Msaada kuhusu Talaka

Msaada kuhusu Talaka

nimelipenda swali ameline

talaka sio jambo jema, but si vibaya kufahamu ikoje na hatua zake.
 
Last edited by a moderator:
SLAA3.JPG

Nashukuru sana sana watu8:; hitaji langu umelitimiza.. ndo mara ya kwanza kuiona talaka kumbe ni maandishi tu kama hivi..mimi nikajua ni kama kadi au kitu fulani hivi cha kutisha...hahaha shukrani.
 
Wasalaam ndugu wana MMU
Naomba kujua jinsi talaka ilivyo maana naisikia tu..ni kitu gani jamani ni kadi? ama maandishi tu yanaandikwa? inauzwa? na maneno yanayoandikwa kwenye talaka ni yapi? ningepata wa kunifafanulia maana ya talaka 3 pia ningefurahi..au aina za talaka kwa ujumla..Dini yangu ya kikristo hairuhusu hili ila ni aibu kwa mwanandoa kutolijua hili.
Asanteni.

Ameline, talaka ni tamko kuwa ndoa ya wahusika imefika mwisho! katika mazingira ya dunia ya sasa, matamko hayatoshi, ndio ikaja haja ya kuwa na maandishi!

Mahakamani kuna form maalum ya kujaza kuhalalisha tamko la talaka! ktk uislamu mashahidi pia wanatosha kuhalalisha talaka, then yakafuata maandishi! ktk uislam talaka 1 inamaanisha mke anapewa fursa ya kujirekebisha (hapa ni kama mume ameona kuna walakini kwa mkewe) m.mungu alimaanisha kuwa ktk mazingira ya watu waliozoea kulala pa1, kula na kunywa pa1, kushare mambo ya kitandani kwa miaka na miaka, si rahisi hawa kutengana, hivvo ktk kipindi cha talaka 1, huenda mmoja wapo akajirudi na kumtamani mwenzie, na hii ikawa sababu ya kuokoa ndoa hii (ktk uislam talaka inakufa by default kama mume atafanya mapenzi na mkewe kipindi hiki)

Talaka ya pili itatoka baada ya siku 30 tangu ile ya kwanza (kumradhi kama hii data ina kasoro), talaka ya pili inamaanisha mume ameshikilia msimamo kuwa lazima mke aachike! na hii pia inaweza kumaanisha pia kuwa mke nae amedhamiria kuachika! na hii itadumu pia kwa siku zingine 30!

Talaka ya tatu itatoka baada ya siku 30 tangu itoke ya pili! Hapa sasa ndoa ishavunjika rasmi, hapa inakamilisha siku 90 za talaka! Ameline, wakati huu wa siku 90, m.mungu amemaanisha ni kipindi kizuri kujua kama mke ni mjamzito ama laa kabla ya talaka (kumbuka zama zile technology haikuruhusu kujua ujauzito hata wa miezi miwili), na hii isije kuleta mtafaruku baadae kuhusu baba halisi wa mtoto atakapozaliwa baadae na hasa kama mwanamke tajwa ataolewa na m'me mwingine! wakati wote huu wa miezi mi3, mwanamke anapewa huduma zake zote alizokuwa akipewa kama mke, kasoro huduma ile ya kitandani, mf. chakula, malazi, mavazi, matibabu, huduma za watoto, usafiri mpk kipindi hiki kiishe!

Na kama mwanamke ndiye chanzo cha kudai talaka, huku mume akiwa hana nia ya kumuacha mkewe, shari'a inaruhusu mume kudai mahari yake aliyotumia kumuolea! Na mwanamke anaeachika baada ya talaka 3, hawezi kuolewa na mtalaka wake mpaka mwanamke huyo aolewe na mwanaume mwingine afu aachike, ndio mtalaka wa awali anaweza kumuoa tena, kwa procedures zile zile za kuoana! N a ktk uislamu hairuhusiwi kumuacha mke kwa talaka 3, kisha ukamuomba rafiki yako amuoe (baada ya ww kujutia uamuzi wako) kisha amuache, ili wewe uoe tena, ni haram na ndoa inakuwa batili hapa!

Ameline nimejaribu kudokoa Talaka in islamic perspective, ila kwa mahakamani talaka sio issue, mnaenda saa 2 asubuhi na saa 3.30 kila mmoja ana copy yake ya Talaka! Nakaribisha masahihisho na pia maswali!
 
nimelipenda swali ameline

talaka sio jambo jema, but si vibaya kufahamu ikoje na hatua zake.

ni kweli ndugu..nilikua naumiza akili kuwa na shauku ya kulijua hili jitu talaka ni kitu gani? sasa nashukuru walionisaidia nimeshaelewa sasa..
 
Last edited by a moderator:
Wasalaam ndugu wana MMU
Naomba kujua jinsi talaka ilivyo maana naisikia tu..ni kitu gani jamani ni kadi? ama maandishi tu yanaandikwa? inauzwa? na maneno yanayoandikwa kwenye talaka ni yapi? ningepata wa kunifafanulia maana ya talaka 3 pia ningefurahi..au aina za talaka kwa ujumla..Dini yangu ya kikristo hairuhusu hili ila ni aibu kwa mwanandoa kutolijua hili.
Asanteni.

mbona nahisi km uko kwenye mchakato wa kumtema excel mwenzangu huko?

this is a serious issue... kwanini uwaze talaka lakini?
 
hapana talaka sio kadi!

Si kila maandishi ni talaka!
Maandishi ni uthibitisho wa talaka!

No! Talaka haiuzwi!

Bi mwantope binti sadi, nimekuacha kwa sababu .............!

Talaka ya kwanza: ni pale Mume anapomtamkia mkewe, "nimekuacha mke wangu kwa sababu [mfano: haujui kupika! Rudi nyumbani ukajifunze kupika! Or unakiburi: rudi kwenu wakakufundishe adabu! Nk nk!]
Nb: maandiko ni uthibitisho kama kweli talaka imetoka! Ni muhimu kuandika coz kuna ke hawajaachwa, let say kagombana na mmewe, anaamua kurudi kwao na kusema kaachwa, so, maandiko ndio yatathibitisha! Kinyume na hapo ke anaambiwa rudi kwa mmeo! Nb: ni wazazi wacha mungu ndio husema hivyo!
...
Talaka ya pili:
haina tofauti yoyote na talaka ya kwanza except, hii itakuwa ni ya mara ya pili wakati ilie ni ya mara ya kwanza!
...
NB: Talaka ya kwanza na ya pili ni talaka rejea! Ikimaanisha, unaweza kumrudia mkeo kabla ya kumalizika Eda!
Eda ni kipindi/time ya mke kukaa bila mme, kuna eda tofauti tofauti kuzingatia hali ya mke, kwa mfano umemuacha mke na mimba, eda yake itamalizika pale atakapojifungua!
Kwa alieachwa bila mimba ni kabla ya hedhi/period 3, kwa waliakata hedhi/siku zao au wanamatatizo ya hedhi, ni miezi mitatu!
...
Ikumbukwe talaka ya 1 na ya 2 ni talaka rejea ikiwa mume kamrudia mkewe kabla ya kumaliza eda!
...
Ikumbukwe tena, si lazima mume kutamka nakuacha kwa talaka 1 au 2! Hapa kuna mzozo miongoni mwa wanazuoni/islamic scholars!
...
Talaka ya tatu:
Ni talaka isiyorejea! Ikimaanisha, ukimuacha mkeo, hauezi kumrudia mpaka aolewe na mtu mwengine afu aachwe kwa talaka isiorejea! Issue za mahari zinahusika hapa!

Kuna aina kuu mbili za talaka:
1 Talaka rejea: ni talaka ya kwanza na yapili!
2 Talaka zisizo rejea = ukimpa mke talaka hizi hauwezi kumrudia hadi ufate masharti maalum!
Talaka zisizorejea ni:
1 Talaka 3!
.
2 Dhihar = kumfananisha mke na maharimu (mtu ambae kisheria huwezi kumuoa) wako! Kwa mfano: "nakuona kama mgongo wa mama yangu!" hiyo ni talaka dhihar!
.
3 Talala kabla jimai = talaka kabla ya tendo la ndoa kwa wanandoa!
.
4 Talaka Khul = ni talaka aitoayo Mke!

NABHANI NIMEKUSAIDIA JAPO KIDOGO!

duuu! ndugu yangu Mashxizo sijui niseme nini ila nashukuru sana sana maana nimeelewa kila nilichokua nahitaji asante sana..
 
mbona nahisi km uko kwenye mchakato wa kumtema excel mwenzangu huko?

this is a serious issue... kwanini uwaze talaka lakini?

ni swala ambalo huniumiza kichwa muda mrefu sana sana nikiuliza watu wanapuuza tu sasa nashukuru wadau wote walionifafanulia suala hili..
 
hongera kwa kulifanikisha ameline!

halafu mbona nanusa nusa kama vile uko Arusha? ni kweli ama nimebugi?
 
