Msaada kupata/kusafirisha bidhaa kutoka Kenya

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
2,322
5,946
Wakuu habari,
Nina shida ya kupata bidhaa kutoka kenya, utaratibu upo vipi kusafirisha, kuna material nimezi spot kenya nahitaji kuzileta bongo, nimewasiliana na muuzaji tayari, sasa nahitaji kufahamu ni njia ipi nzuri nitumie ili niweze kuzipata.

NB:
Wale wa Tz vs ke naomba mkae kando.
 
Mkuu wasiliana na mkenya ambaye unanua bidhaa kutoka kwake ili ujue jinsi anavotaka kupokea hela zake. Ukifanya biashara yote hii kupitia benki kila kitu kitakuwa rahisi. Benki itakupa fomu muhimu ya Import Declaration ambayo humo ndani inaashiria aina ya bidhaa, malipo ambayo unatakiwa ulipie bidhaa zenyewe n.k, n.k. Equity huwa wako very fast na ukianza process yenyewe leo hii ikifika jioni watakuwa wametuma fomu yenyewe Dar kwa TISCAN, kampuni ya inspectors ya kitanzania ya kushughulikia imports za aina hizi. Ukisha wasiliana na TISCAN uanze shughuli ya kuzisafirisha kutoka Kenya. Upande wa Kenya hutapata stress nyingi. Utapata usaidizi wote na fomu zote sehemu moja, Huduma Centre iwe boda pale Sirare, Namanga au Nairobi na watakushauri kuhusu malipo yeyote ya ziada.
 
Inalingana na kile unachotaka kununua. Hata hivyo, ungefwata kile ambacho pingli-nywee amenena
 
Nilitaka kumueleza afafanue zaidi kuhusu bidhaa anazotaka kusafirisha ila nikakumbuka hii ni Jf na hata mimi mwenyewe huwa sipendi kabisa kuanika shughuli zangu hadharani. Akianza shughuli yenyewe kama nilivomueleza hapo juu nadhani atafanikiwa bila stress nyingi.
 
Mkuu wasiliana na mkenya ambaye unanua bidhaa kutoka kwake ili ujue jinsi anavotaka kupokea hela zake. Ukifanya biashara yote hii kupitia benki kila kitu kitakuwa rahisi. Benki itakupa fomu muhimu ya Import Declaration ambayo humo ndani inaashiria aina ya bidhaa, malipo ambayo unatakiwa ulipie bidhaa zenyewe n.k, n.k. Equity huwa wako very fast na ukianza process yenyewe leo hii ikifika jioni watakuwa wametuma fomu yenyewe Dar kwa TISCAN, kampuni ya inspectors ya kitanzania ya kushughulikia imports za aina hizi. Ukisha wasiliana na TISCAN uanze shughuli ya kuzisafirisha kutoka Kenya. Upande wa Kenya hutapata stress nyingi. Utapata usaidizi wote na fomu zote sehemu moja, Huduma Centre iwe boda pale Sirare, Namanga au Nairobi na watakushauri kuhusu malipo yeyote ya ziada.
Wewe sio TZ vs KE?
 
Ikifika wakati wa kusaidiana kwa hali na mali mbona tusisaidiane?. Hayo mengine huwa matani tuu, wewe unadhania tukipatana na wewe hapa Kenya ama popote pale hatuwezi saidia juu ya ushindani wa JF?. la hasha .
Sio kusaidiana, kuna mtu anapigania doo ya saro utafikiri yupo kwenye third world war
 
Wewe sio TZ vs KE?
Hahaa! Sidhani, kozi ya Tz vs. Kenya niliikamilisha kitambo sana. Utotoni enzi zile nikisoma na watz, tulikuwa tunabishana kuhusu rangi za bendera zetu na wimbo wa taifa na kwa miaka mingi wenzako walikuwa wanapenda kumsifia bondia wao.(alikuwa anaitwa Matumla au?) Alafu tukiwazidia na stori za wachuna ngozi, ambazo zilikuwa zimevuma enzi hizo, walikuwa wanaanza kuimba wimbo flani hivi. "Taaanzaniiia Tanzaniiiaa nakupenda kwa moyo woteee, nchi yangu Tanzaniiiaa jina lako litamu sana weee!...niamkapo asubuhi nakuwaza eweee wanguuu" . Utoto raha sana maanake hakukuwa na chuki za aina yeyote ile. Sasa hivi mimi ni mtu na akili zake na hizi ligi za Jf huwa nazichukulia kama utani tu. Isipokuwa hapa kuna wale ambao wamejawa na chuki kweli kweli.
 
