Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,058
- 16,927
Wasalaam.
Hii ni Kwa wanaume wenzangu japo hata akina dada,mama mnaweza toa ushauri.
Iko hivi,
Juzi, yaani jumamosi,
Nilijichanganya kwa kuhisi nimepotelewa na kifaa changu ndani cha muhimu mno,yaani mno.
Sasa kumbe kuna mtu aliniazima na Mimi nikasahau kabisa kuwa nimeazimisha Mtu.
Basi katika kutafutatafuta na kukosa ,tuhuma zote nikazielekeza Kwa kijana wangu,ambaye muda mwingi sikai naye kwani huwa anaishimkoani anakosoma.
Basi nilitoa maneno yoooote mabaya,huku mwanangu akikataa hajahusika ,nikamsogelea nikamtikisa kama kutaka kumpiga, lakini kijana akapiga magoti huku akidai hajachukua kifaa kile.kwani Hana kazi nacho.
Kwahiyo tangu juzi tumekaa Kwa kukwepana huku nikiamini kijana kapoteza kifaa changu,
Chaajabu jioni hii saa 11 nimeletewa kifaa na mtu niliyekuwa nimemuazima huku akishukuru kwakuwa kimemsaidia mno ,ni takribani wiki tatu zimepita tangu aazime.
Sasa ,najikuta mwenye hatia,mwanangu nimemuonea,natamani hata nimuombe msamaha,je, inawezekana kumuomba msamaha mwanao wa kumzaa?
Majibu yenu tafadhali.