Msaada kuhusu mashine za kutoa risiti kwa mauzo/manunuzi

Msaada kuhusu mashine za kutoa risiti kwa mauzo/manunuzi

Mystic

Senior Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
150
Reaction score
37
Salaam wanajamii!
Nimetumia mashine ya Datecs, kwa bahati mbaya nimeuza katika mashine zaidi sana ya kiwango halisi (Ni zaidi ya mauzo ninayoweza kufanya kwa mwezi). Nahitaji ufumbuzi katika hili; Nifanye nini / nimuone nani ili kufuta hayo mauzo?
 
Kama ipo connected na TRA huwezi futa ndo maana wanalazimisha kutumia hizo machine, na pili kwa nini ufute, hutaki kulipa kodi halali ya serikali?
 
Wasiliana na helpline ya tra wakupe ufumbuzi. Ipo kwenye website yao.
 
NInavyoelewa jamaa hataki kulipa kodi siyo kwamba machine mbovu 🙂

Nadhani kakosea kubonyeza, kwa mfano badala ya 50,000 kaandika 500,000. Hapo utaratibu unasemaje?
 
Nadhani kakosea kubonyeza, kwa mfano badala ya 50,000 kaandika 500,000. Hapo utaratibu unasemaje?
Nafikiri unaweza override transactions kama zimeingizwa kimakosa ila record bado itakuwapo kwenye machine. Nimeona hii mfano kitu kimewekwa kwenye sale na unapolipa unauziwa bei ya zamani kabla ya sale, kinachotokea manager/au mtu mwingine lazima aje ku-override ile transaction. Ila kuhusu jamaa naona anataka machine nyingine kwa vile amefanya biashara kubwa kwa siku moja na hivyo panga la TRA ni kubwa vile vile.
 
Ku-override kivipi? kama ameshatoa riceipt na ikaonesha "legal receipt" hakuna njia ya kufuta hayo mauzo. Mkuu Mystic unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na TRA, uwe na nakala ya Z report yako, kama umekosea kwa bahati mbaya haina haja ya kupanic, kwa maelezo zaidi wasiliana na supplier wa hiyo mashine akupe taratibu za kufuata! Kama uliuziwa na TFS niinbox.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom