Msaada kwa mwanangu

Msaada kwa mwanangu

Habari za jioni wana jukwa.

Kwa muda sasa kuna hali inamtokea mwanangu ila sijui ni ugonjwa au ni kitu gani. Akiwa na mwaka moja kama mnavojua watoto alikuwa anacheza katika sehemu ya hatari, nilishikwa na hofu maana ni kwenye ngazi.

Basi nikamfokea, ila baada ya hapo ndiyo tatizo likaanza. Alikuwa analia kama anakakamaa hivi, pumzi hazitoki yaani anabaki kimya tu. Nilimchukua kwa uwoga na kumuweka kifuani na kumbembeleza.

Leo akiwa na umri wa miaka 2 na miezi 3 imetokea tena, safari hii akiwa na mama yake wametoka dukani karibu na nyumbani akataka abebwe mama yake akampiga kibao kidogo akaanza kulia na kujitupa chini na kuanza hali kama ya mwanzo kama anakaukia hivi. Mama yake alilia sana na badaye alikaa sawa.

Naomba ushauri kwa madakatari na hata ambao watoto wao wanahali kama hiyo. Shida ni nini au nifanyeje mwanangu asiwe na hali hiyo? Nahofia akifika umri wa kusoma itakuwaje huko shuleni au kwa ambaye hamjui ikimtokea itakuwaje?

Naombeni msaada wenu wanajukwaa.
Pole, anahitajika kuangaliwa kwenye mazingira haya hospitalini:
1: Phobic anxiety
2: Heart disorders
3: Stress induced seizer
 
Back
Top Bottom