Msaada kwenye Tuta: Qatar Airways

Inategemea wapi unaelekea lakini nitachangia kidogo kwa uzoefu niliopata kwa kusafiri na hao Qatar pamoja na baadhi ya mashirika hayo yalioyatajwa between London na Dar.

Egyptair kweli ni rahisi ila wanasumbua transit masaa ni mengi na wanaweza kukusumbua hapo Cairo kutegemea na karatasi gani unasafiria na mizigo inaweza kupotea transit.

SwissAir ni rahisi vilevile transit fupi, service zao average, good connection Zurich ila nisichopenda mimi ni usumbufu ambapo unafika na kuondoka Dar usiku na kutokea London unaruka mapema mno reporting time saa 11 alfajiri.

KLM na Kenya Airways wana ubia kwa hio connection ni nzuri na una choice zaidi ya kupanga flying time. Service Kenya airways ni nzuri kupita mashirika yote na kama mtu wa ulabu humo ni tusker ushindwe wewe.

Ethiopian bei nafuu service nzuri ila transit nao ni ndefu.

Mimi mara nyingi ninasafiri na hawa Qatar kwa sababu ni nafuu na wakati mwengine ninapata tiketi ya bure kutokana na Q-miles zangu (air millege) Qatar Airways advantage zake, from London - Doha ndege airbus A340 ambayo ina nafasi zaidi ya kunyoosha miguu, cabin storage kubwa, connection time Doha less than hour na service nzuri lakini kutoka Doha- Dar ndege ndogo A320 huna nafasi ya kunyoosha miguu na wafanyabiashara wengi kiasi cha kwamba inakuwa taabu kupata cabin ya ku-store hand luggage, service average ila wanakuheshimu ukiwa privilege club member, na from Dar-London transit ni ndefu mno 7 hours pale Doha tena usiku.

Kwa tiketi rahisi online tembelea ticket comparison sites utapata unafuu kama unanunua e-ticket na jaribu kusafiri kati ya wiki (tue-thurs).

opodo.co.uk (opodo.com)

skyscanner.net

kayak.co.uk
 
Kenya airways per se nilipanda ndege yao kwa mgongo wa KLM kutoka amsterdam -nairobi..nilijuuuta kuwafahamu maana huduma kwa wateja ilikuwa ziro hata wakenya waliokuwepo waliona aibu. mfano tv screens kwenye byingi zilikuwa mbovu na bado wali issue matangazo kuwa kuna entertainment programs kibao, na hakuna apology, wahudumu walikuwa wanakimbia kimbia tu kwen kutoa huduma hasa wakituona siye wenzao baso ni dharau mtindo mmoja....
 
mpanda klm siku hizi bei yao nafuu sana na allowance ya mzingi ni kilo nyingi about 40kg
 
Kwa kweli sikushauri utumie Egypt air. Niliitumia back in July from London to Dar kupitia Cairo. Kwanza jamaa hawazingatii muda hata kidogo. Tulianza kupoteza muda London kwani ndege ilichelewa kwa masaa mawili. Kwa kuwa tulikuwa tunaunganisha ndege pale Cairo niliwauliza kama tutawahi na walinihakikishia kuwa tutawahi na walinicheck-in mpaka sector ya Cairo-Dar. Cha ajabu tulipofika Cairo saa sita usiku (Cairo time) tulikuta ndege imeshaondoka kuelekea Dar. Tuliambia kuwa tutawekwa kwenye ndege inayofuata ambayo itaondoka masa 24 baadae. Haya maneno tulikuwa tunaambiwa kwa dharau kubwa tu na wawakilishi wa Egypt air pale Cairo. Mpaka tunapelekwa hotelini ilikuwa saa 12 asubuhi. Kwa kuwa nilikuwa na mtot mdogo wa miaka 2, nilipata taabu sana. Toka siku hiyo nimeapa kuwa sitatumia huduma za Egypt air tena.

Mkuu Shakazulu,

Airline yoyote inaweza kuchelewa kutokana na matatizo mbali mbali hata KLM, Swissair, BA, Kenya Airways na hata hao Quatar wanaweza kuchelewa tu. Na kuchelewa kwa ndege not neccessarily uwe ni uzembe wa airline, kuna hali mbaya ya hewa, kuna uwanja kufungwa kwa sababu ya accident n.k. Nimesafiri na Egypt Air karibu mara nne lakini sijawahi kukutwa na hayo uliyoyaeleza.

Tiba.
 
Kuchelewa sio tatizo ila treatment unayopata toka kwa hao mabwana ndio tatizo. Customer care yao ni zero.
 
Wazee Heshima Mbele!

Ile safari ndio imekamilika kwa kweli na ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu kila kitu kimeenda shwari na sasa nimerejea kwenye kiota changu hapa bongo, salama bin salimini. Nimetumia hudma za Qatar na ukweli lazma usemwe kuwa sikupatwa na masaibu makubwa.

Nashukuru kuwa ushauri wenu ulizingatiwa na hapan' shaka tutaendelea kupeana mikakati ya kimaisha kwa kuwa naamini JF kuna vichwa lukuki na watu wenye xperiens ndefu yenye kuhitajika, ukiondoa wakorofi wachache.

In'challah Mwenyezi Mungu atawajaalia nyote.

Masalama.
 
Karibu tena Bongo.
Asante maana Mungu wangu kupitia jina la Yesu kakupigania safari nzima.
Jina lake liimidiwe.
 
Qatary air ways so far is the best I can say, so take your ticket you will tell us.Goodluck.
 
Wazee Heshima Mbele!

Ile safari ndio imekamilika kwa kweli na ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu kila kitu kimeenda shwari na sasa nimerejea kwenye kiota changu hapa bongo, salama bin salimini. Nimetumia hudma za Qatar na ukweli lazma usemwe kuwa sikupatwa na masaibu makubwa.

Nashukuru kuwa ushauri wenu ulizingatiwa na hapan' shaka tutaendelea kupeana mikakati ya kimaisha kwa kuwa naamini JF kuna vichwa lukuki na watu wenye xperiens ndefu yenye kuhitajika, ukiondoa wakorofi wachache.

In'challah Mwenyezi Mungu atawajaalia nyote.

Masalama.

Uwe unanipa thanks kila bandiko langu maana nilikushauri bure.....teh teh teh
 
Back
Top Bottom