakini bado ile taa inablink. Pia nikirudisha battery ile taa inaendelea kublink throughout hadi niiondoe.

Naomba msaada wa mwenye kujua namna ya kutatua hiyo changamoto kabla sijaenda kwa mafundi anisaidie.

Natanguliza shukurani zangu.
 

racka98

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
251
250
Jarb kutoa betri na disconnect charger then shikilia button ya kuwasha kwa sekunde kma 30 hvi then jarb kuiwasha tena ukirudisihia kila kitu.

Ikigoma tafta betri nyingine yenye charge alaf uiweke uone kma itawaka. Na pia jarb kutafta power adapter nyingine

Mara nyingi laptop ikiwa ina blink hyo taa ya charge inamaanisha imeingia kwenye short circuit prevention mode kutokana na betri kuisha kabisa au short kwenye charger. Kuitoa kwenye hyo mode ni kwa kushikilia hyo button ya power au kubadilisha charger kma ndo ilikua inasababisha hlo tatzo
 

tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
857
1,000
Asante sana kwa maelezo mazuri. Nimejaribu kufanya hivyo ila sijafanikiwa. Ngoja nijaribu option ya mwisho ya kutumia adopter nyingine nione kama nitafaulu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom