Msaada: Laptop inashika sana moto

Marco Polo

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
11,415
17,853
Heshima kwenu wataalam wa jukwaa....Nina laptop nimenunua Jana ni HP ...ila inashika sana moto kama techno vile NA pia inavuma sana....pia nimeichunguza haina mlango wa CD ...VP wakuu maana jamaa kanipa siku 7 niiangalie nikiona hainifai niirudishe
 
Inawezekana feni ya kupoozea jiko imekufa... Mwambie aifungue abadilishe feni. Am sure itaacha kuvuma...
 
VP NA mlango wa Cd sio kigezo cha ubora wa laptop?
Mlango wa CD sio tena muhimu kwa teknolojia ya sasa nani anatumia CD? CD zimekuwa replaced na USB au flash... Hata wakati hizi za CD zinaingia, tulikuwa tunatumia floppy disk, nazo zikaanza kupotea mpaka leo hakuna computer inatumia floppy disk...
So teknolojia ya CD isikuumize kichwa. Hicho ni moja ya kiashiria kuwa hiyo laptop ni ya kisasa...
 
Mini laptops huwa hazina mlango wa cd. Zinatumia external cd drive... inawezekana ya kwako ni mini. Pia usipende kuweka laptop kitandani inakuwa haipoi vizuri, betri haitakuwa na maisha marefu pia
 
Ahsante Chief.
 
Mini laptops huwa hazina mlango wa cd. Zinatumia external cd drive... inawezekana ya kwako ni mini. Pia usipende kuweka laptop kitandani inakuwa haipoi vizuri, betri haitakuwa na maisha marefu pia
Nimekusikia mkuu
 
Nina hp ina chemka kama ya kwako, niliwaza labda naioverload maana inapiga sana kazi morning to everning kila siku.

But sijatake action yeyote iko vizuri tu
 
Haijalishi unaiweka wapi, chamsingi hakikisha sehemu za kutolea hewa nje, hazizibwi.
Pia inawezekana feni ni zima lkn ndan ya computer yako, kuna vumbi sana, Ukiweza kusafishwa itasaidia.
 
1. pc ikipata joto kubwa sana inajizima au kujishusha clock speed
2. joto sio kubwa kama halijazidi kiwango ambacho manufacture amekisema hata kama wewe unaliona kubwa.

angalia hio pc ina cpu gani? nenda mycomputer halafu right click then properties nisomee jina lake.
 
Manufacturer; Hawlet...... Processor;intel(R) core(T) i5 CPU M 450@2.53Ghz....RAM 6gb....system type 64 bit operating system ...,
 
Manufacturer; Hawlet...... Processor;intel(R) core(T) i5 CPU M 450@2.53Ghz....RAM 6gb....system type 64 bit operating system ...,
hii cpu inavumilia hadi nyuzi 105 C

tafuta software ya kupimia joto uangalie laptop hio, mfano wa hio software ni kama HWMonitor idownload hapa

HWMONITOR | Softwares | CPUID

pia fahamu hio ni generation ya kwanza ya i5 zina joto sana hizo cpu na zinatumia umeme mwingi.
 
Ukiweka kitandani lazima isumbue weka juu ya meza na kama ni mpya huenda itakuwa sawa soon. Iwashe alafu iache masaa 24 uone kwanza kabla siku saba hazijafika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom