Msaada: Laptop yangu imegoma kuwaka

Msaada: Laptop yangu imegoma kuwaka

truegooner

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2014
Posts
779
Reaction score
339
Habarini.

Nina tatizo na laptop yangu. Nilikuwa na-install program Fulani katika laptop yangu ya HP G62. Katika kui-restart ikawa inachukua zaidi ya dk 20. Yaani iliganda, hivyo nikajaribu kuizima kwa kui-force. Nili-hold down the power button kwa secunde kama 15 lakini bado ilikataa kuzima, hivyo nikai-unplug kutoka kwenye umeme kasha nikatoa betri ndo ikazima.

Lakini toka hapo haiwaki tena. Nimesoma forum kibao jinsi ya kutatua tatizo lakini imegoma. Je kuna mtu ambaye amewahi pata tatizo kama hili au kulisikia mahali na pia akawa na njia ya kulitatua? Yaani maisha bila laptop yamekuwa magumu kweli.
Msaada tafadharini. Nipo Dar es salaam, ukonga.
 
jaribu kuchomoa betri ya laptop kisha uiwashe laptop bila ya kutumia betri, kama bado angalia hiyo chaja ya laptop (adapter) angalia hizo nyaya zake labda mojawapo imelegea ndio maana labda haipitishi umeme. kama bado sasa hapo uanze kuchanga hela na uipeleke kwa fundi wa uhakika wa computer.
 
Nashukuru sana kwa mchango wako ndugu, nimejaribu kuiwasha bila ya kuwepo na betri imekataa, nimejaribu charger kwenye laptop nyingine, hiyo charger ni nzima. Nimetumia technique ya kutoa betri, kisha una unplug kutoka kwenye umeme, na kubonyeza power button kwa kuishikilia kwa kama 20 second, ila imegoma! Je ni mafundi gani wazuri wa laptop? Nafikiri motherboard ina fault kwa sasa.
 
truegooner ungesema upo wapi ili wadau wakupe recommendation ya fundi huko uliko.
 
Last edited by a moderator:
Software ulo instal itakuwa na matatizo na mi nahisi umeinstal game hapo nakushauri uende kwa mawakala wa HP kama wapo hapo town ila watakupiga cha juu sana kaka na pia fanya mpango ununue smart phone kama huna itakusaidia sana katika michakato yako ya maisha.
 
mafundi wazuri wa laptop wapo kariakoo mtaa wa kongo kwenye maduka wanayouza computer. Hasa kuna duka linaitwa sunrise au uhuru electronics wanamafundi wazur na hata gharama zao sio kubwa. Pia hata humu jamvini kuna mafundi wa computer, so tafuta thread zao ama nenda hapo kariakoo.
 
Nenda Jengo la Machinga complex ilipo bank ya akiba panda hizo ngazi ghorofa ya tatu uliza mafundi computer utawakuta wengi sana na ni wataalam wenye uwezo wa kufumua motherboard nadhani watakusaidia na hawana bei kubwa

Sent from my iPhone 4S using JamiiForums
 
Nashukuru mkuu, nitapita hapo kesho!
 
mafundi wazuri wa laptop wapo kariakoo mtaa wa kongo kwenye maduka wanayouza computer. Hasa kuna duka linaitwa sunrise au uhuru electronics wanamafundi wazur na hata gharama zao sio kubwa. Pia hata humu jamvini kuna mafundi wa computer, so tafuta thread zao ama nenda hapo kariakoo.

Asante ndugu.
 
Software ulo instal itakuwa na matatizo na mi nahisi umeinstal game hapo nakushauri uende kwa mawakala wa HP kama wapo hapo town ila watakupiga cha juu sana kaka na pia fanya mpango ununue smart phone kama huna itakusaidia sana katika michakato yako ya maisha.

Haikuwa game, ni kisoftware package fulani kwa wikipedia 2011. Asante kwa ushauri ndugu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom