Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Candid Scope, Mar 31, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  KAMA vile imeshindwa kusoma alama za nyakati, serikali imeamua kuchakachua mchakato wa marekebisho ya katiba mpya kwa kuandaa muswada ambao unapinga yote yanayopendekezwa na wananchi.

  Badala yake, serikali inarejesha yote yanayokataliwa na wadau, hali ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi na hatimaye kusababisha mchakato mzima kurudiwa huko mbele.


  Mabadiliko ya katiba ni madai ya msingi na matakwa ya lazima kama nchi hii inataka kujenga na kudumisha amani ya kweli na kuleta maendeleo kwa watu wake.


  Katika mazingira ambamo wananchi wamekuwa wanalalamikia mamlaka yaliyopitiliza ya rais, kama kikwazo cha maendeleo na badiliko la msingi katika katiba, muswada wa sasa unaoletwa na serikali, unalenga kuendelea kusimika mamlaka hayo.


  Uchambuzi uliofanywa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), ambaye awali ndiye alidhamiria kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu mchakato wa katiba mpya, unaonyesha kuwa muswada huo uliochapwa katika gazeti la serikali toleo No. 1 Vol. 92 la tarehe 11, Machi 2011, unataka kumpa rais mamlaka ya kuunda tume ya kuongoza mchakato mzima wa katiba bila kuhusisha Bunge ama wadau wengine wa msingi.


  Wakati wanaharakati na wananchi kwa ujumla wamekuwa wanasisitiza wananchi wawe na mamlaka ya mwisho katika kuamua hatima ya katiba yao, muswada huu wa serikali unarejesha mamlaka hayo kwa rais.


  Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011 unatarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni, na CCM kwa kutumia wingi wa wabunge wao, wanaoiunga mkono serikali hata kwa masuala wasiyokubaliana nayo, wanatarajiwa kuunga mkono muswada huo, kuhujumu mabadiliko makubwa ambayo taifa lingefanya baada ya miaka 50 ya uhuru.


  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ambayo gazeti hili lina nakala yake, mbunge huyo wa Ubungo anasema:

  "Maudhui ya muswada huu yamedhihirisha tahadhari niliyotoa mara kadhaa kwamba serikali haina dhamira ya kweli ya kuhakikisha panakuwepo na mchakato mzuri wa kuwa na katiba mpya.

  "Muswada huo umelenga kuhalalisha yote ambayo yalitangazwa kufanywa na rais kuhusu mchakato wa katiba mpya na kupingwa na wadau mbalimbali; sasa yanataka kupewa uhalali kwa sheria inayotaka kutungwa na Bunge kupitia muswada huo.


  "Muswada huo unataka kumpa mamlaka rais ya kuunda tume ya kuongoza mchakato mzima wa katiba bila kuhusisha Bunge ama wadau wengine wa msingi. Muswada huo pia utaka kumpa rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa tume husika bila kushauriana na mtu yeyote isipokuwa Rais wa Zanzibar.


  "Muswada huo unaelekeza kuwa katika kuteua wajumbe, rais atazingatia uwakilishi wa makundi ya kijamii, lakini makundi husika hayatajwi hata kwa ujumla wake, hivyo kuacha mamlaka yote ya kuamua uwakilishi kubaki kwa rais.


  "Muswada huo unataka kumpa rais mamlaka ya kutengeneza hadidu rejea za tume, jambo ambalo lilipaswa kufanywa na Bunge kwa kuwa sehemu ya sheria husika ama kufanywa na mkutano mkuu wa kikatiba. Kwa kutoa mamlaka ya kuunda hadidu rejea kwa rais, mwanya umetolewa kwa mtu mmoja kuweka mipaka ya nini kinastahili kufanywa na tume wakati wa mchakato wa katiba mpya, hivyo kuminya wigo wa mabadiliko.


  "Muswada huo unataka tume iwasilishe ripoti yake kwa rais ambaye atampa nakala Rais wa Zanzibar na baadaye kumwelekeza waziri mwenye dhamana kupeleka yale atakayoamua rais bungeni. Muswada huu kwa kuwa na kifungu hiki utaendeleza yaliyofanywa na marais waliopita kuhusu ripoti na mapendekezo ya tume nyingine, hivyo kukwamisha mabadiliko ya kweli.


  "Muswada huo unataka kutoa mamlaka kwa tume itakayoundwa kuitisha jukwaa (fora) ambalo litaundwa kwa ajili ya kupata maoni pekee (ad hoc) badala ya kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa Katiba (National Conference/congress) kama wadau walivyohitaji.


  "Aidha, uwakilishi katika jukwaa hilo umetajwa tu kuwa ni wa kijiografia na kimakundi bila kuweka bayana mnyumbuliko wa uwakilishi. Muswada huo unataka kutoa mamlaka finyu kwa jukwaa hilo kuwa ni kutoa ushauri kuhusiana na muswada; tofauti na mkutano mkuu wa kikatiba ambao ungekuwa na mamlaka zaidi katika mchakato husika.


  "Muswada huo unataka kutoa mamlaka kwa rais kuitisha Bunge la katiba (constituent assembly) ikiwemo kuteua wajumbe wa Bunge husika. Muswada huo unataka kutoa mamlaka makubwa kwa rais kuteua wawakilishi wa chombo kikuu zaidi katika mchakato wa katiba bila kushauriana na kundi lolote ama wananchi kuhusika katika uteuzi ama kuwa na wawakilishi walioteuliwa na makundi yenyewe, mathalani vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za dini, vyama vya wakulima, vyama vya wanafunzi, vyama wa wafanyakazi nk.


  "Muswada huo unataka rais ashauriane na Rais wa Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pekee. Muswada huo unatoa mamlaka makubwa zaidi ya rais kuamua hata kufanya Bunge la kawaida kuwa ndilo Bunge la Katiba, jambo ambalo linaweza kurejesha udhaifu uliofanywa katika mchakato wa katiba inayotumika sasa ambapo umma uliporwa wajibu na mamlaka yake ya kushiriki moja kwa moja katika kupitisha katiba.


  "Muswada huo kwa ujumla haujaeleza muda wa mchakato wa katiba na vipindi vitakavyotumiwa na vyombo mbalimbali katika hatua mbalimbali za mchakato wa katiba; ama kutoa mamlaka ya kuwekwa kwa muda huo kwa chombo chenye uwakilishi mpana wa umma kama mkutano wa katiba au Bunge, hivyo kutoa mwanya kwa mchakato mzima kucheleweshwa.


  "Haya ni baadhi ya maudhui ndani ya muswada husika ambayo yamenishtusha na kunifanya nitoe tamko hili la awali wakati nikiendelea kufanya uchambuzi wa kina ambao nitautolea kauli katika hatua za baadaye."

  Mnyika alitoa wito kwa vyama vya siasa, asasi za kiraia, vyombo vya habari, taasisi za dini na Watanzania kwa ujumla kufuatilia na kupata nakala ya muswada huo ama maudhui yake kwa ajili ya kuujadili kwa dharura na kutoa matamko.

  Sanjari na hilo, alitoa wito kwa serikali itoe taarifa kwa umma namna ambavyo wananchi wanaweza kupata nakala za muswada huo nyeti na sababu za serikali kupuuza maoni mengi ya wadau yaliyotolewa kabla ya kuandaliwa kwa muswada huo kuhusu mchakato unaofaa kuongoza mabadiliko ya katiba katika taifa letu.


  Mara kwa mara mbunge huyo amekuwa akisisitiza kuwa ipo haja kwa mchakato wa katiba mpya kupata uhalali wa umma kwa kurejea ibara 8 ambayo inatamka kwamba, "madaraka na mamlaka ni umma na serikali inafanya kazi kwa niaba na Bunge ndicho chombo kikuu cha kusimamia wajibu huo kwa kutokana na mamlaka ya kikatiba yaliyopo kwenye ibara ya 63(2) na (3) na ibara ya 98 inayohusika na mabadiliko ya katiba."

  Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika hotuba yake bungeni Februari 8 mwaka huu, pamoja na mambo mengine, alieleza kwamba muswada kuhusu mchakato wa katiba utawasilishwa kwenye mkutano wa tatu wa Bunge mwezi Aprili mwaka huu na kwamba utahusu kuundwa kwa tume.

