ningegusia zote ila naomba niongee kidogo tu kuhusu Treasury bonds ,,wengine wataongelea hizo zingine ..
Wewe naona umependelea ya kila mwezi, kuna njia mbili kuu za kupata mapato kutoka kwa Treasury bond:
Ya kwanza wanaita coupon payments (Riba za Kila Muda), kwa mama ya unapata riba mara kwa mara (kila mwezi, robo mwaka, au mwaka) kulingana na masharti ya bond, muda ukifika unapokea kiasi cha awali (principal).
Mfano kwa wewe,,
Principal (uwekezaji) unawekeza milioni 100,000,000 , Coupon Rate (kiwango cha riba) ni 10% kwa mwaka,,muda wa bond tuseme ni Miaka 5 ,,malipo ya riba ni kila mwezi itakua 833,333/-
Jumla ya riba kwa miaka 5 ni 10,000,000 × 5 = 50,000,000
Jumla ya mapato ambayo utachukua baada ya miaka mitano ni 100,000,000 + 50,000,000 =milion 150.