huyo hakutaka kuwamegea mwache afe nazo kwani kama alikuwa na uwezo wa kuziweka kwenye E mail ina maana ana mtu ambaye amemueleza Pass word yake in case akifa. We subiri atajatokea mmoja wenu atakua na hiyo password. We una haraka nazo hizo siri zake za nini ndio maana hakukuambia alikua hataki mtu azijue. Na kama yupo atakuwa ana instructions maalum za kutokuelezea hicho alichokiweka. Tafadhali wana jamii naomba msimpe huyo jamaa hiyo mbinu kama yupo anaezijua kwani inaonekana akiweza kufanikisha madhara yake yatakuwa kwa wengi atawafungulia E mail zao na kupata habari ambazo yeye astahili kuzifahamu.
Nina ndugu yangu ambae amefariki, na imekujakugundulika siri zake nyingi alikuwa amezihifazi kwenye Email yake. Hivyo naomba msaada kwa yeyote mwenye kufahamu namna ya kugundua password kesheria ili kuwazafungua hii mail. Na hata kama kisheria ni process ndefu, basi kijinai (hackers) wasalaam!.
Tunajifunza nini? ni bora jamaa angezimwaga kwenye karatasi akawapa mashehe na mapadiri?
Pole sana ndugu yangu-ngoja utapata ushauri,hapa hakishindikani kitu. Ila kuwarahisishia wataalamu,waeleze ni email gani yahoo,hotmail,outlook etc. Na je unalipa au unataka msaada wa bure kabisa?
Hii ni kazi ya administrator wa mirathi hiyo, ambapo atakuwa amechaguliwa na kikao cha familia!..Hii haraka yako Broda inazua maswali mengi!..Watu wanaweza kukusaidia jinsi ya kuhack, lakini ikasababisha havoc kubwa zaidi kuliko thamani ya mali zilizopo kwenye hizo mail...Hivyo jitahidi ufuate taratibu za kisheria zinavyoelekeza!