Wazee wa ligi ,tz vs kny tunavokatazama haka ka uzi! Tunasubiria hapa pembeni tu
wanasemaga kadamshee...singida- dodoma, mtwara na kigoma-ma-ma

FB_IMG_1508561210802.jpg
 
Ikifika wakati wa kusaidiana kwa hali na mali mbona tusisaidiane?. Hayo mengine huwa matani tuu, wewe unadhania tukipatana na wewe hapa Kenya ama popote pale hatuwezi saidia juu ya ushindani wa JF?. la hasha .
Mtoa mada amesema waziwazi, hataki tz vs ke hapa. Sasa nashanga mjomba pingli- nywee kawahi kiti cha mbele.
 
Hahaa! Sidhani, kozi ya Tz vs. Kenya niliikamilisha kitambo sana. Utotoni enzi zile nikisoma na watz, tulikuwa tunabishana kuhusu rangi za bendera zetu na wimbo wa taifa na kwa miaka mingi wenzako walikuwa wanapenda kumsifia bondia wao.(alikuwa anaitwa Matumla au?) Alafu tukiwazidia na stori za wachuna ngozi, ambazo zilikuwa zimevuma enzi hizo, walikuwa wanaanza kuimba wimbo flani hivi. "Taaanzaniiia Tanzaniiiaa nakupenda kwa moyo woteee, nchi yangu Tanzaniiiaa jina lako litamu sana weee!...niamkapo asubuhi nakuwaza eweee wanguuu" . Utoto raha sana maanake hakukuwa na chuki za aina yeyote ile. Sasa hivi mimi ni mtu na akili zake na hizi ligi za Jf huwa nazichukulia kama utani tu. Isipokuwa hapa kuna wale ambao wamejawa na chuki kweli kweli.
Mimi napata tabu sana kuamini eti wewe umeacha ligi ya tz vs ke. Nikipitia post zako chache tu nyuma nona bado zina rangi ya tz vs ke.
 
Acha zako wewe, mbona watu wa ligi za 24/7 tunawajua vizuri? Kama mimi sifai, basi pia wewe ndio captain na ingefaa upigwe ban kwenye uzi huu.
Haha, ukitaka nipigwe ban peleka maombi kwa JF ukiambatanisha na vielelezo. Tena utakuwa umenisaidia sana kupata muda wa kufanya mengine maana hii JF inakula sana bundle yangu na muda pia.
 
:D:D:D JF ni kama mlevi na pombe aina ya pingu, kabla hujaanza kunywa unafungwa kwanza kamba kwenye suruali miguuni maana ukilewa kinachofuata uharo... Kuna muda huwa naamua nisiweke bando lakini kila nikikumbuka mijadala ya humu uzalendo unanishinda...
 
Mimi napata tabu sana kuamini eti wewe umeacha ligi ya tz vs ke. Nikipitia post zako chache tu nyuma nona bado zina rangi ya tz vs ke.
Dah! Leo umeniamulia sio bure. Hivi unatarajia mzalendo kama mimi nikalie fence kila mara ndio waniite tikiti maji kama Kalonzo Musyoka? Wakati mnaishambulia nchi yangu? Mijadala ya kutupiana vijembe huwa ina utamu wake wa kipekee ila chuki sina kabisa ndugu yangu. Alafu ukiendelea na hii offensive yako dhidi yangu ntaongea na mawakili wangu jombaa.
 
Bora ungetaja kabisa nini unataka kuagiza, maana kila kitu kina mfumo na mkakati wake. Kunazo hata hutumwa kwa Dar express hayo mabasi ya Dar to Nairobi.
Lakini uwe makini maana upande wa Tanzania wanatia viberiti hata vifaranga, japo umesema wazee wa ligi tukae pembeni ila ni muhimu kukumbushia tu, kale kachuki ka watu wenu katakupeleka hasara hadi utamani kujitoa uhai.
 
Back
Top Bottom