Laptop yangu HP baada ya kuizima haiwaki tena na haipeleki chaji

Kiwangwa Son

Senior Member
Nov 29, 2018
178
115
Wataalam wa tech habari ya majukumu.

Nina laptop yangu nipo nayo karibu mwaka na nusu haijawahi kusumbua mahali popote ilikuwa shwari tu. Ila leo naona ndo mara ya kwanza imeanza kunionyesha mauzauza.

Nilikuwa natumia vizuri tuu tangu asubuhi matumizi ya kawaida kama movies na kusikiliza nyimbo audio na video. Kuna muda umeme ulikatika hivyo nikaamua kuizima ili kutunza chaji, nikaitoa chaji ikiwa na asilimia kama 70 hivi nikaiweka geto nikaenda kwenye harakati zangu now nimerudi nawasha haiwaki na chaji haipeleki na wakati nilivyokuwa naizima ilikuwa na chaji.

Nimejaribu kutoa betri kuiwashia kwenye chaji lakini wapi haiwaki na hakuna taa yoyote inayotoa mwanga kuashiria pc itawaka..
Chaji nimejaribu kuitest ni iko powa nzima tuu sasa sijajua changamoto nini hapa wakubwa.

Siku kama 3 nyuma kuna notification ilikuwa inaniletea wakati wa kuwasha kwamba internal battery ipo very low and need to be replaced, primary battery 601 then inawaka au nikibonyeza enter inawaka.

Sasa sielewi kama labda hiyo primary battery ndo sababu au vipi, naombeni msaada wenu wakubwa.

Nianzie wapi kusolv hapa..
 
DingiMbishi

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
346
402
Nangojea mwongozo,siti ya mbele kabisa,na mm kaHp kangu mini kamefanya hivyohivyo,kamekuwa kama kadesktop yaani bila umeme huwezi kukatumia wakatu kalikuwa kanakaa na chaji masaa 3 hadi 6 bila kukichomeka kwenye umeme
 
daraja la kigamboni

JF-Expert Member
Apr 28, 2016
2,006
1,539
Hata mimi limenitokea tatizo hilo
Labda ndo shida ya hizo hp laptop
Nimepeleka kwa mafundi, wa kwanza hakugundua tatizo, wa pili hajapata solution toka December mwaka jana
 
Kiwangwa Son

Senior Member
Nov 29, 2018
178
115
Nangojea mwongozo,siti ya mbele kabisa,na mm kaHp kangu mini kamefanya hivyohivyo,kamekuwa kama kadesktop yaani bila umeme huwezi kukatumia wakatu kalikuwa kanakaa na chaji masaa 3 hadi 6 bila kukichomeka kwenye umeme
Kwahiyo yako inawaka ila imekuwa desktop au nayo haiwaki kabisa mkuu..
 
Kiwangwa Son

Senior Member
Nov 29, 2018
178
115
Ukibadili battery vipi?
bado sijajaribu kubadili ila battery wakati nazima pc ilikuwa na 70 asilimia na niliitumia bila chaji kama 30saa hivi kabla sijaizima ambapo nilivyozima kuja kurudi ndo nakuta hivyo
 
mmwamba

JF-Expert Member
May 18, 2014
236
235
1. Safisha RAM
2. Discharge CIMOS battery, toa RAM na CIMOS baterry ukiwa umetoa connection zote za power ie battery and power cabble ibaki kama ilivo bila kuwa na battery na iko disconnected na power cable hapo sasa hold power button kwa sekunde kama 45 hadi dak 1..baada ya kudischarge rudisha cimos battery na ram na battery
 
Million dollars

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,507
2,008
Shida ipo kwenye Motherboard hapo! Power haifiki sehemu ambayo inatakiwa kufika ili kuiwasha Laptop! Ushauri wangu hapo peleka kwa Fundi unayemuamini apime motherboard mjue imezingua kipande kipi ili parekebishwe au kama kuna kifaa kibadilishwe, tofauti na hapo nunua motherboard mpya bei yake si chini ya Laki
 
Andrew Tate

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
3,326
5,006
Yangu nayo hp ilitokea kama hivyo ikazima kwa miezi kama 2 hivi, nikatafuta solution kote na kujaribu zote mpaka nikaja kuuliza jf lakini sikupata suluhisho.
Isipokuwa tatizo nililitafuta mwenyewe wakati najaribu kusafisha fan na kuchomoa chomoa battery pia kuzima na kuwasha kila dk, alafu ikarest moja kwa moja.

Nikahisi labda motherboard imeungua hivyo nikaanza kupiga hesabu za motherboard mpya, lakini siku moja kama maajabu fulani nilivyochomeka wire wa charge ikaanza kushika moto then paap! imewaka.

ila najua bila shaka tatizo litakuwa lillikuwa kwenye battery na moto kutofika sehemu husika.
Jaribu solutions zote itawaka tu baada ya muda.
 
Mkuu sijui tatizo huwaga ni nini kwenye hizi hp leo imewaka nimeshangaa maana niliona niachane nayo tu nisiikorofishe.
Leo nimejaribu imewaka flesh tuu hadi nimeshangaa..
 
Andrew Tate

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
3,326
5,006
Mkuu sijui tatizo huwaga ni nini kwenye hizi hp leo imewaka nimeshangaa maana niliona niachane nayo tu nisiikorofishe.
Leo nimejaribu imewaka flesh tuu hadi nimeshangaa..
Unaona sasa! yangu ilikaa miezi 2 plus kufungua fungua lakini ikaja kuwaka kimaajabu na mpaka leo inapiga kazi bila shida.
Hp kuna tatizo kwenye hardware zao ambalo bado wameshindwa kulitafutia utatuzi na hawajaligundua.
 
Kiwangwa Son

Senior Member
Nov 29, 2018
178
115
Unaona sasa! yangu ilikaa miezi 2 plus kufungua fungua lakini ikaja kuwaka kimaajabu na mpaka leo inapiga kazi bila shida.
Hp kuna tatizo kwenye hardware zao ambalo bado wameshindwa kulitafutia utatuzi na hawajaligundua.
Nikweli mkuu ningehangaika bure ningepigwa pesa na mafundi wetu
 
brianraymond255

New Member
Mar 21, 2022
4
0
Wataalam wa tech habari ya majukumu.

Nina laptop yangu nipo nayo karibu mwaka na nusu haijawahi kusumbua mahali popote ilikuwa shwari tu. Ila leo naona ndo mara ya kwanza imeanza kunionyesha mauzauza.

Nilikuwa natumia vizuri tuu tangu asubuhi matumizi ya kawaida kama movies na kusikiliza nyimbo audio na video. Kuna muda umeme ulikatika hivyo nikaamua kuizima ili kutunza chaji, nikaitoa chaji ikiwa na asilimia kama 70 hivi nikaiweka geto nikaenda kwenye harakati zangu now nimerudi nawasha haiwaki na chaji haipeleki na wakati nilivyokuwa naizima ilikuwa na chaji.

Nimejaribu kutoa betri kuiwashia kwenye chaji lakini wapi haiwaki na hakuna taa yoyote inayotoa mwanga kuashiria pc itawaka..
Chaji nimejaribu kuitest ni iko powa nzima tuu sasa sijajua changamoto nini hapa wakubwa.

Siku kama 3 nyuma kuna notification ilikuwa inaniletea wakati wa kuwasha kwamba internal battery ipo very low and need to be replaced, primary battery 601 then inawaka au nikibonyeza enter inawaka.

Sasa sielewi kama labda hiyo primary battery ndo sababu au vipi, naombeni msaada wenu wakubwa.

Nianzie wapi kusolv hapa..
karibu E-sky Technology tokuhudumie tunashuhulika kutatua matatzo yote ya computer yako
0625787147.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom