Msaada: kwa wanaofahamu batery bora za gari N50

De Finger

Member
Jan 20, 2017
6
11
Nahitaji kununua batery mpya ya gari N50 naomba ushauri ipi ni batery bora. Matumizi yangu ya gari ni mara chache huwa naiacha bila kuiwasha hata siku 3
 
IMG_20180421_161527.jpg
 
De Finger, kwa ujumla kuna aina mbili za battery .. Kuna maintenance free ambazo hazitumii maji na zinazo tumia maji ( battery acid ).
Maintenance free ni kwa watu wasiopenda usumbufu wa kila mara kucheki na kuongeza hayo maji ( acid/ distilled water ) ila disadvantage yake ikifa inakufa ghafla kama mtu aliyekufa kwa heart attack .. Za kutumia maji inatakiwa uwe makini kuchunga level ya acid, na muda wake ukiisha inakupa warning inaanza kufa taratibu.
Cha msingi zingatia tareh iliyotengenezwa mara nyingi inagongwa mhuri wa moto kwenye betri ( manufactured date ) usichukuwe zaidi ya miezi 12 toka itengenezwe, kisha wauzaji wakupe guarantee au warranty ya angalau miezi 12 kama watakubali.
 
jaribu INDEX ya India...ambayo ni maintenance free....yaani haiongezwi maji....niliweka N40 kwenye gari Machi 2015 nikaitoa November 2017...
hizi battery zipo vizuri sana...
Pia ATLAS ya Korea ni nzuri sana nyo pia naitumia....jaribu hizo mbili nina ushahidi nazo
 
Betri za kuongeza maji kwa ulimwengu wa leo hasa kwa magari madogo sikushauri...achana nazo kabisa ni usumbufu tu
 
Chukua Atlas, nimeweka kwenye gari tokea mwaka 2014 mpaka sasa bado iko vizuri
Atlas za mwanzoni zilikuwa nzuri sana. Siku hizi si nzuri sijui ni kwa nini. Nimenunua ATLAS nikijua bado ni imara, baada ya miezi si hivi ikawashida. Inaonyesha iko fully charging lakini hata kuwasha gari haiwashi.

Ikanilazimu ninunue ALPHALINE wauzaji wanadai bado ni bidhaa mpya hivyo haijachakachuliwa. Iko imara sana. Japo najua nayo pia baadaye itachakachuliwa.

Lakini ukipata ATLAS isiyo feki. Ni battery nzuri sana.
 
Nitakapokuja kununua betri nyingine ya gari, sitonunua tena Atlas.
 
Back
Top Bottom