Msaada kuhusu leseni ya gari

IrDA

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
743
353
Nna leseni class D,je kupata class B lazima nikafanye testing upya? au ni taratibu gani nnazotakiwa kufuata?

Wadau baada ya kutafutatafuta kwenye website ya TRA hatimaye nikapata ufafanuzi,naomba nishare hapa kwa ambao pia walikuwa wanatatizo kama langu.

B – License to drive all types of motor vehicles except motor cycles, commercial, heavy duty and public service vehicles.

D – License to drive all types of vehicles except motor cycles, heavy duty and public service vehicles

Kutokana na maelezo hayo hapo juu nikafahamu kuwa,mtu mwenye daraja D haitaji kuwa na B.Bali mtu mwenye daraja B anaweza kuomba kupata daraja D ili aweze kuendesha magari madogo ya kibiashara.
Kwa maelezo zaidi jinsi ya kuongeza daraja la leseni na kupata leseni mpya unaweza ukapitia hapa
http://www.tra.go.tz/index.php/2012-11-20-06-37-07/159-what-are-the-categories-of-driving-licenses

Shukrani kwa wote walionipa maelezo ya awali
 
Unamaanisha kwa mfumo mpya? Sidhani kama unaweza kuwa na D bila kuwa na B.

D - Commercial Light Duty (Pickup)
B - Private Vehicles (Magari yote madogo (Saloon,4x4 etc) kasoro pikipiki)

So hauwezi kuwa na license D bila kuwa na B.
 
mi nnayo Leseni ya pikipiki ya Zanzibar, nataka nichukue ya huku nichanganye na ya gari....kuna mchakato gani hapo??
 
Unamaanisha kwa mfumo mpya? Sidhani kama unaweza kuwa na D bila kuwa na B.

D - Commercial Light Duty (Pickup)
B - Private Vehicles (Magari yote madogo (Saloon,4x4 etc) kasoro pikipiki)

So hauwezi kuwa na license D bila kuwa na B.

Mkuu ni kwa mfumo mpya,je taratibu gani nifuate kupata B?
 
Mkuu ni kwa mfumo mpya,je taratibu gani nifuate kupata B?

Umepataje D mpya bila B? Mimi nilikuwa na ile ya gari ya kawaida ya zamani, nikapewa B & D moja kwa moja.

Pia walitangaza kuwa muda wa kubadili leseni unaisha april 30 so unless wameongeza basi inabidi uanze upya kabisa, kama vile haujawahi kuwa na leseni.
 
Mbona mimi nina D na sina B? Kwani tatizo ninini
 
Nna leseni class D,je kupata class B lazima nikafanye testing upya? au ni taratibu gani nnazotakiwa kufuata?

Mkuu kwa class D si unaruhusiwa kuendesha magari yote madogo yasiyokuwa ya abiria (kibiashara) na magari ya mizigo ambayo hayazidi tani 3.5,sasa class B ya nini tena wakati magari ya class B yamekua included on Class D license?
 
utaratibu saiv inakuwa kama unaanza upya hata kama huta testiwa lakin ada ya kutestiwa lazima utoe pia ada ya learner kwa kila class kwa mfano A,B,D,E utatoa 40,000/= hii ni learner fee tu then lesen yenyewe ni 40000/= ukijumlisha inafika kama laki hivi..
 
Mimi nina class a,b na d,class B ni ya magari madogo kama carina,rav 4 na mengine kama hayo,na A ni kwa ajili ya pikipiki,D ni magari yote isipokuwa ya mizigo mikubwa,apa hat class B ipo sasa,D unaweza endesha prado,pickup na magar ambayo yanabebe tan isiyozid tano,leseni yenyewe nilipata ki magumashi mwaka jana
 
Mbona mimi nina D na sina B? Kwani tatizo ninini

Swali ni uliipataje D peke yake maana kimantiki haina maana kuwa na D bila kuwa na B pia.
Ulikuwa na leseni ipi ya zamani?
B & D zinaenda pamoja kwenye system mpya.
Technically hakuna tofauti class zote mbili zinaruhusu magari madogo yote, ila kama haipo kwenye license lazima traffic watakusumbua.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom