Msaada kwa walokole juu ya mahusiano kwa huyu msichana nimpendae

Duh....kweli huu Ni muujiza!!!
..
Miaka mi3 unalea muujiza..
Nakutengeneza mazingira.

Kwahiyo unasubiri Dada afunuliwe kwa njia ya roho mtakatifu ama ndoto!?

Unaonekana unampenda Na nia yako Ni njema,lakini:

Kinachokutesa siyo uoga wa kutenda dhambi,bali Ni uoga Na hofu ya kumwambia ukweli!

Na bahati mbaya sana ushamfanya Dada yako.

Lakini usijali!!!....

Jikaze mwambie baada ya maombi ya mda mrefu takribani miaka mi3 umeona maono...yeye ndo mwanamke ulopewa Na Bwana..

Na umeoneshwa mumefunga ndoa.Na yakwamba baada ya maono Yale umejiskia amani kumwambia ili nae ajue muujiza wa Bwana juu yenu!

Then muulize maoni yake kuhusu hilo...

Yeye anaonaje muendelee kuombaa au mmushirikishe baba mchungaji harakati za uchumba hadi ndoa zianze...

Vinginevyo mwambie ukweli kwa kutumia lugha ya kawaida "achana Na stori za miujiza Na maono"

1.Mwambie unampenda sana
2.Tangu mfahamiane umejiridhisha anafaa kuwa mkeo.
3.Ungependa atafakari ombi lako ktk Bwana Kama itampendeza muoane.

Atakachokujibu ndo kitakupa jibu Ni muujiza ama la!

Mwisho:Ukianza kupenda ujue umekua,acha kuazima simu ya mamaaa!




Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
Asante mkuu

jf ya sasa sio ya zamani
 
Endelea kumuomba MUNGU ni muhimu sana kama umechagua njia hiyo ila jitahidi usimlazimishe MUNGU kuwa akupe huyo huyo uliyeona anakufaa maana huna uwezo wa kujua nani atakufaa.
Muombe MUNGU mke mwema na yeye atakuonyesha kama ni huyo au siye.
 
Bwana Yesu apewe sifa habari za usiku,

Tukianza na mada kilichonileta hapa kuna dada nimetokea kumpenda sana kwa kipindi cha miaka mitatu sasa3 sasa mimi ni kijana niliyelelewa kwenye misingi ya dini hivyo sijawahi kumeleza wazi hisia zangu kwa sababu zifuatazo;

Kwanza, nimejaribu kumjenga katika mazoea ya urafiki kwanza ili niweze kumtambua zaidi na kuaanda mazingira ya kumueleza ukweli pasipo poteza muujiza huu.

Pili, nimeendelea kutulia zaidi kwa Mungu kwa kuendelea kumuombea kwa Mungu mpaka pale nitakapoona wakati sahihi Mungu.

Kwanini nakuja JF?

-Je ninachokifanya sahihi kuendelea kumsubiri?

-Kuna athari nitapata nikiendelea kutunza huu muujiza wa huyu dada?

-Kitu gani ninaweza kufanya zaidi huyu mdada anipende mimi pasipo kipingamizi?

My note;
-Unaruhusiwa mtu yoyote kuchangia.

-Ushauri wenu utanijenga zaidi.
I doubt uelewa wako kuhusu maombi unayosali na ulokole wako kama ulivyosema
Haya maswali uliouliza hapa ni Mungu tu ndio anakujibu sasa ajabu unatuuliza sisi binadamu wenzio
yani maombi upeleke kwa Mungu maswali utuulize sisi, we kaka upo serious kweli?
 
Ushauri;
Kijana, kama umeokoka, nenda kwanza mshirikishe mchungaji wako hisia zako kwa hako kabinti ka waridi wa moyo wako. Usimtongoze kwani ukristo hauruhusu mtongozano.
Mshirikishe mchungaji kwanza ndipo akuelekeze la kufanya. Kufanya hivyo sio kwamba ati hujui kutongoza.
Asante mkuu kwa ushauri mzuri
 
Sitaki kujua umri wako wala mambo ya shule afu hiyo simu ya mama yako mwambie leo unalala nayo,,, Sawa?

Kwanza huyo binti naye kaokoka au ndo wale wa kitaani kwetu majohe?

Pili,,,, umesema urafiki wenu umedumu miaka mitatu sio? Na bado unahitaji Muda ili umjue zaidi,,,,, huo ni uzoba na utimbulo

Mwanaume Hua akipenda anapigania fasta ili aushinde moyo wa ampendae,,,, je wewe umemfanyia nini huyo binti ktk miaka yote mitatu? Kama unaleta upole na ukimya au umakini sijui kwasababu ya dini hapo utakuja kuarikwa kwenye harusi yake na mjanja mwingine

Tabia zako na zake zinaendana? Maana ktk miaka mitatu ni lazima mlishawahi toka out pamoja Tena sio Mara moja au mbili,,,, je ulifanya nini ambacho kiliweka kumbukumbu,,,, kama hufanyi vitu vinavyojenga kumbukumbu iliyomvutia basi ukianza kumtongoza ni_pm ili nikupe ujuzi zaidi

Je huyo binti kakuzidi umri au ndo rika moja,,, bado hujui mapenzi kwahyo hakikisha ukimpata Mwanamke umridhishe sio unamchezea chezea tu hata hufanyi mambo akafika kileleni kwahyo unaweza ukampata kwa bahati nasibu na ukamkosa kwa bahati mbaya kwa tafsiri yako lkn kumbe binti alishayajua na anaelewa nini mapenzi so make sure you're satisfying her quench her desire

Yapo mengi tu kufanya ili kuushinda moyo wake

Sio lazima umtongoze kwa maneno et "nikwambie kitu, nakupenda" hii ni style ya zamani itasababisha upigwe karenda Bure mpe vitu mtoto akutongoze yeye kama ninavyofanya,,, mengine ntamalizia baadae

Sent from my TECNO-Y3 using JamiiForums mobile app
Mkuu kama upo naomba uje hapa nina shida fulani....
 
Endelea kumuomba MUNGU ni muhimu sana kama umechagua njia hiyo ila jitahidi usimlazimishe MUNGU kuwa akupe huyo huyo uliyeona anakufaa maana huna uwezo wa kujua nani atakufaa.
Muombe MUNGU mke mwema na yeye atakuonyesha kama ni huyo au siye.
Mkuu jambo nzuri na sahihi litakalonionyesha huyu binti umeniambia MAOMBI hapa nimekuelewa vizuri......ila kuna jambo lingine watu wa MUNGU wanapenda kuongelea juu ya amani ya moyo....
 
I doubt uelewa wako kuhusu maombi unayosali na ulokole wako kama ulivyosema
Haya maswali uliouliza hapa ni Mungu tu ndio anakujibu sasa ajabu unatuuliza sisi binadamu wenzio
yani maombi upeleke kwa Mungu maswali utuulize sisi, we kaka upo serious kweli?
Maombi yangu yapo sahihi na hicho ninachokiamini sana kwa amani ya moyo niliyonayo.....kuhusu kuwauliza nyie unaweza ukawa na muujiza ukaupoteza kama unasoma biblia utaelewa hapa nyie mnaweza kunisaidia kwa kiasi fulani
 
Back
Top Bottom