Msaada kuhusu kupima DNA

Huyu mtoto ni wako.
1. Kama adingekuwa wako hangekuachia akaondoka.
2. Alijua utakwama lakini kwa mafanikio makubwa ulipata busara ukamlea kupitia mkweo na mtoto kawa mkubwa. Inamuuma.
3. Mkeo hana tofauti na muuaji, alitegemea mtoto angekushinda kumlea ili umpigie magoti.
4. Huko alikoenda amekwama kila kitu akaona amgeukie mtoto ili akuumize zaidi lakini ulifanya jambo zuri kumkabidhi mtoto kwa mujibu wa taratibu na sheria.
5. Kuna alichokitarajia kwako akaamua kuolewa sasa alikikosa akaamua kumrudia ex wake, hawa wawili lao moja.
6. Fanya ujasusi wa kumhusu ex wake. Fanya utafiti Je ana watoto? Kama anao wangapi? Ajiri mwanamke kijasusi hata ajifanye house girl akawapige picha watoto wake ufanye ulinganisho wa sura zao na huyu mwanao.
7. Ili ujue ni kweli ndiyo sababu ya yeye kukwambia mtoto ni wa ex wake.
8. 99% to 101% mtoto ni wako Kama sivyo mama yake angeliungana naye kwani tangu ujauzito wake wanawake hunong'ona na mama zao ila huyu hakuwai kufanya hivyo kwasababu hakuwa na sababu ya kufanya hivyo. Mtoto ni wako usijiumize nafsi yako.
9. Rudi nyuma kipindi cha mimba changa huyu mkeo alikuwaje? Je alikuwa mtu wa kutokatoka kabla ya kupata ujauzito? Je baada ya kujifungua sababu kuu ya kukuachia mtoto ilikuwa ni ipi. Na Kama ikiwezekana weka hapa chanzo cha mtafaruku hadi akamuacha mtoto sababu kubwa ilikuwa ni ipi.
10. Napenda kukusisitizia kuwa mtoto ni wako ila huyu mkeo anajua kuwa MAPENZI YAKO MAKUBWA NI KWA HUYU MTOTO SASA ILI AKUUMIZE AKAAMUA KUTAMKA HUO UJINGA. Huyu siyo wa kumrudia kamwe atakuua.

Mwisho type marejesho.
 
Mkuu kama gharama ni 150k naweza kupambna kidogo kidogo nkaipata niko Moro mjini inamana wanapima hospital za kawaida au kuna hospital maalum nsaidie kwa hilo kama unajua pia.
Hawapimi Hospital.....!

Kwa Dar es salaam, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ndo Huwa inapima....!

Office zao zipo jirani na Ocean road.
 
Gharama ya DNA ni Wastani wa 150,000.....!

All in all kila kinachotokea Kwa Binadamu kina sababu.
Ipo sababu Kwa Nini umeachana na huyo Mwanamke.....!
Pia ipo sababu Kwa Nini umeletewa huyo Mtoto na Mungu ili Umtunze...!
Achaa kuongopa,Mungu hajamleta huyo mtoto kwa jamaa, ni mwanamke ndiyo kamleta huyo mtoto kwa jamaa! Tuwe wakweli, Jamaa ana haki ya kujua kama kweli huyo ni mtoto wake au laa, maana kuna Baba mwingine nae katajwa kwa huyo mtoto!!
 
Madaktari wanaopima DNA wameruhusiwa kutoa majibu ya uongo ikiwa ataona inafaa!,hiyo ni kwaajili ya mtoto apate mahitaji yake nakueupusha watoto wa mitaani.
kama utahitaji majibu ya kweli kabisa nafikiri itakubidi utumie fedha zaidi,
Hivyo ndugu kaa ukijua dunia haipo kwaajili ya sisi wanaume, yani dunia kwetu ni ubaya ubwela...🤣
 
Naunga mkono. Yaani unapunguziwa mzigo unakataa
Yani nishatumia gharama kumlea ikiwa sio wangu huoni haja ya mimi kulipwa, mana ukiachilia mbali matumiz ya kila siku nlishlipa sh. Laki tatu ya makosa ya kumpa mimba binti yao yan kuna mambo mengi ata kuandika nakosa nguvu
 
Umeongea poa sana yan
 
Da nimekusoma mkuu ila nlishapigwaga na faini ya kumpa mimba binti yao sh laki tatu hiyo ni nje na matumiz ivi vitu vinaniumiza akili sana bas tu ndoivo maisha yenyew magumu tu
 
Kiufupi
Sikulea mimba ila aliniletea mtoto na kusema ni wangu.

Nlipomuuliza mimba umeleaje pekeako na hukunambia akasema aliolewa na mme mwingine ambae alikataa kuwa mtoto sio wake kwakuwa muda waliokaa inaonekana mimba ilitangulia kabla ya ndoa

Nkamuangalia mtoto nikaona ni kama nafanana nae na mtoto mchanga mi mwanaume siwez kufananisha sana ila nkaanza kumlea tangu hapo.

Nlipokubali kumlea wazaz wake ndo wakaniita kuwa nilipe fidia kwa yule alielea mimba nakuongeza kuwa yule mwanaume anawalaumu kumuozesha mke ambae alikuwa na mimba.
Sikuhoji kitu nkalipa sh laki tatu ambazo nlitakiwa kulipa huku nikiendelea kumlea mtoto.

Sasa mtoto alizaliwa akiwa mikonon mwa uyo mme wake na majina anayotumia clinic ni hayo hayo jina nlilompa linatumika tu kwenye kumuita. Sasa hata kubadili jina kwenye kadi kwa muda wote kuanzia mama yake na bibi yake wote hawakubadili wanasema kubadili jina ni ngumu ( binafsi sielewi)

Sasa badae ndo mapichapicha mara mtoto sio wako mara unajisumbua kulea mtoto sio wako mara mtoto ana kadi tatu uyo we jisumbue tu.

Sasa nikae kimya vip gharama zangu?
Au niache kulea vip ikiwa ni damu yangu afu akawa anateseka, hapo ndo naumia
 
Achaa kuongopa,Mungu hajamleta huyo mtoto kwa jamaa, ni mwanamke ndiyo kamleta huyo mtoto kwa jamaa! Tuwe wakweli, Jamaa ana haki ya kujua kama kweli huyo ni mtoto wake au laa, maana kuna Baba mwingine nae katajwa kwa huyo mtoto!!
Kwel kaka
 
Da
Daah kwa Scenario Hii Umepigwa Nyumbani na Umepigwa Ugenini, Tena Cleansheet hii
 
Mawasiliano na huyo Mwanamke yalitakiwa yakatike toka alipokutelekezea mtoto
Yalikoma siku hiyo hiyo ila kila kukicha ananitafuta kwa namba mpya na kero zipo constant. Nshablock namba zaid ya nane na bado atakutafuta tu
 
Nashukuru angalau umefanya nitabasamu, ubaya ubwela
 
Yalikoma siku hiyo hiyo ila kila kukicha ananitafuta kwa namba mpya na kero zipo constant. Nshablock namba zaid ya nane na bado atakutafuta tu
Endelea kupiga block huyo! Kakubambikia mtoto mpumbavu sana huyo mwanamke! Achana nae Dalili za mvua ni Mawingu Sasa kama unataka mvua ya mawe ikunyeshee endelea kuweka mazoea nae!
Wanawake wanaweza kukuharibia future yako hivi hivi. Kuwa makini sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…