Msaada kwa anayekijua chuo cha NIT

Msaada kwa anayekijua chuo cha NIT

Itakuwa imeombwa na watu weng sana ndo maana wameitoa
Labda aisee ila Nacte hawapokei simu bhana... kuna matatizo mengi eti.. ningekuwa Dar ningeenda ofisini kwao. Mfano kuna kozi guidebook inaonyesha ni priority na ada ni 1.2m lakini pale kwenye machaguo sio priority na ada ni 1.6m.
 
Mi huwa nawashauri wanafunzi kuchagua vyuo vilivyo stick kwenye kozi maalum,
Kwahiyo NIT kwenye koz za transport na procurement nikizuri.
 
Changamoto zipo lakini ni za kawaida kama vyuo vingine na hizi changamoto nadhani kwa kuwa miaka ya karibuni wameanzisha course nyingi hivyo kupelekea kupokea wanafunzi wengi. 1. Madarasa ya kusomea, hii inapelekea kusoma kwa shift unaweza kukuta mnasoma mwaka mmoja lakini unakuta wengine wanamalizia muhula wengine wapo likizo hivyo hivyo. 2. Sehemu za kulala pia ni changamoto kuna uwezekano wa jukosa hostel za chuo hivyo ajiandae kupanga hostel nje ya chuo. 3. Changamoto ya ngono ni kawaida sehemu zozote zile. 4. Vibaka upande wa usiku ajichunge sana anapokua anatoka nje ya chuo kipindi cha usiku. Mazingira yapo poa tu kwa kusomea hasa kipindi hichi cha kiangazi maana wametengeneza vimbweta vya kusomea vingi tu chini ya miti kuzunguka chuo. 6. Chuo kipo mjini hivyo changamoto za mjini za kawaida. 7. Chuo kipo karibu na soko hivyo la vyakula la mabibo. 8. Walimu wapo poa tu. 9. Maktaba pia ni changamoto maana maktaba iliyopo ni ndogo lakini watu wanashea hivyo hivyo na mambo yanakwenda lakini nahisi wanlifanyia kazi hilo
hongera mkuu umeelezea vizur lkn umesahau changamoto ya mkopo kucheleweshwa sana
 
Changamoto za kawaida tuu.
Mpe hela za vitini za kutosha maana hiyo course ina matirio mpaka inakera...
Kama ana uwezo wa kupanga ni vizuri zaidi maana vijana wa hostel hawajambo kwa kusafisha haswa kipindi baada ya semester exams.
Kama ni mzee wa vizenga imekula kwake maana akidakwa sasahivi hakuna msalie mtume kuna deputy mkuu wa chuo huyo ni bad news.
All in all kama atakutana na waalimu vijana (maana wameajiriwa wengi lately) asiwaletee kujua sana atasup mpaka anaingia kazini.
 
Wakuu kwa habari ya admission letter inakaaje na nimejalibu kuingia email ya chuo olaaaa
 
Chaguliwa kwanza maana kupata NIT hasa kwa transport ni mziki
 
Back
Top Bottom