  Makongamano, mikutano na midahalo imekuwa ikifanyika kujadili suala la mabadiliko ya katiba na wanazuoni wamesisitiza mara kadhaa kuwa katiba isiyotokana na matakwa ya wananchi, na isiyopitishwa na wananchi, si ya wananchi.


  Iwapo serikali itapuuza wito huu, itakuwa inalielekeza taifa katika machafuko ya kisiasa, na italazimika kufanya mchakato mpya ili kukidhi matakwa haya ya kisheria katika uundwaji wa katiba mpya.


  Hatua hii ya serikali kuchakachua mchakato wa katiba imedhihirisha pia kwamba Rais Jakaya Kikwete alidandia hoja asiyoijua mapana na marefu yake alipokiri kwamba nchi inahitaji katiba mpya, baada ya wimbo na joto la kisiasa lililoibuliwa na aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA, Dk. Willibrord Slaa.


  Dk. Slaa aliahidi kuwa angeanzisha mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100 za utawala wake. Rais Kikwete hakuwahi kuahidi wakati wa kampeni kwamba angerekebisha katiba.


  Hata hivyo, baada ya wananchi kudai katiba, huku Mnyika akiahidi kupeleka hoja binafsi bungeni kwa ajili hiyo, ghafla Rais Kikwete alitekeleza ahadi hiyo ndani ya siku 100 za utawala wake – hatua ambayo wachambuzi walisema ililenga kuwanyamazisha wananchi na kuipokonya CHADEMA ajenda.


  Hata hivyo, wananchi wanaendelea na mijadala kuhusu katiba mpya; na sasa linaandaliwa kongamano la pili lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), lenye lengo la kuwapa wananchi uelewa wa kutosha ili waweze kushiriki kikamilifu katika mchakato wa katiba mpya.


  Mwenyekiti wa UDASA, Dk. Mushumbusi Kibogoya, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, alisema mada kuu katika kongamano hilo ni ‘Maudhui na Misingi ya Katiba Mpya.'


  "Safari hii tunataka watu waweze kujua zaidi kuhusu katiba, wawe tayari kutoa mawazo ili tume au kamati itakapowatembelea wawe na kitu cha kusema, watakapoachwa hivi hivi hawatakuwa na cha kuzungumza," alisema Dk. Mushumbusi.

  Watoa mada katika kongamano hilo litakalofanyika keshokutwa ni Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga.

   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katiba ni ya serikali au wananchi? Katiba ni ya CCM au raia wa Tanzania?
   
 3. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Issue siyo ya kuwajulisha raia tuu juu ya katiba kuwa wajue nini cha kujibu pindi watakapoulizwa na tume hiyo ya kikwete, jambo la maana hapa ni kuwahamasisha wananchi waikatae hyo tume bali mjadala huu juu ya Katiba mpya upelekwe bungeni kwani kule ndo kuna wawakiklishi wetu!.

  Mara nyingi CCM imekuwa ikifanya maamuzi yake kwa manufaa yao wenyewe na kusingizia kuwa ni maamuzi na maoni ya wananchi kitu ambacho huwa ni uongo mtupu!

  Mi nachoona ni kwamba CCM inafaham fika kwamba maeneo ya Mjini haipendwi na ndo maana sehemu hizo hutawaliwa na vyama pinzani, emu angalia Arusha mjini, Moshi, Mwanza, Mbeya, Dar, Musoma, Shy, nk. Ni dhahiri kwamba imebakiwa na maeneo ya vijijini ambako upeo wa elimu hususani juu ya siasa ni mdogo sana! si ajabu hata wengine hawafahamu nini maana ya katiba na huko ndo kuna idadi kubwa ya wa Tz. CCM kwa kutaka ushahidi usio na manufaa kwa taifa itaelekeza tume hiyo huko vijijini na si katika maeneo ya mijini maana wanfahamu fika kuwa huko watapingwa kwa asilimia zote!

  RAI yangu kwa hilio kongamano ni kuihimiza serikali kufuta huo mswada mara moja badala yake iichie bunge kazi hii ya kujadili juu ya themes zinazotakiwa kuwemo katika katiba mpya, Vinginevyo ni kuitisha maandamano ya nchi nzima juu ya kukataa mswada huo wenye hila ya kutaka kumwachia madaraka makubwa rais!

