Wasalaam ndugu wana MMU
Naomba kujua jinsi talaka ilivyo maana naisikia tu..ni kitu gani jamani ni kadi?
hapana talaka sio kadi!
ama maandishi tu yanaandikwa?
Si kila maandishi ni talaka!
Maandishi ni uthibitisho wa talaka!
No! Talaka haiuzwi!
na maneno yanayoandikwa kwenye talaka ni yapi?
Bi mwantope binti sadi, nimekuacha kwa sababu .............!
ningepata wa kunifafanulia maana ya talaka 3 pia ningefurahi
Talaka ya kwanza: ni pale Mume anapomtamkia mkewe, "nimekuacha mke wangu kwa sababu [mfano: haujui kupika! Rudi nyumbani ukajifunze kupika! Or unakiburi: rudi kwenu wakakufundishe adabu! Nk nk!]
Nb: maandiko ni uthibitisho kama kweli talaka imetoka! Ni muhimu kuandika coz kuna ke hawajaachwa, let say kagombana na mmewe, anaamua kurudi kwao na kusema kaachwa, so, maandiko ndio yatathibitisha! Kinyume na hapo ke anaambiwa rudi kwa mmeo! Nb: ni wazazi wacha mungu ndio husema hivyo!
...
Talaka ya pili:
haina tofauti yoyote na talaka ya kwanza except, hii itakuwa ni ya mara ya pili wakati ilie ni ya mara ya kwanza!
...
NB: Talaka ya kwanza na ya pili ni talaka rejea! Ikimaanisha, unaweza kumrudia mkeo kabla ya kumalizika Eda!
Eda ni kipindi/time ya mke kukaa bila mme, kuna eda tofauti tofauti kuzingatia hali ya mke, kwa mfano umemuacha mke na mimba, eda yake itamalizika pale atakapojifungua!
Kwa alieachwa bila mimba ni kabla ya hedhi/period 3, kwa waliakata hedhi/siku zao au wanamatatizo ya hedhi, ni miezi mitatu!
...
Ikumbukwe talaka ya 1 na ya 2 ni talaka rejea ikiwa mume kamrudia mkewe kabla ya kumaliza eda!
...
Ikumbukwe tena, si lazima mume kutamka nakuacha kwa talaka 1 au 2! Hapa kuna mzozo miongoni mwa wanazuoni/islamic scholars!
...
Talaka ya tatu:
Ni talaka isiyorejea! Ikimaanisha, ukimuacha mkeo, hauezi kumrudia mpaka aolewe na mtu mwengine afu aachwe kwa talaka isiorejea! Issue za mahari zinahusika hapa!
au aina za talaka kwa ujumla..
Kuna aina kuu mbili za talaka:
1 Talaka rejea: ni talaka ya kwanza na yapili!
2 Talaka zisizo rejea = ukimpa mke talaka hizi hauwezi kumrudia hadi ufate masharti maalum!
Talaka zisizorejea ni:
1 Talaka 3!
.
2 Dhihar = kumfananisha mke na maharimu (mtu ambae kisheria huwezi kumuoa) wako! Kwa mfano: "nakuona kama mgongo wa mama yangu!" hiyo ni talaka dhihar!
.
3 Talala kabla jimai = talaka kabla ya tendo la ndoa kwa wanandoa!
.
4 Talaka Khul = ni talaka aitoayo Mke!
Dini yangu ya kikristo hairuhusu hili ila ni aibu kwa mwanandoa kutolijua hili.
Asanteni.
NABHANI NIMEKUSAIDIA JAPO KIDOGO!