Magonjwa ya kuku na tiba zake

Pritty wa joseph

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
2,380
2,040
MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE

UTANGULIZI
Kuku kama wanyama wengine hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo mengine yanatibika kwa dawa na mengine hayana tiba bali kuku hupewa chanjo maalumu ambayo huzuia magonjwa hayo.Leo nitawaeleza baadhi ya magonjwa ambayo hushambulia kuku mara kwa mara na ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wafugaji wa kuku.

A.) MAGONJWA YANAYOHITAJI CHANJO

1> GUMBORO
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

DALILI ZA UGONJWA
-Kuku kuzubaa na kulundikana, pamoja na kusinzia
-Kuku kuharisha
-Kuwa na vifo vingi kwa kuku

TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa za oxytetracycline hupunguza vifo.

KINGA
wakinge kuku wapo kwa kuwapa chanjo ya gumboro (Gumboro vaccine)

*2> MAHEPE (Marecks)*
Ugonjwa huu husababishwa na virusi*

DALILI
-Kuku hupata ulemavu na vifo vya mara kwa mara.

TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba

KINGA
Chanjo hutolewa kwa vifaranga wenye umri wa siku moja,vifaranga hupewa chanjo ya mahepe (Marecks vaccine)

3>NDUI YA KUKU (Fowl Pox)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

DALILI
-Kuku hupatwa na vidonda kichwani.
-Kuku hupata uvimbe mweupe kwenye mdomo na kushindwa kula.

TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba.

KINGA
Chanja kuku wako wa siku 60-90 kwa chanjo ya Ndui ya kuku (Fowl pox vaccine).

*4>MDONDO (New castle)*
Ugonjwa huu husababishwa na virusi

DALILI
-Ugonjwa huu hutokea kwa ghafla na kuenea kwa haraka
-Vifo vya kuku huwa vingi
-kuku hupumua kwa shida
-Kuku hupooza na kulemaa miguu
-Kuku hupinda shingo yake
-Kuku hupunguza kutaga mayai
-kuku huarisha
-Kuku Kuzunguka zunguka na kutembea kinyume nyume.

TIBA
Hauna tiba

KINGA
Chanja vifaranga wako na kuku wako kwa chanjo ya Mdondo (New Castlef vaccine) na urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.

B.)MAGONJWA* YANAYOTIBIKA KWA DAWA
1>KUHARA DAMU (coccidiosis)(Koksidiosisi
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.

DALILI
-Kuku huzubaa na kujikunyata
-Kuku kuharisha LinkedI chenye damu au kinyesi cha kahawi
-Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa koti
-Kuku hupungukiwa homa ya kula
-Vifo huwa vingi kwa vifaranga

*TIBA*
Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium, au Basulfa.

KINGA
Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu unyevuunyevu katika banda la kuku,

2>HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)
Husababishwa na bakteria

DALILI
-Kuku hupata homa kali
-Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano
-Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye wiki 1-2
-Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula
-Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga mayai yenye ganda laini na hupata vifo vya ghafla

TIBA
Dawa za oxytetracycline kama Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.

KINGA
Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji kwa kuku.
Tenganisha kuku wagonjwa na wazima

C)MINYOO
Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga

DALILI
-Kuku hukonda
-Kuku huarisha
-Kuku hukohoa
-Kuku hupunguza utagaji
-Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri
-Kuku hupungua uzito

TIBA
Tumia dawa za minyoo kama piperazine

KINGA
Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila
baada ya miezi mitatu

D) VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI
Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani kwa sana lakini nao huathiriwa sana.

DALILI
-Kuku kutochangamka
-Ukuaji mdogo wa kuku
-Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au viroboto
-Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu

TIBA
Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao.

KINGA
Boresha usafi wa mabanda ya kuku.

E)UKOSEFU WA VITAMINI A
Huathiri sana kuku wadogo.

DALILI
-Kuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowana.
-Mara nyingi ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi

TIBA
wape kuku wote dawa za vitamini za kuku zinazouzwa dukani.

KINGA
Wape kuku wako mchicha na majani mabichi mara kwa mara.

ZINGATIO
Fuata ushauri wa matumizi sahihi kwa kiladawa pindi ununuapo katika duka la dawa..
 
Coccidissis husababishwa na Virus mkuu ? Nadhani ni protozoa kama sijakosea
 
Vipi kwa mafua ya kuku,dawa yake ni ipi?
Fluban
e5e16e25a24be2f781a960fb15744e09.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom