Msaada kuhusu kupima DNA

Ukigundua kaka yako au mtoto wako wa kiume amebambikiwa mtoto unaweza kumpa huu ushauri?
 
Pole sana ndugu yangu wamekutesa sana Kisaikolojia.

Huyo Mwanamke alijua kabisa unapenda watoto akashikia hapo hapo
 
Kosa lilianzia hapa
 
Mambo ya kuhendekeza ujinga haya.
 
huyo hakuwa mke wake mbona unashindwa kuelewa kiswahili.
 
Gharama ni affordable lakini ni mchakato mrefu. Mtatakiwa kuanzia ustawi wa jamii huku mtasuluhishwa, ikishindikana kabisa mtaenda polisi kuna dawati la jinsia uko mtasuluhishwa pia, ikishindikana tena mnaenda mahakamani ambapo mtapewa kibali cha kupima dna then ndio mnaenda kwa mkemia wa serikali.

katika huo mchakato mwanamke akikataa kupima dna basi vipimo havifanyiki ni lazima mama mtoto akubali, kwaiyo anaweza kukwambia mtoto sio wako lakini katikati ya mchakato wa kupima dna akabadilika kwaiyo mchakato unaishia hapo.

Vile vile DNA za bongo ni za mchongo, lazima majibu yatasema mtoto ni wako hata kama sio wako. Wamasema wanalinda masilahi ya mtoto.

Cha kufanya: kama uwezo unaruhusu chukua sample zako na mtoto kapime DNA hapo Nairobi, Kenya. Kule hawana longolongo na kama sio mtoto wako wanakuambia tu hapo hapo
 
Mkuu ulipohudumia mpaka mtoto kua salama ni hatua nzuri tu.

Cha kufanya ni vizuri ukapima DNA ukaujua ukweli japo kuna maneno maneno kua dna za bongo michongo mingi kukwepa watoto wa mtaani sijui mtoto kuteseka na mambo kama izo ila ni bora ukawa na uhakika wa kidaktari.

Kama dna huiwezi bas amini tu huyo mtoto sio wako.
 
Mkuu umeshauri vizuri hasa kipengele cha kusema asiamini chochote kutoka kwa mwanamke aliyemtekeza mtoto. Ila sasa kuna upande mwingine. Kama siyo wake na huyo baab halisi akaja jitokeza siku moja na kumdai itakuwaje? Mimi nadhani ni vizuri kabisa mambo yakawekwa sawa tangu sasa. Hata kama siyo wake na anataka kumlea, basi afanye mchakato ili ijulikane na kusiwe na mgongano baadae.
 
Busara kubwa sana hii!
 
Kitu cha kwanza kabisa mimi huwa naamini mtoto mara nyingi ni lazima ata-copy ufanano wowote kutoka kwa mzazi hata kwa kiasi kidogo. Huyo ukimwangalia unadhani kuna kitu mnafanana? Na huyo mwanamme mweingine je, kuna kitu wanafanana?
 
Njia nzuri ya kumshinda adui ni ku respond tofauti na alivyotarajia. Sasa huyo mwanamke matarajio yake ni kukuvunja moyo uachane na huyo mtoto. Wewe endelea kumhudumia bila kujali, hata kama si wako endelea hadi pale utapojihisi una amani kuishia hapo.
 
Nashukuru
 
Nashukuru
 
Mu addopt tu awe wako bila haja yya dna.na kikuuliza mpe uthibitisho ni wako.
Siku raha za mijegesho ikiisha huko atarudisha msambwanda wake
 
Umesema kwel
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…