Msaada kwa aneyeyajua ya jeshini!

Msaada kwa aneyeyajua ya jeshini!

Babu mchumi

Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
62
Reaction score
11
Habari zenu the great thinkers!
Mimi nina degree ya uchumi ya pale mlimani,nina shauku kubwa ya kutaka kujiunga na jeshi JWTZ japo nasikia nafasi ni adimu sana kupata,,lengo ni kutaka kuuliza hivi kima cha chini cha mshahara kikoje,, yaan kwa profesnl na form six!?
Na je kuna challenge gani huko?
 
Mkuu naskia kwa sasa ngazi ya degree unaanzia mshahara wa 1.2M ukiacha marupurupu mengine
 
Habari zenu the great thinkers!
Mimi nina degree ya uchumi ya pale mlimani,nina shauku kubwa ya kutaka kujiunga na jeshi JWTZ japo nasikia nafasi ni adimu sana kupata,,lengo ni kutaka kuuliza hivi kima cha chini cha mshahara kikoje,, yaan kwa profesnl na form six!?
Na je kuna challenge gani huko?

Kwanza kajiunge na ulinzi shirikishi upate uzoefu
 
Unasikia lakini huna hakika..na degree yako kama huna cheo usitegemee hiyo hela

Trust me, I grew up in millitary baracks. Sasa unafikiri kama umeenda officer cadet ambayo its obvious lazima uende kama wewe una degree, utakosaje cheo?
 
Habari zenu the great thinkers!
Mimi nina degree ya uchumi ya pale mlimani,nina shauku kubwa ya kutaka kujiunga na jeshi JWTZ japo nasikia nafasi ni adimu sana kupata,,lengo ni kutaka kuuliza hivi kima cha chini cha mshahara kikoje,, yaan kwa profesnl na form six!?
Na je kuna challenge gani huko?

Kwa hiyo elimu yako (degree) kama ukifuzu cozy ya uafisa (TMA Monduli),utaanza na cheo cha luteni (nyota mbili)....

Mshahara (take home) utaanza na 1.6M Month,lakini kuna marupurupu na posho...

Changamoto zilizopo ni kwamba cozy officer cadet si ya kitoto,ni ngumu kiasi kwamba huwa inalinganishwa na mabawa mawili ya ukomando....

Kuhusu nafasi za ajirs,nahisi bado haujachelewa coz jeshi linauhitaji mkubwa wa wasomi ili kuongeza ufanisi katika chombo hicho...
ALL THE BEST COMMANDER
 
Last edited by a moderator:

Asante mkuu kwa kunyoosha maelezo.
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu kwa kunyoosha maelezo.

USHAURI TUU!!
Kama kweli una nia ya dhati ya kujiunga na jeshi,nenda makao makuu ya JKT (dsm)...utakutana na vijana wadogowadogo lakini ni maafisa,unaweza kusocialize nao wakakupa details za kuanzia (wale madogo wako poa,wachangamfu alafu hawana wivu wa maendeleo)
 
Kaka ngoja mi nikuchane makavu, mi nilikua JKT miezi mitatu iliyopita kwa mujibu wa sheria.. sasa mkuu kule mambo co ya kitoto, yaani inabidi ufungue moyo kuna usumbufu na kero nyingi saaana akyamama kila siku ya maisha yako lazima kuna mtu atakufanyia jambo ambalo hutolipenda na utachukia,, Inahitaji uvumilivi mkubwa saana na ucwe mtu wa kukacrika mapema.. kazi kwako.. kuna PT, ROOTMARCH, SIX WEEKS ZA KUKESHA, KWATA vyote vinaboa Dah yaan we nenda tu ila fungua moyo. kunywa maji mengi..
 
Ni above 1m nje ya posho ila lazima utambue una miaka mitatu kama sio miwili kuifikia hiyo pesa
 
Mimi sijasiki nchi inayoanzisha kozi ya miezi mitatu ya kijeshi ambapo vijana wadogo makuruta wanatakiwa wajue kila kitu kwa muda huo mfupi.matokeo yake ni hayo mateso mnayoyapata na hata kusababisha vifo kwa vijana wetu.jkt kwa mujibu wa sheria imeanzishwa kiholela kama kambi za wakimbizi.bajeti yao ni finyu,miundo mbinu mibovu,vijana wamerundikwa kama nyanya na kuambukizana magonjwa ya mlipuko kama vile uti wa mgongo.pia kuna mazingira hatarishi kiasi kwamba kuna taarifa kwamba kuna waliofukiwa na vifusi huko masange jkt tabora.kwa taarifa hii angalia jamii forum ya tarehe 25.8.2013.huko huko jkt kuna wanaosulubiwa huku wanaumwa na hawapewi matibabu.mfano hai ni kifo cha mtoto wangu halima rehani aliefariki huko masange jkt tabora na huku wauaji hawa wakijaribu kwa nguvu zao zote kuficha sababu za kifo chake.mbali ya hayo kuna tetesi za vifo vingi zinazotisha.kwa haya yote hakuna anaejali na ndio kwanza wana mpango wa kuongeza idadi ya vijana huko jkt kutoka elfu kumi hadi elfu orobaini.je kwa matayarisha haya duni watakufa wangapi?haraka yote hiyo inayogharimu maisha ya vijana wetu ni ya nini?au mradi wa ibada za ki freemason za kuua watu bila ya kujali ndio umeanzishwa huko jkt?
 
Duh!!pole sana mkubwa kwa kufiwa na mwanao.
 
cheo ndo kinamata sasa nyie ungopeanane,usiingie jeshini kwa kufuata mkumbo mtajuta,au umekosa ajira sasa na kufanya ndio kimbilio
 
hakunaga mishahara kama hyo ,hao wote hawa hawanauhakika jaribu kuwachek wahusika wenyewe
 
Back
Top Bottom