Msaada kwa walokole juu ya mahusiano kwa huyu msichana nimpendae

Bwana Yesu apewe sifa habari za usiku,

Tukianza na mada kilichonileta hapa kuna dada nimetokea kumpenda sana kwa kipindi cha miaka mitatu sasa3 sasa mimi ni kijana niliyelelewa kwenye misingi ya dini hivyo sijawahi kumeleza wazi hisia zangu kwa sababu zifuatazo;

Kwanza, nimejaribu kumjenga katika mazoea ya urafiki kwanza ili niweze kumtambua zaidi na kuaanda mazingira ya kumueleza ukweli pasipo poteza muujiza huu.

Pili, nimeendelea kutulia zaidi kwa Mungu kwa kuendelea kumuombea kwa Mungu mpaka pale nitakapoona wakati sahihi Mungu.

Kwanini nakuja JF?

-Je ninachokifanya sahihi kuendelea kumsubiri?

-Kuna athari nitapata nikiendelea kutunza huu muujiza wa huyu dada?

-Kitu gani ninaweza kufanya zaidi huyu mdada anipende mimi pasipo kipingamizi?

My note;
-Unaruhusiwa mtu yoyote kuchangia.

-Ushauri wenu utanijenga zaidi.
Hayo maswali yoote yatajibiwa na Mungu uliemtumaini hapo awali,kuja humu unakosea sana,utakua polluted tu.
Dah nakumbuka nilianza uhuni chuo mwaka wa pili dah nilikuaga sijawah kuonja issue mmmh hatari jamani,hapo ndo uhusiano na Mungu wangu ukainhia doa,lakin sasa nimemrudia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujafikia umri wa kitafuta mchumba kwa sasa kazana na biashara au shule jijenge kiuchumi ukifika 30 uwe walau na uwezo wa kupata 25000 kwa siku utafurah .we na ndoa bado Huyo ni Mke was kaka zako wenye maisha yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetisha kaka Mungu na akubariki
Mkuu;
Wewe ndo uliyebebwa au ndiye uliye beba hilo rumbesa? Ulikuwa mlokole kwa muda gani?? Kwanza kama hujui, walokole ndio wanaopeana unyumba kwa staha na starehe kuliko mkristo mwingine yeyote. Walokole wameelekezwa na biblia kuwa wasinyimane. Mke hana amri juu ya mwili wake na vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake. Upo hapo??
Nadhani ulikutana na viruka njia au wale waliobatizwa kwa maji ya baraka.
 
Back
Top Bottom