Sasa mkuu kwa kua unataka kwenda njia hiyo, nitakushauri uanze na kitabu, kuna kitabu tafuta kinaitwa Contemporary Logic Design. Download na software inaitwa Xilinx unaweza pata trial version yake bure, ni software kubwa sana download file yake kama 7GB, ukiinstall inahitaji kama 20GB ya harddisk space, hii ndiyo itakua inakusaidia ku~simulate circuits zako, unaweza ukachora circuit na ukasimulate ukaona outputs zote, au unaweza ukaandika code kwa kutumia Verilog yenyewe ikakutengenezea circuit automatically.
Anza na kitabu, soma page to page, ndani yake utajifunza kutengeneza electronic circuits kwa njia mbalimbali, utaanzia kwenye transistors, utasoma CMOS, then utakuja basic za logic gates, piga combination logic vizuri maana ndio kama building block ya kila kitu huko mbele, the piga sequential logic, wakati unasoma utakua unaona simple projects, mfano utaona Binary counter, isome uielewe, then kaa chini chora kwenye karatasi prototype yako, fungua xilinx, chora diagram yake then simulate uone kama inaleta correct output. Hakikisha kabla hujamaliza kitabu uwe unaweza kukaa chini, ukaandika logic ya kuweza kufanya vitu vichange angalau kwa simulation, mfano:
- Vending machine system
- Traffic alert system
- Elevator control
- Door lock system inayotumia namba au card ku-unlock
- Object counter e.t.c
Na kama project ambayo ni challenging ya kujipima nitakushauri utengeneze a micro-processor ya 8-bit from scratch, ukimaliza hiki kitabu utaweza kuitengeneza though it will take you time.
Sasa utamu wa logic design unakuja pale ambapo utakaa na kutengeneza real devices maana hapo juu utakachokua unafanya ni kukaa na kusimulate tu kwenye computer, real devices itakulazimu kutoa mshiko, itabidi ununue FPGA, Arduino, na sensors kibao uanze kufanya your own projects, na hapa pia kama hujui programming utapata tabu kidogo kwa hiyo ni muhimu kujifunza C.