Msaada kwa mkewe umesababisha kero kubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kwa mkewe umesababisha kero kubwa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtu B, Jun 1, 2010.

 1. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni jamaa yangu tuko naye hapa kazini na namheshimu sana kama kaka yangu, umri wake kwenye 40's hivi. Hata wafanyakazi wenzangu wanaamini mimi ni mdogo wake kwa jinsi tulivyo karibu. Mkewe ni shemeji yangu kwa maana hiyo. Mwaka huu mwanzoni kaka akanisimulia shida yake ambayo alisema ni mimi tu ananiambia, si kwamba anadhani nitaweza kumsaidia, bali anaisema tu kupunguza tension kichwani. Akasema mkewe amepoteza kabisa hamu ya ngono, yaani hataki kabisa, na si kwamba ana-cheat popote ni kwamba hajisikii hata kidogo na hataki hata kugusiwa jambo hilo. Huyu kaka ana ule upole wa kilokole fulani, hana mambo ya mademu wala nini. Kwa hiyo kitendo cha mkewe kukosa hamu kimemuumiza sana maana yeye mwenyewe kaka anajisikia anahitaji hiyo kitu sana na hataki kuipata popote zaidi ya kwa mkewe.

  Siku moja kampuni moja ya madawa wakawa wanafanya kama workshop fulani ya kujitangaza kwa madaktari, nikapata tenda ya kuwamo mle ndani niwarekebishie vifaa vyao vya presentation. Katika presentation yao wakaonesha dawa fulani inaitwa Dr Scotts Evening Prime Rose, wakaisifu sana kuwa huwa inawaongezea wanawake ashki, basi nikamkumbuka jamaa yangu. Niliporudi ofisini nikampa habari hiyo akaahidi kuifanyia kazi. Na kweli akainunua, na alisema mkewe alionesha ushirikiano mkubwa sana wa kuimeza kama alivyoshauriwa. Baada ya mwezi tu akaanza kuona mabadiliko, mkewe akaanza kupenda sana tendo, tena akawa yeye ndiye anayedai haki yake, na maisha yakaanza kuwa matamu tena.

  Tatizo: Anasema hamu ya shemeji imepitiliza hadi sasa kaka hamuwezi tena, yaani anataka tendo mara nyingi na anataka kwa muda mrefu sana ambao kaka hawezi. Imefikia kaka anamuomba shemeji aache ile dawa kwa muda au apunguze dozi lakini shemeji inaonekana amekuwa addicted, hataki kuiacha. Sithubutu kumshauri chochote huyo shemeji maana sitaki ajue kuwa mumewe alinihusisha kwenye tatizo lake. Wakubwa, jamaa yangu afanyeje hapo?
   
 2. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yesu na Maria yamekua hayo tena!!! sasa kwani jamaa si alitaka mke awe na hamu na hamu kaipata kwann anashindwa tena?
  Lakini aongee na mkewe kistaarabu amshauri aache hiyo dawa hv vitu artificial sio vizuri inawezekana mama alikua na psychological problems zilizomfanya asiwe na hamu, au alikua ananyonyesha au ana stress. ingekua mm nisingemshauri kutumia dawa bali azidishe mapenzi kwa mkewe na kujaribu kuchunguza nn kilisabbisha asitamani tendo.
   
 3. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuhusu psychological problems sina uhakika, lakini mtoto wao wa mwisho yuko darasa la tatu. Hiyo ya ushauri wa dawa nilimpa jamaa yangu baada ya kuiona inazungumziwa tena mbele ya madaktari wasomi nikaamini ni salama, na hata alikoipata huyo jamaa walimpa ushauri vizuri tu jinsi ya kuitumia, naye akafikisha ushauri kwa mkewe ambaye aliupokea kwa mikono miwili, inaelekea hata yeye suala la kukosa hamu lilikuwa linamtesa ndio maana akakubali kumeza dawa. Sasa dawa imekolea kupita kiasi hadi mume anashindwa kukidhi, na shemeji kashakuwa addicted!
   
 4. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuhusu psychological problems sina uhakika, lakini mtoto wao wa mwisho yuko darasa la tatu. Hiyo ya ushauri wa dawa nilimpa jamaa yangu baada ya kuiona inazungumziwa tena mbele ya madaktari wasomi nikaamini ni salama, na hata alikoipata huyo jamaa walimpa ushauri vizuri tu jinsi ya kuitumia, naye akafikisha ushauri kwa mkewe ambaye aliupokea kwa mikono miwili, inaelekea hata yeye suala la kukosa hamu lilikuwa linamtesa ndio maana akakubali kumeza dawa. Sasa dawa imekolea kupita kiasi hadi mume anashindwa kukidhi, na shemeji kashakuwa addicted!
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mmmh ...kwani hizo dawa hazina dozi? hazina mwisho wake wa matumizi?

  akaonane na daktari aliyempa kwa ushauri zaidi
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha labda huyo dada mlimzidishia dose hii si kawaida ..nendeni kwa waliowauzia madawa wawape namna ya kumsaidia
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Duniani kuna mambo........
  Hiyo dawa akinywa mwanamke asiye na mume je??????
   
 8. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ndo itakua kama ile kesi ya kubaka mtoto wa kiume kule moshi!
   
 9. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  basi rudi kwa wale waliowauzia dawa huenda mlipewa dose kubwa wanaweza kupunguza. wasiwasi wangu ni je akiajaacha hizo dawa si ndio kabisa hata wazo la sex litapotea? maana kwa maelezo yako anatumia bado!
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hahahahahaaa.Arudi kwa hao waliomuuzia hiyo dawa wanaweza kuwa na dawa ya kupunguza makali.
   
 11. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hayo ndio matatizo ya madawa ukiyazidisha tiba lazima iwe mgogoro, kwa vile wewe ni mtaalamu wa IT jaribu kuwasiliana na hiyo kampuni iliyotengeneza au cheki kwenye mtandao unaweza kupata solution!!
   
 12. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Anazidisha dozi ili iweje?? Akaonane na Dr.
   
 13. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  na yeye akanunue VIAGRA anywe, itakuwa ngoma droo
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  MtuB Wapi inapatikana dawa hiyo aisee? naihitaji na mie! Ama ni ya wanawake peke yao?
   
 15. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hiyo dawa ni kwa wanawake pekee. Mbona inapatikana tu kwenye pharmacies.
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Itakuwa mauaji!
   
 17. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi alivyoeleza hali ya mkewe, nafikiri hata hiyo viagra hatamuweza nayo. Kwanza jamaa shida yake siyo erection, ni kwamba anachoka physically kutokana na uhitaji wa mkewe kupitiliza. Sidhani kama viagra ni suluhisho.

  Kinachomuumiza pia ni kwamba hapo kabla alikuwa anamlaumu sana mkewe kwa kukatalia unyumba, sasa kibao kimegeuka. Yani anafikiri mkewe anakomolea ili naye ajisikie vibaya kwa jinsi alivyokuwa anamlaumu hapo kabla. Ati inawezekana ndiyo maana amekatalia kuacha hiyo dawa.
   
 18. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa maelezo yake ni kwamba aliambiwa ameze vidonge viwili asubuhi na jioni, halafu hamu ikisharudi awe anameza kimoja kimoja asubuhi na jioni. Lakini shemeji kashupalia kumeza viwili viwili, mwenzie alipomwambia sasa punguza basi kama ulivyoambiwa umeze kimoja, anadai bado hamu haijarudi kama anavyotaka. Lakini mumewe anaona hamu ya mwenzie tayari ilishapitiliza, akimwambia anaulizwa 'kwani anayesikia hamu yangu wewe au mimi? Mie nakwambia bado sijajisikia kama ninavyohitaji'. Hadi mwenzie anaona sasa anachotafuta huyo mkewe ni balaa, maana hapo alipofika tu jamaa hamuwezi tena. Sijui kaka anajisikia insecure au ni nini (mawazo yangu tu).
   
 19. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa maelezo yake ni kwamba aliambiwa ameze vidonge viwili asubuhi na jioni, halafu hamu ikisharudi awe anameza kimoja kimoja asubuhi na jioni. Lakini shemeji kashupalia kumeza viwili viwili, mwenzie alipomwambia sasa punguza basi kama ulivyoambiwa umeze kimoja, anadai bado hamu haijarudi kama anavyotaka. Lakini mumewe anaona hamu ya mwenzie tayari ilishapitiliza, akimwambia anaulizwa 'kwani anayesikia hamu yangu wewe au mimi? Mie nakwambia bado sijajisikia kama ninavyohitaji'. Hadi mwenzie anaona sasa anachotafuta huyo mkewe ni balaa, maana hapo alipofika tu jamaa hamuwezi tena. Sijui kaka anajisikia insecure au ni nini (mawazo yangu tu).
   
 20. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Mtu B,

  Ulijaribu kumdadisi huyo "Kaka" yako kama naye ni "mwanaume wa shoka"? Maana mwanamke kuishiwa hamu inategemea kwa kiasi KIKUBWA na mwanamume. Mwanamke yeye anahitaji kuwa "switched-on" kwa vyovyote vile kama mwanaume anasubiri mwanamke ndiye aanze huwa ni vigumu sana.

  Kama ulivyosema ni mlokole fulani and so I doubt kama huyo "kaka" haya mambo yanamjia vizuri akili
   
Loading...