Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Kwakweli siku zingatia hilo...kwani ndio ilikuwa mara yangu ya kwaNza kufanya kilimo...ila kuna project nyingine naenda kuianza wiki hii nadhani itazingatia vigezo vyote vya vipimo
fe448252a1daeb13b214a2a8adb6ca1d.jpg

Mche hadi mche ni urefu/umbali gani??
Na Mstari hadi mstari ni urefu/umbali gani??
 
Ile picha ya juu ya BEFORE inafanania kama Open Space au Kiwanja cha michezo,
Anyway, ushaanza kupanda, ni wapi huko?? naweza kufanya study tour??
Karibu sana hapo ni kitunda Dar es salaam...
Naanza kupanda kesho Mungu akijaalia...hivyo karibu sana ndugu
 
Poa poa, na water source yako ni nini??
Lipo bomba kati kati ya eneo...uwezekano wa kuchimba kisima hapo ni mkubwa kuna chemchem ipo kina kifupi sana....ila niliona kuvuta bomba nitatunza ardhi japo gharama zitakuwa endelevu kwa supplier wangu wa maji
 
Nilimdikiliza kwa kina mtaalam wa Kilimo kupitia radio anasema kwa mavuno mengi zaidi inashauriwa kupanda mbegu za nyanya moja kwa moja shambani kuliko kuanzia kitaluni.
Je inafaa?
KUPANDA KWENYE KITARU KUNAKUPA UHAKIKA WA MICHE KWA KUWA WAKATI WA KUPANDIKIZA UTACHAGUA MICHE YENYE AFYA....ILA NI VIGUMU SANA KUANGALIA MICHE YOTE UKIWA TEYARI UMESHA IPANDA MOJA KWA MOJA....HIVYO ANGALIA UNACHOONA WEWE INAFAA VYOVYOTE UTAKAVYOAMUA NDIVYO SAHIHI FANYA UKIONA MATOKEO NI MABAYA FANYA KWA KINYUME CHAKE
 
Vipi Kaka,kwa Dar Wap Ntapjta Sehem Wanauza Miche Ya Nyanya F1?
Kwa miche sikushauri ata kidogo watz siku hizi si waaminifu wanaweza kukuuzia miche ambayo huku ihitaji mfano unataka mbegu fupi yeye akupe ndefu au kinyume chake...nunua mbegu na hata kwenye mbegu pia labda utembelee shamba la rafiki yako kisha ukivutiwa na mazao kutoka kwenye shamba la huyo rafiki ndo akuelekeze ukanunue mbegu kama yake
 
Nilimdikiliza kwa kina mtaalam wa Kilimo kupitia radio anasema kwa mavuno mengi zaidi inashauriwa kupanda mbegu za nyanya moja kwa moja shambani kuliko kuanzia kitaluni.
Je inafaa?

Huyo hajielewi na sio mtaalam wa kilimo bali atakua tu mkulima kaulizwa au hata hajui shamba kukoje.
Lazima nyanya ipitie kitaluni sababu utakaposia direct kwanza mbegu utashindwa kuweka kwa spacing stahiki pili huduma kama za,kupiga dawa kitaluni rahisi kuliko shamba zima.
Pia kitalu hupunguza gharama ya kukuza miche kueni makini na elimu za kilimo zinazotolewa holela.
Natamani ningemfahamu huyo mtaalam pumbavu sana watu tunawatoa kwenye primitive stage yeye anawarudisha huko. Hybrid seeds ndio kilimo bora na inauzwa kwa punje sasa ununue mbegu karibu ya laki saba halafu upande direct dah.
Sasa hivi kiujumla ni watu kuhama kutoka kitalu cha chini na kutumia trays sio kurudi backwards
 
Huku kwetu ukitaka mbegu nzuri ni kuagiza kenya angalau wako na uhakika ,soko la mbegu kiujumla limevamiwa sijui labda huko uliko mkuu
nilinunua mbegu ya tikiti maji asali f1 mwanza sitasahau matunzo yangu yalienda bure nilishikishwa mbegu feki sina hamu
 

Attachments

  • 20160103_040248.jpg
    20160103_040248.jpg
    142.2 KB · Views: 78

Similar Discussions

Back
Top Bottom