MSAADA Kuna umuhimu gani wa kuusoma Mara ya kwanza/ mara ya pili Muswada wa mapitio ya katiba pya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MSAADA Kuna umuhimu gani wa kuusoma Mara ya kwanza/ mara ya pili Muswada wa mapitio ya katiba pya?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by silver25, Nov 17, 2011.

 1. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wadau nimekuwa nikifuatilia Bunge kwa umakini sana na Kuona Chama cha demokrasia na Maendelea CDM wakitoka nje kwa kukataa kuendelea kujadili muswada wa Mapendekezo ya Katiba mya kwa kutaka usomwe kwa mara ya Kwanza.. wakimaanisha uli ulio somwa kwa mara ya kwanzqa ulikataliwa na wabunge wote kwasababu uliandikwa kwa Lugha ya Kiingereza kwa maana hiyo ni Zero. kama wameanza upya.

  Bado sijajua Faida zake je Munaweza niaidia ili namimi nikiona wanatoka nijue labda wanania ya Kutusaidia sisi Watanzania au wanania ya kuuchelewesha uhondo wa katiba itakayo tusaidia sisi wananchi wa chini? nitafurahi sana kupata details za kutosha
   
 2. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa katiba hii iliyopo: A proposal for a new law i.e BILL should be read twice before the house of representatives. Kusomwa kwa mara ya kwanza ni kuruhusu amendments toka kwa wabunge na wadau wengine. Baada ya kusomwa huku, yale mapendekezo hurudishwa ktk CABINET kufanyiwa marekebisho ikiwa Rais (Head of the Cabinet) ataona mapendekezo hayo yanafaa. Baada ya maboresho (au bila maboresho) muswada huo utarejeshwa kwa mara ya pili kuangaliwa vipengele vilivyofanyiwa marekebisho ili kuruhusu more amendments. Na baadae tena mswada unarudishwa kwa Rais na baraza la mawaziri wataangalia tena mapendekezo ya wabunge. Kama wabunge wameukubali, Rais atausaini na tangu hapo mswaada huo unakuwa SHERIA. Na ikiwa wabunge wameugomea kwa mara ya pili, Rais analazimika kulivunja bunge.

  ISHU YA KATIBA: Muswada wa uundwaji wa tume ya kuratibu uandikwaji wa katiba mpya ulipelekwa bungeni kwa lengo la kusomwa mara ya kwanza. Kweli ulisomwa, lkn ulikataliwa na wabunge wote kwa ujumla wao kwa sababu kuwa na mapungufu makubwa yaliyosababisha hata usijadilike. Kengo lilikuwa uandikwe upya kwa misingi yenye kujadilika. Serikali ikaurejea na kuuandika upya kwa kiswahili na ndio juzi hapa wameupeleka tena bungeni. Mzozo uliopo ni serikali kuusoma kwa mara ya pili, badala ya mara ya kwanza. (ukumbuke mswada husomwa mara ya kwanza kuruhusu amendments, sasa huu haukufanyiwa amendments bali structure yake ndio iliyokosolewa). Wanachodai CHADEMA na wanaharakati ni kwamba, taratibu za msingi za kuunda tume ya kuratibu uchukuaji maoni, ndio msingi wa ufanisi wa shughuli yenyewe na hii ni kweli kabisa. Sasa kama jambo hili litafanywa kwa makosa, hata maoni yatakayotolewa hayatakuwa na faida sanasana yataishia mikononi mwa Rais ambaye amepewa mamlaka ya kuamua nini afanyie maoni hayo.

  Kwa mtazamo wa haraka haraka wa katiba ya zamani, madaraka makubwa aliyonayo rais ndio tatizo la maendeleo ya nchi yetu. Sasa hofu ya wanaharakati (na watanzania wote wenye kuelewa nini kinaendelea) ni kwamba hata uundwaji tu wa tume ya kuratibu upatikanaji wa katiba mpya tayari unahodhiwa na serikali badala ya wananchi. Kwa hiyo summary ya huu mzozo ni kwamba, muswada ule unasomwaje kwa mara ya pili ikiwa haukusomwa mara ya kwanza?

  Ukilitafakari hili utagundua kuwa CCM bado hawana nia ya dhati ya kuona uwajibikaji unakuwa sehemu ya utamaduni wetu. Na ndio maana hawako tayari kuona tuna mamlaka ya kumwajibisha kiongozi
   
 3. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru sana Mdau kwa maoni yako ya kina sana nakuhakikishia nimeelewa vya kutoha kwanini CDM wanaukatalia huo muswada kusomwa kwa mara ya pili.. so unadhani juhudi zao zitafanikiwa? maana naona kabisa kunahaja ya Watanzania kuwaunga mkono kwa kuandaa maandamano ya kuupinga uamuzi wa CCM na CUF kulazimisha kuendelea na maadhimio yao
   
 4. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Awali ya yot nataka ufute ndoto ulizo nazo kuwa kuna mtu/watu ambao wanaweza kukuletea katiba ambayo itakusaidia wananchi wa chini kama ulivyo dai katika swali lako; ni muhimu kila mmoja wetu akashirik katika mchakato huu tokea mwanzo hadi dakika ya mwisho pasipo kutoa fursa au mwanya wa kuaminiana kama ambavyo CCM, CUF na TLp wanataka tuendelea watanzania waendele kufanya kama walivyofanya katika miaka 50 iliyopita.

  Kama alivyosema ndg Kibamba katika BBC jana haramu haiwezi kuza halali hat siku moja. Matatizo karibu yote yanayoikumba Tanzania na watanzania chimbuko lake ni mapungufu yaliyomo ndani ya Katiba za nchi mbali mbali ambazo zimekuwa zikitumika mkuanzia ya kwanza kabisa miaka ya 60 ambapo hapa lazima nimlaumu Mwalimu Nyerere kwa kuanzisha huu utaratibu wa kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kushirikishwa katika uundajwaji wa Katiba. Miswada yote ya Katiba na marekebisho yake tokea tupate uhuru imekuwa ikifikishwa bungeni chini ya hati ya dharura. Hii maan yake ni muswada kusomwa na na kuanza kujadiliwa na wabunge hapo hapo na kwa haraka na kupitishwa siku hiyo hiyo. Ipo katiba moja nafikiri ni ile ya 1977 ilijadiliwa na wabunge watatu tu kama sijakosea.
   
Loading...