Habarini wanajamvi! Najua hapa ni msaada wa kila kitu! Mimi nina sehemu yangu nahudumia watu sasa nina watu zaidi ya 2000 ambao nimewasave namba zao za simu na majina yao! nimewasave katika MICROSOFT EXEL hawa watu nahitaji kuwatumia SMS moja iende kwa Watu woteee Zaidi Ya 2000 je njia gani nitumie ambayo ni Rahisi zaidii! Nikifikiria kuanza kuandika majina Yote 2000 na kuyasave katika Simu yangu itanichukua mda mrefu sana sana! Sasa njia ipi ni rahisi?
je kuna njia rahisi ya kuhamisha haya majina toka kwenye Exel kwenda kwenye phonebook yangu? au kuna njia yoyote rahisi ya kuwatumia hawa watu ujumbe?
Msaada tafadhari
Kama unahitaji njia rahisi tumia na utume msj zako kupitia simu endapo una kifurushi cha meseji za kutosha then Google Contacts;
Kwenye hyo Excel sheet yako fanya hivi:
1. Uwe na column mbili column moja yenye majina ya watu na ya pili namba za simu
2. Column ya majina ipe title/heading ya "Given Name", column ya pili ya namba za simu ipe title/heading ya "Phone 1 - Value"
3. Baada ya kuweka hzo column names, nenda File->"Save as" halafu chagua CSV(Text CSV) halafu usave kama CSV kwenye location utakayokumbuka
4. Ukishakuwa na CSV yako ingia Google Contacts kupitia
contacts.google.com then click "Go to the old version".
5. Ukifika kwenye old version ya Google Contacts nenda "More" halafu "Import" then uchague ile CSV yako uliyosave mwanzo
6. Ikishamaliza kuimport ni vizuri kutengenezea Group mpya hizo contacts ili kuzitenganisha na contacts zako zingine kama zipo kwa hyo select zote halafu click "Groups"->"Create New" halafu uconfirm ili zote ziwe kwenye Group moja.
7.Baada ya hapo kama email account uliyotumia hapo juu haipo kwenye smartphone yako nenda kwenye nenda Settings->Accounts->Add account click Google, ingiza details zake, baada ya hapo "Sync Contacts".
8. Ikishamaliza kusync contacts namba ulizoimport kwenye Google account hapo juu zitatokea kwenye simu yako na utaweza kutuma meseji kwa contacts zote hzo kama group moja