Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Wanatafiti na kuuza hawana uhakika na mbegu zao(RIjwan),swali la mleta mada limejibiwa na wana nadharia,au wauza mbegu.

Uhalisia ni huu,kama mbegu zilizo shambani ni hybrid majibu yaliyotolewa ni sahihi lakini kama mbegu ulizo nazo ni OPV majibu uliyopewa si ya kweli unaweza kurudia mbegu na zikakupa tija kwa zaidi ya 90%.

Kwa OPV mbegu nzuri zaidi ni mwanga,tengeru(japo wanunuzi wanasumbua kipindi cha uzalishaji mkubwa),Kiboko na Meru.

Mbegu bora zaidi kwa uzalishaji ni hybrid,wengi huzikimbia kwa ukubwa wa gharama zake.Hybrid za nyanya zipo aina nyingi na zinazalishwa na kampuni tofauti.

Kwa uzoefu wangu mbegu bora zaidi kwa sasa (TZ) za hybrid ni Monica,Ashanti na Eden. Zinafuatiwa kwa karibu na kipato,milele na nuru.Kigezo changu cha ubora ni ukubwa na kuvutia walaji kwa tunda husika na ustahimilivu sokoni.

Kwa tija zaidi wasiliana na wakulima usihangaike na wataalam wa nadharia Ofisini au wauzaji wa mbegu,watakupoteza,
Boss hapo kusema Rijk zwaan wanatafiti na kuuza hawana uhakika na mbegu zao umechemka mkuu, Rijk zwaan ndio kampuni pekee Tanzania na Afrika mashariki na kati ambayo inazalisha mbegu zake hapa hapa nchini ndio maana inamatawi matatu Q sem, Afrisem na Mararua. Wao wanatafuti na kufanya breeding hapa hapa Tanzania ndio maana mbegu zao zinafanya vyema sana nchini, kampuni nyingine zote wanaagiza mbegu iliyozalishwa haswa China wao wanakuja kufanya trials kama inakubali nchini wakiona inafaa wananunua kwa mzalishaji na kufanya packing na kuuza, ndio maana ni jarrah rz mbegu ya rijk zwaan ya nnje (open field) ambayo kwa eka moja inakupa crate 1000 ukiitunza vyema, nyingine zote ziko chini ya crate 500 kwa eka moja
 
Mkuu nna swali hapa!

Assila f1 ni semi determined au??

Assila naweza lima kipindi cha mvua??
Assila ni semi determinate, kuhusu msimu mostly tatizo huwa maji mengi ardhini
So kuamua ipi inafaa kwenye mvua au lah inategemea na udongo wako maana nyanya ya kwenye kiangazi Arusha ikilimwa kipindi cha mvua Dsm itafanya vyema sana sababu kuu ardhi maji hayakai sana dsm kulinganisha na Arusha
 
Ni mbegu ipi inayorefuka hadi mita nane ili iwe chaguo langu, halafu kilimo chagreen house lazima umwagiliaji uwe wa droplets? Maaada jamani
Ziko nyingi ila mfano mchache Monteazul, Valouro etc (rijk zwaan), victory f1(east west), anna f1 (sina hakika kampuni gani), kikubwa tafuta any variety ambayo ni indeterminate.
Green house ni lazima kutumia drips sababu cost ya Green house si chini ya milioni sita so tunahakikisha hakuna risky yoyote so kunyesha kwa mfereji ni risk sana kwa kusambaza magonjwa ya ardhini hususani mnyauko which is the less thing utaomba ukutano nayo kwenye Gh maana unaweza shindwa kabisa kuzalisha kwa kutumia udongo wa kawaida.
4b4f836a889c85394cf0d4e45213dd91.jpg

Hapo juu udongo una mnyauko imebidi kutumia mifugo na media maana ardhi haifai kwa kilimo cha mazao jamii ya nyanya
 
Kama ni F1 yaani Hybrid lazima kila msimu ununue sababu ukiirudia unaenda kwenye F2 sasa kwa waliosoma genetics kidogo wanafahamu ,ukiwa kwenye F2 utapata wachache wenye sifa za parents ila wengine watakua na sifa zilizojificha (zisizotakiwa) kama vile kutovumilia magonjwa ,kutoa mavuno kidogo,kua na nyanya ndogo etc hivyo kama unanunua F1 ya zao lolote jua kwa ubora wa mavuno usirudie mbegu ila kama unacheza bahati nasibu rudia .
Tazama jarrah f1 hiz sifa zake ,ukiirudie mbegu hizo sifa zinaondoka
Mkuu hapo sijakupata.. unamaanisha kama msimu huu ulilima ANNA F1.. msimu ujao usilimie tena hiyo ANNA F1. Ulime mfano EDEN F1. Coz ukilima ANNA F1 itaenda kwenye F2? Naomba ufafanuzi.
 
