Msaada kuhusu kuwithdraw mfuko wa PPF baada ya kuacha kazi

Msaada kuhusu kuwithdraw mfuko wa PPF baada ya kuacha kazi

Kind

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
247
Reaction score
40
Wakuu naomba msaada wenu. Napenda kujuzwa taratibu za kuwithdraw toka ppf baada ya kuacha kazi, pia inachukua muda gani kupata hayo malipo. na pia je ukisha chukua malipo unaweza kujiunga tena utapo pata kazi nyingine?

Ni ofisi zao zipi zinashughulikia swala la kuwithdraw? na itachukua muda gani kujiunga tena?
 
Unatakiwa kuwa na barua ya kuachakazi au ya kumalizika na mkataba baada ya hapo utaenda ofisin kwao watakupatia fomu ambazo utajaza baada ya hapo utazipeleka kwa mwajiri wako atakusainia thn utazirudisha ppf. Ndani ya wiki mbili mpaka Tatu unapewa check yako. Pia unaweza kuendeleza michango yako kwa mwajiri mpya unampa mwajiri wako namba yako ya uwanachama michango inaendelea kuingia
 
Kwanza kabisa uwe na barua ya kuacha / kuachishwa kazi, passport size 3, kadi yako ya uanachama nenda tawi lililokaribu nawe watakupa fomu utajaza kisha utapeleka kwa aliyekuwa mwajiri wako atasaini na kugonga muhuri then utarudisha ppf. Fao hutoka ndani ya wiki 2,3 kama hakuna kasoro.

Muhimu: waweza jiunga online upate taarifa ya miamala ya michango yako ili ujue kama imeingia yote mpaka mwezi wa mwisho wewe kukatwa katika mshahara wako ama waweza omba wakuprintie.
Karibu.
 
Du hawajamaa nimeprocess ila ni mwezi sasa hamna majibu
 
mm kwa mfano nlijiunga na kampuni ya mwanzo bt niliacha kazi ghafla baada ya kutoelewan na mwajiri wangu so sikuchukua documents zozote bt nkapata tena kazi kampuni nyngne nkampa mwajiri mpya namba yangu ya uanachama wa ppf anaendeleza michango yangu humo je siku ya kwenda kufatilia mafao yangu ntatakiwa kwenda na barua zote mbili za kuachishwa kazi au moja tu ya hii kazi mpya maana nataka niiache kwa kufata taratibu. msaada pls
 
Back
Top Bottom