Msaada: kwa jirani kuna ng'ombe waleta inzi kwangu

Entim

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,020
2,257
Wanabodi, kwangu kuna inzi wengi nimejaribu kupulizia dawa lakini wapi, nimekuja kugundua wanazalishwa kwa jirani yangu mchafu na anamiliki ng'ombe, mbwa na paka wa kienyeji. Sasa inzi wanahamia jikoni na sebuleni kwangu kama utitiri. Nisaidieni mbinu za kuwathibiti maana siwezi kumshauri jirani auze mifugo wala siwezi kumsisitiza juu ya usafi.
Naomba kuwakilisha.
 
Chimba choo cha nje kifupi weka madini ya kutosha baada ya muda Inzi wote watadili na choo. Hakikisha hakiwi mbali na huyo jamaa harufu imtie akili na yeye.
 
Mtafute kibatala akusaidie kufungua mashtaka kama huyo jirani yako kafuga ng'ombe sehemu ya makazi pasiporuhusiwa. Hata hiyo harufu ya kinyesi cha ng'ombe inayojaa sebuleni kwako ni karaha.
 
Nenda kule dar mtafute mganga mmoja anaitwa magenge mwelezee kisha rudi nyumbani chukua smartphone yako alafu anza kuchati mida ya saa 6.30 hivi mchana itakapofika 7.00 utaona kama kuna wingu ivi la mvua, ilo sio wingu hao ni Nyuki.
 
Chimba choo cha nje kifupi weka madini ya kutosha baada ya muda Inzi wote watadili na choo. Hakikisha hakiwi mbali na huyo jamaa harufu imtie akili na yeye.

Sijakuelewa mkuu, mimi ni mtumishi wa umma natakiwa kioo cha jamii inaniangalia kwa macho mawili.
 
Nenda kule dar mtafute mganga mmoja anaitwa magenge mwelezee kisha rudi nyumbani chukua smartphone yako alafu anza kuchati mida ya saa 6.30 hivi mchana itakapofika 7.00 utaona kama kuna wingu ivi la mvua, ilo sio wingu hao ni Nyuki.

Ushirikina siwezi, bora kukaa kimya kama huna ushauri.
 
Oke kumbe ishu yako iko serious, hapo bora uhame tu! huyo mfugaji inaonyesha ndie founder wa hilo eneo. Mnapo nunua maeneo muwe mnaangalia tabia za kijografia.
 
Jaribu kuweka Wavu kwenye Madirisha yako na Milango hapo itakuwa sio rahisi kwa Nzi kuingia ndani, pia mshauri tu huyo jirani yako aache kufuga Ng'ombe kwenye makazi ya watu.
 
Khaa!! Unaishi wapi bana? Kila mji una sheria ndogondogo kuhusu ufugaji. mtaani kwetu kuna wanoko kama wewe ambao hawataki tufuge hata majogoo eti wanawapigia kelele alfajiri :mvutaji:
 
Kuna dawa ya kuua wadudu inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo na mifugo inaitwa icon 10. inaua inzi, mbu, mende n.k niliwahi kupuliza kwenye kuta kwa nje namadirisha kila mahali kwa miezi 6 mdudu haruki. Itabidi utafute ushauri kwa Dr wa mifugo kabla maana nisumu.
 
Sheria zipo na zinakulinda...! Ila kwa kulinda ujirani mwema tafuta taa za umeme zinazoua inzi funga kwako muuzie na jirani yako kwa bei ya punguzo ili avutiwe kufunga kwake pia.
 
Nenda kule dar mtafute mganga mmoja anaitwa magenge mwelezee kisha rudi nyumbani chukua smartphone yako alafu anza kuchati mida ya saa 6.30 hivi mchana itakapofika 7.00 utaona kama kuna wingu ivi la mvua, ilo sio wingu hao ni Nyuki.

Kumbe wewe ni mwanga.
 
Jaribu kuweka Wavu kwenye Madirisha yako na Milango hapo itakuwa sio rahisi kwa Nzi kuingia ndani, pia mshauri tu huyo jirani yako aache kufuga Ng'ombe kwenye makazi ya watu.

Sawa nashukuru kwa ushauri mkuu...
 
Kuna dawa ya kuua wadudu inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo na mifugo inaitwa icon 10. inaua inzi, mbu, mende n.k niliwahi kupuliza kwenye kuta kwa nje namadirisha kila mahali kwa miezi 6 mdudu haruki. Itabidi utafute ushauri kwa Dr wa mifugo kabla maana nisumu.
organza, nashukuru sana, haswa hiyo dawa nitainunua na kupulizia
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi, kwangu kuna inzi wengi nimejaribu kupulizia dawa lakini wapi, nimekuja kugundua wanazalishwa kwa jirani yangu mchafu na anamiliki ng'ombe, mbwa na paka wa kienyeji. Sasa inzi wanahamia jikoni na sebuleni kwangu kama utitiri. Nisaidieni mbinu za kuwathibiti maana siwezi kumshauri jirani auze mifugo wala siwezi kumsisitiza juu ya usafi.
Naomba kuwakilisha.
Hapo kwenye red sijakupata
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom