Msaada Kuhusu zoezi la uhakiki taarifa za Mpiga kura

makofia360

JF-Expert Member
May 28, 2015
776
2,371
Naona ndoto ya kupiga kura katika familia yetu ya watu saba imetanda giza. Hiyo ni baada ya kuangalia kapitia mobile system kwa namba waliyotuelekeza lakini system imeshindwa kutambua namba zetu ikatuelekeza twende ofisi za kata, Hatukusita tukaenda kibaya zaidi taarifa zetu wote hazikuwepo na kwa nilivyoona inawezekana ni watu wengi hawapo. Swali je Kama taarifa zako hazipo hutaweza kupiga kura?

Jamani, hili janga sasa linataka kuletwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)!

Nimekuwa nikisikia tu malalamiko ya watu wengine walioenda kuhakiki taarifa zao katika 'display' ya Daftari la Kudumu la wapiga kura lililoendeshwa katika mfumo wa BVR. Mimi nimeamua nijihakiki mapema kwa njia ya mtandao kabla hata ya hardcopy hazijabandikwa kwenye ofisi za kata yangu, kwani nipo Dar. Nilianza kwa kutumia simu na nikapata majibu kwamba "Tumeshindwa kuitambua namba ya kadi ... ". Sikukata tamaa, nikaamua kutumia njia ya kompyuta, na majibu yake yakaja kwamba "Samahani, Haujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga kura."

Sina shaka yoyote kwamba labda nitakuwa nimekosea kufuata maelekezo ya kuingiza namba za kitambulisho changu, kwani nipo makini na nina ujuzi wa kutosha wa mambo ya IT. Labda tusaidianekufikisha ujumbe huu katika Tume, kwamba something is wrong on their side; they have to come out and say something!

Jaribuni nanyi pia kuingiza namba zenu kama inavyoelekezwa na Tume katika website yao, ili walau tupate picha ya ukubwa wa tatizo.


attachment.php



Nimesoma taarifa ya watu wengi kupitia JamiiForums kwa wale walioenda kuhakiki majina yao lakini cha kusikitisha ni kuwa majina mengi hayapo kwenye daftari. Je, kama hayapo ni kosa la nani?. Je, kama mtu ana shahada ya kupigia kura na jina halipo kwenye daftari Tume inachukua hatua gani.

Nimesoma wengi wanasema kuwa katika kituo kimoja watu mathalani walijiandikisha watu 1,200 lakini majina yaliyopo kwenye daftari ni 40 tu.

Kwa nia nzuri muanze kuchukua hatua mapema vinginevyo sijui wananchi hawatawaelewa kabisa na mwishoni wataona ni njama za makusudi.

Kuna zoezi la uhakiki wa daftari la kudumu la wapiga kura, naomba hili zoezi lisitishwe, kwa taarifa niilizopata ndani ya watu walioshiriki kuandikisha daftari hili, anasema hili ndo goli lenyewe la mkono alilokuwa anazungumzia nape.

Vijana wote wenye umri kati ya umri wa miaka 18-30 yanakatwa kiujanja ujanja, na hayarudi kwenye vituo. Hoja yangu ni kwa nini majina yote ya watu walioandikishwa yasirudi, na mtu alikuwa anachukuliwa taarifa zake zote na finger prints? Kazi ya database ni nini sasa?

Mbona sijawahi kuona bank au taasisi yoyote inayochukua data kama hizo ikisema majina mengine hayaonekani? Na ni kwanini ni majina ya vijana tu? Huu ndo muda wa viongozi wa ukawa kulifuatilia hili suala kwa undani, maana wako bize kuratibu maandamano ya lowassa wakati wapiga kura wao wanakatwa huku.

Zoezi hili lisitishwe kwasababu litakosesha watu wa pande zote haki yao ya msingi ya kupiga kura. Naomba watu wote tuungane kusema HAPANA kwa udhalimu huu unaofanywa na NEC.

Viongozi wa ukawa amkeni! Fuatilieni mambo ya msingi kwanza, kama kumtembeza mgombea hata Kampeni zikianza atatembezwa

====================
====================


Maelekezo


  1. Tumia ukurasa huu kuhakiki taarifa zako kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura.
  2. Ingiza namba kama inavyoonekana kwenye kitambulisho chako cha Mpiga kura,Mfano T-1000-1000-100-0.
  3. Baada ya kuingiza nambari ya kitambulisho cha mpiga kura bonyeza kitufe kilicho andikwa "Tafuta".
Link: http://voters.nec.go.tz:8081/vote/

Angalizo kwa UKAWA kuhusu jina kutoonekana kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Ndugu wanajamiiforums kuna uwezekano mkubwa Idadi kubwa yaWatz wakakosa kuwapigia kura
/kuwachagua viongozi wanaowataka hii inatokana na ukwelikuwa wako watu wengi ambao wamejiandikisha na mara wanapoenda kufanya uhakiki majina yaohayaonekani! Nilimsikia Mh. Duni Haji akisema kuwa wilaya ya Siha peke yaketakribani watu 6,000 hawapo kwenye daftari!

KAULI YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI WA NEC- Ndugu Kombwey Kailima
Wakati hayo yakiendelea Kombwey amehojiwa na bonge wa Cloudsakasema sheria inataka mtu ambaye jina lake halipo aende kwa mkurugenzi wawilaya/halmashauri husika alipojiandikisha ampe malalamiko yake then mkurugenzindo atashuhglikia tatizo hilo! hivi hii ni practical kweli?

USHAURI WANGU KWA UKAWA
Ni vema viongozi wa ukawa wakafuatilia jambo hili kwaumakini mkubwa kwa kuwa NEC iko chini ya serikali ya CCM mathalani kwa mfanoNEC wanao uwezo wa kuchuja/kusort/kufilter majina ya waliojiandikisha kwakuzingatia umri, jinsia, mkoa, wilaya na hata majina ya ukoo! Hivyo basi kama NEC kwa mfanowakipewa maagizo toka JUU kuwa mfano wilayaya Kinondoni watu wenye umri wa miaka 18-40 wapunguzwe kwenye daftari kwaasilimia 30, uwezekano wa jambo hili kufanyika upo.

Viongozi wa Ukawa wanapoona CCM wanajiamni na maneno kamagoli la mkono linasemwa hadharani wajue HAWATANII.

UKAWA mnapoendeleakufurahia mahudhurio/mafuriko ya watu kwenye mikutano yenu mkumbuke kuwa REFA,UWANJA ni wa CCM. Hakika kama mtadharau hatua hii muhimu ya kuhakikisha kilaaliyejiandikisha anapata haki yake mtakuja kuupika mbichi!

Hivi mnafikiri Kombwey kapelekwa pale kimasihara he has special assignment to do. Hivi hao watu ambao majina yao hayaonekani kwenyedaftari wameelimishwa ni hatua gani wazichukue?

Naomba ieleweke kuwa siwalaumu ukawa lakini huu si wakati wakufurahi wingi wa watu kwenye events ni wakati wa kupambana kufa/kupona. Kila kura 1 ina maana kubwa sana kwa ukawa.

Mathalani wanajeshi wote/askari wote mamlaka ya juuimehakikisha taarifa zao zipo sawa na wapo kwenye daftari! na hili nimelijua baada ya kuzungumza nawanausalama hao.Hivi ni lini hii iliwahi kutokea TZ? kama sio CCM washausoma mchezo

Hakika majina kukoseka kwenye daftari kuna baraka toka juu, haiwezekani watu wengi wakakosekana kiasi hiki Mf. Siha Tz si ya kwanza kutumia tech ya BVR na kwenye BVR system kuna facility ya kuexport data kwenye word/excel sasa how comes wamiss watu wengi namna hiyo. Lazima NEC watakuwa wanafanya data sabotage kwa maelekezo toka juu.Na hakika hapa ndipo goli la mkono lilipo maana mamlaka ya juu inajua kuwa wakiwazungusha kwenye hili wengi watakata tamaa.


Mimi binafsi na wanaonihusu tutahakikisha tunatumiakikamilifu haki zetu hatutokubali kupokonywa haki zetu.

Ahsante kwa kuwa kuna Mungu ambaye hizo mamlaka za juu hazifui dafu mbele yake.Tukitimiza wajibu wetu na tukasimama na MUNGU wetu hakika mabadiliko yenye tija yatakuja Tz.


Mungu tubariki

Mungu ibariki Jamiiforums

Mungu ibariki Tanzania
 
Mkuu hii ni shida kubwa naona goli la mkono limeanza. Hapa Iringa watu wengi wamekuta majina yao hayamo kabisa pamoja na kwamba wana vitambulisho. Viongozi wa vyama inabidi waingilie kati vinginevyo..
 
Huku yani ni shida katika kata na majina niliyoyaona hayazidi 40 na watu walijiandikisha wengi kweli,,,natafakari kwa mfumo wa bvr ilikuwa na ulazima wa kuhakiki kweli? lisipo angaliwa hili tatizo hatutapiga kura wengi
 
Sijajua ila ukikuta jina halipo c unampa kitambulisho akujumuishe kwenye daftari la mpiga kura
 
Aisee nilifikiri mi peke yangu!
Mi nimemfuata diwani nikamweleza,akasema haina shida kura nitapiga tu,cha muhimu ni kwenda kuangalia jina km lipo kwny daftar yatakayobandikwa ulipojiandikishia
 
Huku kwetu Iringa jamaa wa NEC wamekuja kimya kimya na wananchi hatukupewa taarifa. Kwenda leo tunasikia wameondoka jana. Kuangalia majina mengi hayamo ingawa vitambulisho tunavyo, huko kwingine kaa chonjo
 
Hilo limetokea pia mtaani kwangu ambapo watu 1080 waliandikishwa lkn ni majina 269 tu ndio yaliyoonekana kwenye daftal. Hili ni tatizo tena kubwa
 
Ok ndugu viongozi bila shaka mmelisikia hilo tatizo, tunataka majibu otherwise siku ya uchaguzi patachimbika...mimi najua hili zoezi la uhakiki linaloendekea ni kucheck makosa labda kwenye herufi za jina, au jinsia au tarehe ya kuzaliwa e.t.c Ila sitegemei eti jina la mtu lisiwepo wakati ana kitambulisho kinachoonesha Kata na kituo alichojiandikishia..
 
Nasikia eti walioenda kuhakiki ndo siku ya kupiga kura wataambiwa wameshapiga. Kuwa makini
 
makofia360 naomba uirudie ile namba ya NEC tena maana nimeisahau
kwani hata mm nilishaitumia mara ya kwanza na majibu ya Tume ni kuwa namba yangi haipo niende kwenye kituo cha Kata kuhakiki tena
 
hivi hamkwenda kucheki taarifa zenu kwenye ofisi za kata 7-11 august kwa mikoa yote? kama jina liko humo ndo kwa muhimu haya mambo ya mitandao kwa setting zetu sidhani kama yako active sana.

kama mpo Dar au zanzibar nenda kwenye ofisi ya kata bado deadline haijapita.
 
Kwakweli hili ni tatizo na Lisipo angaliwa kwa Makini itaku shida wakati wa upigaji wa kura
 
Nami imegoma aisee sijui kuna kamchezo gani kanaendelea halafu kwa viongozi wa CDM taifa wilaya MVOMERO MOROGORO watu wameongezwa kiujanja na kufikia 18000 wakat maafisa wamehakiki watu wapo wachache tofaut na hyo idadi
 
Back
Top Bottom