Zinazotolewa matawi ni nyanya fupi ambazo hurefu hazizidi mita 1.5 sasa kwa matunda huzaliwa kila baada ya cm15 au 20 (std) hivyo ukitoa matawi kwa mche wa kurefuka 1.5m inamaana itakua na vichane 6 tu ,ukiacha matawi inamaana kila tawi likikua vichane 6 ikiwa matawi manne tu unachane roughly 24,kila kichane kikiwa na matunda manne hapo ni matunda 96 (kg 12 roughly per plant)
Kwa nyanya ndefu inakua tu haina mwisho hivyo utavuna mpaka useme basi maana inafika mpaka mita 8 .
Kwahiyo mwenye nyanya fupi akitoa matawi kapunguza mavuno ila mwenye nyanya ndefu anatoa matawi abakiwe na moja au mawili atakayoeza kuyahudumia vyema .

Nyanya fupi inaitwa fupi sababu kuna urefu ikifika inaweka matunda ya mwisho
Mkuu asante kwa maelezo mazuri.. je Eden F1. Ipo kwenye kundi la nyanya ndefu zaidi ya 1.5m... maana niliponunua mbegu niliambiwa ni nyanya ndefu na sikua aware kuuliza inafika mita mangapi.. naomba ufafanuzi mkuu..
 
Mkuu hapo sijakupata.. unamaanisha kama msimu huu ulilima ANNA F1.. msimu ujao usilimie tena hiyo ANNA F1. Ulime mfano EDEN F1. Coz ukilima ANNA F1 itaenda kwenye F2? Naomba ufafanuzi.

Kuna watu wanafanya local seed extraction kwa kiswahili kuzalisha mbegu but wakulima wanatumia sana neno kukamua,mtu akinunua mbegu leo kesho anatoa za shamban anarudia
 
Kuna watu wanafanya local seed extraction kwa kiswahili kuzalisha mbegu but wakulima wanatumia sana neno kukamua,mtu akinunua mbegu leo kesho anatoa za shamban anarudia
Asante mkuu hapo nimekupata.. nimeuliza pia Eden F1 ipo kwenye kundi la nyanya ndefu zaidi ya mita1.5 au? Maana niliponunua mbegu waliniambia ni ndefu. Ila sikuuliza ni erefu kwa kias gani.. nitashukuru ukinipatia ufafanuzi. Natanguliza shukrani.
 
Mkuu asante kwa maelezo mazuri.. je Eden F1. Ipo kwenye kundi la nyanya ndefu zaidi ya 1.5m... maana niliponunua mbegu niliambiwa ni nyanya ndefu na sikua aware kuuliza inafika mita mangapi.. naomba ufafanuzi mkuu..

Eden ni semi determinate,iko between 1m to 1.5m. Ni ya kupanda nnje hii mbegu ila muhimu ujipange kufungia urefu plus hizi mvua usipofugia umehalika hasara kubwa sana
 
Umenielimisha sana mkuu.. nimefanya big mistake nilikua naondoa suckers.. ila nimejifunza sana.. next time sitarudia kosa.. nyanya zimeanza kuzaa..View attachment 711504

Usiwe unatolea kwa hizi nyanya fupi badala yake unatoa tu majani ya chini kabla ya tunda la kwanza ili isiwe bush sana kukaribisha magonjwa na pia ili majani ya chini yasiguse ardhi na kupandisha magonjwa

IMG_3727.JPG
IMG_3729.JPG


Hiyo nimetoa tu majani ya chini sijatoa tawi lolote na matunda hayo heavy tu
 
Ahsante mkuu.

Kwa ushauri wako ni wapi nitakapopata duka lenye naweza kupata mbegu hizo kwa usahihi mkuu.

Natanguliza shukran.

Kwa dsm sio mwenyeji bahati mbaya mkuu,ila vyema upate duka la kampuni husika yaani ulizia duka la east west seed au kama ni rijk zwaan mpaka uwasiliane nao wao watakutumia mbegu huliko kwa gharama zao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom