M.E.M.A
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 1,373
- 472
Wakuu kuna hili jambo lina nitatiza sana.
KIAPO CHA NDOA:
Mimi___________nakutwaa wewe________uwe mke/mume wangu halali wa ndoa. Niwe nawe kwa umaskini na utajiri, kwa afya njema na ugonjwa, nikupende, nikutunze niwe nawe siku zote hadi mauti itakapotutenga sawa sawa na amri tatatifu ya Bwana.!
Sasa swali!; Kama katika uchumba na urafiki hujawahi hata kumjali mwenzio akiwa mgonjwa na mhitaji, utayaweza hayo kwenye ndoa? Na kuna wengine hawawasaidii wapenzi wao kwa kigezo cha "asiponioa/nisipomuoa je?.
Kuliweka swali vizuri ni kwamba ipo haja ya kushirikiana na mpenzi au mchumba wako hasa katika shughuli nzima ya kuchuma mali? Nimsaidie au nimchunie hadi awe mke/mume? Kwanini ni vizuri na kwa nini sio vizuri? Upande upi ni salama ?