Ameline, talaka ni tamko kuwa ndoa ya wahusika imefika mwisho! katika mazingira ya dunia ya sasa, matamko hayatoshi, ndio ikaja haja ya kuwa na maandishi!

Mahakamani kuna form maalum ya kujaza kuhalalisha tamko la talaka! ktk uislamu mashahidi pia wanatosha kuhalalisha talaka, then yakafuata maandishi! ktk uislam talaka 1 inamaanisha mke anapewa fursa ya kujirekebisha (hapa ni kama mume ameona kuna walakini kwa mkewe) m.mungu alimaanisha kuwa ktk mazingira ya watu waliozoea kulala pa1, kula na kunywa pa1, kushare mambo ya kitandani kwa miaka na miaka, si rahisi hawa kutengana, hivvo ktk kipindi cha talaka 1, huenda mmoja wapo akajirudi na kumtamani mwenzie, na hii ikawa sababu ya kuokoa ndoa hii (ktk uislam talaka inakufa by default kama mume atafanya mapenzi na mkewe kipindi hiki)

Talaka ya pili itatoka baada ya siku 30 tangu ile ya kwanza (kumradhi kama hii data ina kasoro), talaka ya pili inamaanisha mume ameshikilia msimamo kuwa lazima mke aachike! na hii pia inaweza kumaanisha pia kuwa mke nae amedhamiria kuachika! na hii itadumu pia kwa siku zingine 30!

Talaka ya tatu itatoka baada ya siku 30 tangu itoke ya pili! Hapa sasa ndoa ishavunjika rasmi, hapa inakamilisha siku 90 za talaka! Ameline, wakati huu wa siku 90, m.mungu amemaanisha ni kipindi kizuri kujua kama mke ni mjamzito ama laa kabla ya talaka (kumbuka zama zile technology haikuruhusu kujua ujauzito hata wa miezi miwili), na hii isije kuleta mtafaruku baadae kuhusu baba halisi wa mtoto atakapozaliwa baadae na hasa kama mwanamke tajwa ataolewa na m'me mwingine! wakati wote huu wa miezi mi3, mwanamke anapewa huduma zake zote alizokuwa akipewa kama mke, kasoro huduma ile ya kitandani, mf. chakula, malazi, mavazi, matibabu, huduma za watoto, usafiri mpk kipindi hiki kiishe!

Na kama mwanamke ndiye chanzo cha kudai talaka, huku mume akiwa hana nia ya kumuacha mkewe, shari'a inaruhusu mume kudai mahari yake aliyotumia kumuolea! Na mwanamke anaeachika baada ya talaka 3, hawezi kuolewa na mtalaka wake mpaka mwanamke huyo aolewe na mwanaume mwingine afu aachike, ndio mtalaka wa awali anaweza kumuoa tena, kwa procedures zile zile za kuoana! N a ktk uislamu hairuhusiwi kumuacha mke kwa talaka 3, kisha ukamuomba rafiki yako amuoe (baada ya ww kujutia uamuzi wako) kisha amuache, ili wewe uoe tena, ni haram na ndoa inakuwa batili hapa!

Ameline nimejaribu kudokoa Talaka in islamic perspective, ila kwa mahakamani talaka sio issue, mnaenda saa 2 asubuhi na saa 3.30 kila mmoja ana copy yake ya Talaka! Nakaribisha masahihisho na pia maswali!

Nashukuru sana ndugu yangu slim5 nimekuelewa sana hata sioni swali la kuuliza..hakika JF ni kiboko kiu yangu imekat sasa..
 
aaaah hapo uongo mtupuuu hunioni ng'oo nipo shamba huku nalisha bata mzinga

sasa naona unanichokonoa eenh?

satelite yangu inanionesha kwamba umevaa kama komamdo kipensi!!

bisha!
 
kwetu sisi hakuna kuachana kamwe na hakuna kitu kama talaka brother..kumbe hata kutamka? na ni maneno gani ambayo hutamka btother?

Mfano wa kauli kama kumuambia mkeo au mumeo nimekuacha hiyo tayari ni talaka, pia kumfananisha mkeo na mamaako mzazi au kumfananisha mumeo na babaako mzazi, mfano mtu aaweza sema kuanzia leo nakuona kama mamaangu, basi hapo mutakuwa mumeaachana kwasababu mtu hawezi kumuoa mzazi wake
 
Back
Top Bottom