  Shabashiiiiii ccm, why are you doing that????
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Bunge la sasa haliwakilishi wananchi, kumbuka ni wabunge wangapi wameingizwa humo kwa nguvu ya mabomu ya dola.

  Pili, hili siyo bunge la Katiba; bunge la katiba huundwa maalum kwa kazi hiyo; hapa ndipo unaelezwa kuwa inabidi pawepo na uwakilishi mpana zaidi, si vyama vya kisiasa tu. Si unajua kuwa ili uwe mbunge ni lazima uwe katika chama cha siasa? Je hao wasio katika vyama watawakilishwa vipi ikiwa bunge litaachiwa kazi hiyo?

  Jamani wananchi tunapaswa kujua kuwa katika mambo tunayotaka yarekebishwe kwenye katiba mpya ni kumpunguzia rais madaraka aliyo nayo. Hivi mnafikiri anaweza kukubali kirahisi kupunguza madaraka ambayo anajua fika kuwa ndiyo yanampa nguvu ya kuwa rais na kufanya atakavyo? Kumnyang'anya mtu tonge mdomini si kazi rahisi kama mnavyofikiria! Inahitaji ujasiri - ukiingiza mkono mdomoni atakuuma, nawe unamzaba kibao cha shavu ndipo anafungua mdomo!

  Naomba m-scan huo mswada mtuwekee hapa, najua siyo confidential!
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Haki ya wananchi haiwezi kuchezewa na watu wachache wanaotaka kujinufaisha, na katika hili hatutakubali tena
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  utaratibu wa kuunda katiba ni rahisi sana,

  1. serikali iitishe mkutano mkuu wa kitaifa wa makundi yote ya kijamii
  2. makundi ya kijamii yaunde tume ya kukusanya maoni
  3. tume iandae hadiju za rejea halafu mkutano mkuu wa kitaifa uzipitishe au la.
  4.Tume ya katiba ikusanye maoni nchi nzima kulingana na hadiju za rejea.
  5. tume ikimaliza kukusanya maoni iyapitie na kuandaa majumuisho.
  6. mapendekezo hayo yapelekwe kwenye bunge maalum la katiba kwa ajili
  ya kuidhinishwa tu kwani hawana uhalali wa kupindisha maoni ya wananchi
  kwani wao ni watumishi tu.
  7. baada ya kutoka bungeni yatarudishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa
  kura ya maoni (referendum) na wananchi wote na kama yakipita basi katiba
  inakuwa halali kwa maana imetokana na wananchi wenyewe.

  kinyume na hapa serikali itakuwa inajitakia matatizo yasiyo na msingi kwani wananchi wamechoka kuburuzwa kwani tusingependa kilichotokea nchi zingine kitokee hapa.
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,084
  Trophy Points: 280
  You are right. In fact siku ile Mh. aliposema tume itaundwa niliamini ingekuwa shirikishi kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea Tanzania kama si Afrika. Lakini inaonekana tunataka kurudia yale yale. Hivi kama kweli wana nia ya dhati inashindikana nini kuwa na kitu cha mfano kwa sasa na hata vizazi vingi vijavyo? Hivi mioyo yetu (we Africans) inafungwa na vitu gani hasa?

  Mwaka 2001 niliguswa sana na "Loya Jirga" baraza kuu (Supreme Council) la watu wa Afganistan lililokutana kuamua hatma (Katiba) ya nchi yao baada ya utawala wa Taliban. Baraza hili hujumuisha makundi yote ya kijamii (wazee, makabila, n.k) kutoka pande zote za nchi pale yanapohitaka maamuzi muhimu ya kitaifa kama suala la Katiba lililoko mbele yetu sasa. Chombo hiki (Loya Jirga) kiko juu ya mamlaka zote (serikali, mahakama, bunge, n.k) za nchi na kwa hakika ndicho chombo cha uwakilishi wa wananchi wote na hukutana pale tu kunapokuwa na haja ya kufanya hivyo - mara moja kwa miaka.

  Laiti serikali yetu na CCM wangejifunza kutokana na hili na kutuletea chombo, sio lazima kama hiki, lakini kinachofanana na hiki kwa suala hili la katiba. I am sure serikali, rais, na CCM wangejenga imani kubwa sana kwa wananchi kwa hili and it is their golden chance lakini ndio hivyo tena inaonekana SIKIO LA KUFA.

  Kwa habari ya Loya Jirga bofya hapa: Loya jirga - Wikipedia, the free encyclopedia
   
 8. p

  plawala JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado wao walio wachache wanatuchezea sisi tulio wengi.safari hii tunasema hapana
   
 9. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wananchi,vyama vya upinzani,NGOs na taasisi mbalimbali zimeshiriki wazi kabisa kutoa maoni yao kwa serikali kuhusu katiba ya jamhuri iweje.

  Ila kama basi serikali iliyo madarakani imeona ipuuze hayo raia wa tanzania wanayohitaji,kana kwamba ipo pale kujiwakilisha yenyewe na kusahau waliyoiweka pale kwa niaba yao; itabidi wananchi wenyewe tuamue kutokuwa na imani na serikali.

  Haiwezekani nchi iburuzwe kwa nusu karne na bado tuambiwe tupo huru; uhuru wa kuchangia mawazo hata ya katiba hatuna,haki ya kuchagua mliiona ilivochakachuliwa,uhuru wa kuandamana kutoa kero zetu nao wanataka watunyime...eti tupo huru kweli??

  Tusipo kaa imara kwenye hili la katiba sijui kama tutakuja kuona tanzania ng'aavu,yenye maendeleo kamwe! Tutabaki kuwa mabingwa wa majungu tu,huyu fisadi,huyu ana kile..lakini umasikini utasambaa nchi yote, watafaidi wale wachache. Tuchukue hatua kwenye hili sasa,tusiwaachie wachache wafanye waonavyo wao; na kama tukiamua kuwaachia tujilaumu wenyewe baadae

  Hii nchi nimeichoka,ila sitachoka kuipigania kwani inanihusu sana; nikifikiria taifa la kesho ambao ni watoto na wajukuu zangu sioni sababu ya kukaa kimya,na kuwaacha wachache waendelee kujichana! Kwani huko mbeleni yatakuja matabaka ya wenye nazo na wasio nazo, na hilo gap tukiliacha likue kwa miaka mingine 10 halitakaa kuja kuwa sawa kamwe! Rasilimali zetu ndio hizihizi ambazo leo wanazikomba,kesho keshokutwa tutabaki na nini?

  Tuamue sasa..nawasilisha
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sasa wananchi tupige hatua aidi ya maneno maneno kujiletea mabadiliko tunayoyataka laa sivyo ndio hivyo tutakua tunagongwa tu makusudi barabarani kama yule masikini mwenzetu trafiki na mtoto wa Lowassa na kesi kuendeshwa kama ya Chenge tu.

   
 11. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Nakala ya Mswada huu inapatikana wapi?
   
 12. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wanajamvi chonde chonde ninaomba kama kuna mwanajamvi yeyote anao ho mswada kwa ajili ya katiba mpya atuwekee hapa. Tunahitaji kuelemishana kwa kasi ya sauti au mwanga kuhusiana na huu mswada kama utasitahili kuungwa mkono na tufanye na kama siyo, basi tufanye maamuzi sahihi kabla ya kupitishwa.
  Naomba kuwakilisha.
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wana jf nimelifuatilia kwa makini sana kongamano la katiba mpya lakini nimepata shida sana kwenda nalo sawa kwasababu sijauona mswada wenyewe. Ingawa hata Jaji mstaafu, mzee Samata amesema aliuona jana tu, naamini kuna wana jamii wanaweza kutuwekea hapa ili na sisi tuweze kujadili kwa reference. Tusaidieni tafadhali
   
 14. W

  Wanzuki Senior Member

  #14
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani, kweli kabisa! Ngoja niongeze nguvu ya kuuomba huo muswada! Mwenye nao tafadhali!!
   
 15. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hakika tunahitaji huuu mswada tuudadavue kwa kasi ya ajabu, tukisubiri miujiza ndani ya lile bunge ambapo mwenye maamuzi ya mwisho ni spika; kwa kuhoji wanaoafiki waseme ndiyooooo na wasiyoafiki waseme siyooo. Tutakuwa hatujatenda haki kwa kizazi kijacho. Mdahalo wa mlimani (kwa mujibu wa threads) umedhihirisha kuwa tunaelekea kubambikwa kama hatutapinga kwa bidii zote.
  Mwenye nao chonde chonde atubandikie hapa, tutautafakari hata ktk vilugha vyetu vya kienyeji na kuwatumia ndg zetu huko vijijini ili mradi ktk hili la Tz ijayo tushiriki sote
   
 16. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Nimejiuliza sana na kujizuia kuandika mawazo na hisia zangu. Siku ya leo kama zilivyo siku nyingine ni siku ya huzuni.

  Kama mwananchi najisikia kuangushwa (again I have been let down). Nimejisikia aibu sana wakati wachangiaji walipokuwa wanaongelea muswada wa marejeo ya katiba.

  Niliposikiliza yote waliyozungumza nikabaki najiuliza, je Mh. Celina Kombani na Mh. Jaji Werema wanajisikiaje?

  Kwa muswada huu nafsi zao haziwasuti hata kidogo? Kwa uzembe na ukosefu wa umakini uliojidhihirisha hawajisikii aibu?

  Inawezekanaje jambo ambalo ni sensitive kiasi hiki kufanyiwa mzaha? Tutaendelea hivi mpaka lini? Nalazimika kuamini kwamba viongozi hawa wawili ni wa kuangaliwa upya. Wanapwaya sana.

  Tafsiri mbovu ya sheria aliyoitoa Mh. Werema ilisababisha watu kufa na kupigwa Arusha. Leo tena anaturudisha kule kule. Kwa muswada huu haiwezekani wananchi wakakaa kimya. Haiwezekani.

  Amani na utulivu haviwezi kuendelea kuwepo kama viongozi wetu wataendelea kuwa wazembe na wasio na umakini kama ilivyojidhihirisha kwa uandaaji wa muswada.

  Ni aibu na jambo la kusikitisha. Kama baraza la mawaziri lilipitisha ni aibu kubwa.

  Mwakyembe na Sitta, mnapigana vita ya ufisadi mnaacha vita ya kulinda na kutetea haki za watanzania. Ufisadi mtaushindaje endapo mnaruhusu sheria mbovu kuandaliwa? Uanasheria wenu uko wapi? Hamkusoma huu muswada? Huu ni unafiki.

  Kama wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaweza kuona mapungufu ya muswada huu ninyi mmeyaona? Kwenye Baraza la Mawaziri mlipitisha?

  Dhambi hizi zitakuwa shingoni mwenu viongozi wote mnaosaliti Taifa hili. Amani itakapotoweka kwa sababu mmeendelea kuminya haki dhambi hiyo itawatafuna daima. Msisingizie vyama vya upinzani wala wasomi.

  Mnakera na mnatia hasira sana.

  Ufuatao ni mswada wa Sheria ambayo inapendekezwa kutumika kuelekea Katiba Mpya. Sheria hii ndiyo ambayo iliijadiliwa kwa undani mapema leo Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam katika mjadala wa wazi uliohusisha wanasiasa, wasomi na wadau mbalimbali.

  NB: Angalia ukurasa wa 17 unakosekena (mojawapo ya sehemu za nyongeza); Tunamshukuru Mhe. Zitto kwa kutupatia nafasi ya kuupitia kupitia Blog Yake Hapa. - Mwanakijiji

   
 17. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Unajua ndugu yangu..yawezekana hata kujadiliwa na baraza haukufika huko lakini pia si hata kamati ya bunge imeambiwa ni kitu cha "dharura" hawa ndo watumishi wetu wanaomaliza marupurupu kwa kazi zisizokuwa na maana kwa watanzania...wezi wakubwa!
   
 18. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Asante Mwanakijiji
   
 19. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #19
  Apr 2, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Ahsante mkuu.
  Tuupitie halafu ueledi, busara na hekima zetu zitawale majadiliano.
   
 20. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inawezekana Rweye. Inauma sana jinsi mambo yanavyofanyika. Unajiuliza, ni kwa manufaa ya nani? Wanamfurahisha nani? Wanataka kufanikisha nini? Kwa niaba ya nani? Majibu yote yanaacha maswali mengi zaidi.
   
Loading...